Neno Swahili,ni neno la kiarabu,maana yake pwani.Waarabu ndio waanzilishi wa lugha hii baada kufikia Pwani ya Afrika ya mashariki,na kuchanganya damu na wenyeji wa maeneo hayo.
Ndio maana lugha hii ina maneno mengi ya kiarabu,japo yapo maneno ya kibantu na kihindi na kijerumani,na utamu wa lugha hii,azungumze mtu wa Pwani,aliyezaliwa na kukulia Pwani ya bahari ya Afrika mashariki.
Kwa hiyo twaweza kusema lugha hii ni ya watu waliochanganya damu ya kiarabu na ya wenyeji wa Pwani,wakapatikana waswahili.Kwa kenya maeneo ya Pwani,kabila la waswahili lipo,hasa maeneo ya Mombasa.
Waswahili wanatamaduni zao,mila na desturi zao.Na wanapozungumza lugha hii,wanaizungumza kifasaha sana,kuliko akizungumza asiye mswahili.Lugha hii ni tamu na nzuri,akizungumza mswahili mwenyewe.
Hawa hawa waswahili(damu ya kuchanganya,baina ya waarabu na wenyeji wa pwani),ndio waliineza lugha hii,mpaka katika nchi ya kiarabu ya Oman,ni lugha ya pili kwa kuzungumzwa na watu baada ya kiarabu.Maajabu yaliyoko huko Oman,kuna watu hawajui lugha ya kiarabu,lakini wanazungumza kiswahili.