Watanzania dunia itawacheka mkiwapa upinzani nchi - JK Nyerere

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067

Nukuu isiyo rasmi

''Eti mnataka kuwapa nchi CHADEMA kwa majaribio. Majaribio nchi nzima? Wapeni hata mkoa kama mnataka majaribio.. Vyama vingi vya upinzani vipo kwa ajili ya Ruzuku. Hutaviona kwenye uongozi kwa kuwa viongozi wao wote wapo kwa maslahi..''

Hayo ni maneno ya muasisi wa taifa, Mwl JK Nyerere. Nimekumbushia tu!
 
Hayo ya miaka mingi iliyopita. Alisema Dar haiwezi ongozwa na upinzani mbona sasa hvi upo chini ya upinzani. Mabadiliko yapo tu na huwezi kuyazuia.

Hoja mezani ni yanayotukabali sasa hvi. Mwenge uendelee kupoteza mamilioni ya watanzania wakati hizo pesa tunazihitaji kwa maendeleo ya mtanzania.

1. Watanzania hawana hospital na zahanati vijijini. Wamama wajawazito na wengi wanapotez maisha kila siku kwa kukosa huduma za afya then tuendelee kuishi kwa hotuba na usanii kwenye mwenge. Kwa nini hz hela zisikajengee vituo vya afya vijijini?

2. Hospitali nyingi hazina dawa na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya. Bado tunganganie kupoteza mamilioni ya hela kukimbiza mwenge.

3. Wapo watoto wengi wa masikini vijijin na baadhi ya miji hawana madarasa ya kusomea na hata walio na madarasa hawana madawati ya kusomea. Bado watu waendelee kutetea nadharia ya kukimbiza mwenge kuwa ni maendeleo.

4. Shule nyingi hazina vitabu na vifaa vingine kwa ajili ya kuendeleza elimu yetu. Elimu.ndo mkombozi mkubwa kwa taifa. Kama ilivgokwisha kuanishwa ujinga ni adui wa mtanzania. Hatuwezi kuondoa ujinga kwa kukimbiza mwenge tunatakiwa kuinvest hela nyingi kwenye elimu. Kwanini tuendelea kupoteza hela kukimbiza mwenge wakati tunaweza kutumia hiyo hela kuinua elimu yetu?

5. Wapo wanafunzi wengi wenye uwezo wa kiakili wa maskini lakini wanakosa kujiunga vyuo kila mwaka kwa kukosa ada. Kwanin hii hela isiende katika fungu la kuwasaidia na kundi hili linalokosa elimu?

6. Miundo mbinu mingi haijakaa vizuri. Hizo hela zinaweza kujenga barabara kadhaa lami katika mikoa mojawapo Tz. Why tupoteza hii hela bila msingi wowote?

7. Tanzania sasa hvi haina ndege hata moja. Hii hela nina imani inaweza angalau ikanunua hata ndege moja au mbili. Kwa miaka mitano kama tukiamua kuinvest hii hela sehemu.moja tuseme kwenye Aviation industry baada ya miaka mitano tutakuwa mbali sana. Baada ya miaka kumi tukifanya tadhimini hela ambayo tumewekeza kwenye Industry kama hii tutakuwa mbali sana. Na tunaweza kuwa na kitu cha kujivunia tofauti.na kupoteza hela bila mpango wowote.

Kwa nini Watanzania tusiwaze kama watu waliokatika ulimwengu unaenda kwa kasi kubwa sana ya maendeleo. Tusiwaze kama watu walio katika miaka 1961 ya kupata uhuru. We are in another era that needs changes of minds. We real need to think out of the box. Tusifungwe na sera ajabu ajabu.

Tumkubali Mh Magufuli maana anafanya maamuzi ambayo kweli mengi ni katika kutuondoa katika mfumo wa kuwaza kizamani zamani tu. Viongozi wanakuwa na sera za kizamani ambazo hazimkomboi mtanzania.


Tuache siasa za porojo za kizamani. Tuangalie namna ya kulikomboa taifa letu na umasikini uliopiga kutu.
 
Alikuwa sahihi, majaribio yamefanyika Moshi, Arusha, Mwanza na pote huko kuna maendeleo makubwa sana.

Ni wakati sasa Lindi, Mtwara, Tabora, Ruvuma waamke na kuchagua upinzani !
 
Nyerere alikuwa na mapungufu pia, usitulazimishe tuanze kuyatoa mapungufu yake hapa, mwache mzee wa watu apumzike
 
Wakuu mlisoma mpaka mwisho? Niliandika, 'Nimekumbushia tu'.
Mbona mnakuwa wakali!?
 
Mwenyewe alikili... alikuwa na mazuri yake na mapungufu yake... kama yeye ndo aliruhusu vyama vingi baada ya 80% ya watz kukataa.... kwa kauli hiyo basi hayo ni katika mapungufu yake... anadhani dot com generation, watoto wa miaka ya 90 wenye haki ya kupiga kura watafikiria kama yeye mtu wa mwaka 1922? Changes are inevitable na ndo maana wakulu hawataki INEC... NEC kwao ndo habar ya mjini...
 
Inaelekea u kijana akili yako imezeeka au unazeeka vibaya you are soooooo yesterdays kukumbushia ujinga wa mtu aliyejenga msingi mbovu uliotufikisha hapa na kusbabisha nchi kuwa na wajinga wapumbavu na masikini kama wewe.
 
Nyerere sio Mungu, kwamba akisema yeye ndo basi, watu wengi sasa wamesoma kuliko yeye, watu sikuizi wana upeo na strategies nyingi kuliko yeye na wameprove hilo, mambo yanabadilika kila sekunde ya dunia hii, yeye kwetu ni baba wa taifa alifanya mambo mengi mazuri kwa wakati wake kulingana na mazingira yaliyokuwepo, sasaiv dunia iko tofauti, kuendelea kufanya referenceya maneno aliyoyasema tena kwenye kampeni huku ukichukua maneno ya mwanzo ukaayacha yale ya mwisho, ukijua watu wengi hawatafungua video, au hawataangalia yote ni kumdhalilisha huyu mzee. Hebu tumuache huyu mzee apumzike tusimuingize kwenye hasira watu waliyonayo juu ya ccm.
 
Mwalimu Nyerere kweye hiyo clip kaongelea matusi badala ya mtu kujenga hoja. Mpaka leo hii jamiiforum matusi ni kama chai ya asubuhi na chakula cha mchana, baadhi ya watu hawawezi kujibu hoja kwa kutumia hoja, wao wanajibu kwa kutegemea matusi.
 
Hii umeikuta kwenye maktaba ya Jecha??
 
Inaelekea u kijana akili yako imezeeka au unazeeka vibaya you are soooooo yesterdays kukumbushia ujinga wa mtu aliyejenga msingi mbovu uliotufikisha hapa na kusbabisha nchi kuwa na wajinga wapumbavu na masikini kama wewe.

Mjinga, mpumbavu na masikini mwenyewe!
 

Mleta mada mbona umemuamsha Mzee wetu toka usingizi wa milele. Hiyo ilikuwa 1995 leo tuko karne nyingine na yeye hayupo.

Alimkataa JK mwenzie lakini alikuja kutawala, KWA HALI HIYO YALIKUWA MAONI YA WAKATI HUO SI YA MILELE
 
Hapo nyerere alijaribu kuzionyesha hisia zake kwa sauti coz uwezi azisha duka na kuwa unawasukuma wateja duka la jirani CCM ni duka la nyerere so lazma alitafutie wateja in positive way on negative.... Lakini Humphrey polepole u-dc utaupata tu tulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…