DAD'S SON
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 392
- 466
Wasalaam,
Tupo katika karne bora sana nadhani ukifuatilia karne tuliopo sasa ndo karne bora kuwai kutokea katika maisha ya mwanadamu. Leo hii upo tandale kwa tumbo unavuta waya unapigia simu mtu yupo Rukwa,nauli yako tu inakufikisha USA ndani ya masaa.
kwa kifupi teknolojia ukuwaji wake umeleta mapinduzi mengi sana katika katika aspects zote za kimaisha.
Yote hayo hapo juu huwezi kuyaweka kwenye kapu bila kuwataja wasomi; watu ambao waliumiza vichwa na mpaka sasa wanaumiza kichwa, wanastahili pongezi sana.
Ukifuatilia kiundani wasomi wa nchi ambazo zimeendelea serikali zao waliona michango ya wasomi nakuamua kuwawezesha ndiyo maana unaona nchi hizo zimefika hapo tunapoziona(zimefanikiwa). Mfano kwa nchi zilizoendelea sector kama ya afya ambayo inasimamiwa na wizara ya afya kuna fungu kubwa wanatoa ili wasomi wao wafanye tafiti mbalimbali kuhusiana na magonjwa na visababishi magonjwa ndo maana mortality rate yao na sisi ni tofauti sana.
Ukija kwa mainjinia wanapewa kipaumbele katika projects zihusuzo nchi husika (huwezi ona injinia wa Kichina anatengeneza gorofa la Muingereza). Kama ulikua hujui basi fahamu kuwa hiyo; ni njia ya kuwawezesha mainjinia wetu(wapewe projects zote za ndani). Kwa ufupi wenzetu wana mazingira rafiki kwa wasomi ndo maana wamefanikiwa.
Kwa hapa kwetu kiukweli nafasi za wasomi ni ndogo mno, maana hata mtu ambaye hana elimu juu ya jambo fulani anaweza aka-draw conclusion na watu wakafuata. Leo hii project hata ya barabara unakutana na Wachina, tumekosa imani na wasomi wetu au kuna kitu behind the scene?
Walimu wapewe kipaumbele, wapewe posho hata 10,000 Tshs kwa siku ili wafundishe kwa moyo wote hii inawezekana kabisa mbunge akikaa kwa kiti chake analipwa sio chini ya 200k, kwanini iwe ngumu kwa walimu?
Wasomi wetu wa mambo ya afya wapewe pesa za utafiti za kutosha hii itasaidia hata ugunduzi wa chanjo mbalimbali,dawa pia hata kupambana na magonjwa kuliko kutegemea ela za wahisani ili nchi yetu inaweza kulisimamia hili, najua unajiuliza inawezekanaje ndio inawezekana serikali inaweza pitia kitabu cha wizara ya afya Inaingiza shilingi ngapi halafu hela inayopatikana kwenye wizara ya afya isiingizwe kwenye matumizi yasio husu wizara ya afya.
Tuna wasomi wa mambo ya kilimo na mifugo tena wengi mno; kwanini tusikae nao meza moja tukajadiliana kuhusu kutengeneza top quality products na kuuza kwa mataifa mengine. Mfano mzuri hakuna asie wajua American Garden jamaa wanauza nyanya, ketchup nk zinakuja mpk Bongo. Hebu wizara ya kilimo na ufugaji tulieni kwenye hili, wezesheni wasomi hawa muone positive impact.
Wizara zinazohusika na Mawasiliano +Teknolojia, hebu kaeni na wasomi wenu wapeni nafasi waulizeni nini kinawafanya msifike mnapotaka kufika. Mfano, hakuna asie fahamu cartoon hizi mambo bila shule huwezi tengeneza but sio kama wasomi wetu hawawezi wanaweza ila wajawezeshwa na mamlaka husikaa, leo kamtafute Elon Musk mzee wa Space X utanielewa nini namanisha, kawatafute wale madogo waliotengeneza Snapchart, kasome historia ya bwana Steve Jobs. Hawa wote waliwezeshwa na nchi zao leo hii wamesaidia kukua kwa uchumi wa nchi zao.
Naomba nikujuze kitu ambacho unakijua lakini sio kwa undani, hizi nchi zinazojinadi kuwa zenyewe ni powerful nations sio kwa kuwa na uchumi mkubwa tu hapana maanake ni kuwa na Teknolojia kubwa na yenye ufanisi wa 100%.
Napenda niseme kuwa hakuna taifa tajiri duniani ambalo halikutambua mchango wa wasomi wa taifa hilo katika ukuaji wa uchumi ni wakati kama nchi kuamua na kuanza kuwapa wasomi wetu njia wezeshi na rafiki ili miaka kadhaa mbele tuwe na Tz ya viwanda na Tanzania ambayo itakuwa ina-export kuliko ku-import bidhaa. Lakini pia wasomi mnaokimbilia kwenye siasa tunajua kwanini mlikimbilia huko tunajua huko kuna mazingira rafiki kwenu ni wakati sasa kuboresha mlipopakimbia ili kupunguza wengine wasije kutukimbia kwa kutokuwa na mazingira rafiki.