Void ab initio
JF-Expert Member
- Mar 1, 2015
- 5,720
- 5,659
Katiba ipi ile ya Chenge au???Sijui kwa nini wanaharakati wanasema katiba haikupatikana wakati kilichosalia ni kupiga kura tu. Chadema wanafikiri wao wasiposhiriki ndio basi kitu fulani sio halali. Wakati kura zao bungeni hazitoshi kwa lolote bado wanaota kutaka kuendesha nchi. Lazima chadema watambue kwamba wanaweza kushinikiza lakini sio kuamua mambo ya nchi hii kwa sababu wao ni chama chenye uwakilishi hafifu bungeni. Kelele na fujo bungeni hazikipi haki cdm kuongoza kwa hiyo wasiwe wanapiga kelele kusema katiba mpya hakuna wakati katiba ipo inasubiri kupigiwa kura tu.