Washukiwa watatu wa mauaji Tanga wauawa wakati wa majibizano ya risasi na askari

Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
Haiingii akilini kabisaa....sijajua kua tatizo ni uandishi au ndivyo polisi walivyofanya
 
Sielewei, Kila siku wanauawa tu. Kwa nini hakuna hata mmoja anayenusurika ili akashtakiwe? Kwa nini hatusikii askari kauawa katika mapambano? Tena walijuaje hao majambazi ndo walihusika na katika tukio tajwa? Kwa hiyo siku hizi polisi ndio wakamataji, waendesha mashtaka, mahakimu/majaji, na tena watekeleza hukumu (kunyonga). Hapa utawala wa kisheria uko wapi?
Ungekuwa unajua sheria za askari kujilinda dhidi ya adui usingesema hivo coz umeshaambiwa ni kaktika majibizano ya risas wakt wanataka kutoroka hlfu wewe unataka wawakamte kivip sasa au ukiwa askari ndo uuwawe bila formula?
 
Hapa kuna JAMBO KUBWA halipo sawa.
Watuhumiwa wamekamatwa.
Kisha wakawapeleka askari kwenye msitu kuwaonyesha silaha
Baada ya hapo wakataka kutoroka, huku wakijibizana risasi na polisi..na ndipo wakauawa wote ili kunyang'anywa silaha.

MASWALI MAKUBWA:
1. Huko msituni walipelekwa wakiwa hawajafungwa pingu?
2. Je, walikwenda na silaha zao huko msituni, kwa maana kwamba askari hawakuwapekua ili kuwa-disarm?
3. Kama walikuwa wamefungwa pingu, waliwezaje 'kujaribu kutoroka'?
4. Kama walikuwa wamewanyang'anya silaha wakati wanawakamata (assuming walikuwa na silaha hizo in the first place), walizipata wapi tena huko msituni hadi wakaanza kupambana na askari?

NB: Tunapenda tuishi kwa amani. Ujambazi na mauaji hayakubaliki, na wote wanaosababisha machafuko hayo na wasiwasi kwa wananchi ni vema wakidhibitiwa. Lakini pamoja na hayo tunaelewa askari polisi anatakiwa kuhakikisha anawadhibiti wahalifu kisha kuwapeleka mahakamani. Pale anapokuwa katika hatari anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada ikiwa ni pamoja na kuua anayemshambulia ili kujiokoa.
Lakini kwa stori hii na maswali hapo juu naamini hapa kuna kitu hakiko sawa. Labda kama aliyeleta habari hiyo hapa JF awe ameleta taarifa yenye mapungufu.
Killing the messenger(evidence) a.k.a the Enemy within
 
Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
Nilijua nimegundua hilo peke yangu.
 
Mimi naona sawa kabisa kupokonywa siraha upesi hao majambaz naona wanaowatetea hawawajui vzr majambaz ila kwa mtu anayetambua ubaya wa hao watu katu hawez kuwatetea hata kidogo bora polisi watekeleze kaz yao tumechoshwa na kukaa roho juu juu kwa kuogopa majambaz
 
Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
Kweli kabisa. Hata mimi nimepata ukakasi...ina maana walikwenda kuonesha silaha bila pingu mikononi au??
 
Akili za askari wetu hawa hawashindwi hata kukuwekea bunduki kwenye geto lako halafu kuja kuichukua haraka haraka kwa sababu ya vyeo
issue kama hiyo ilitaka kunikuta ili niwape rushwa lakini mimi nikawa mjanja zaidi yao.......ilikuwa kama movie vile baba 'ake
 
Sielewei, Kila siku wanauawa tu. Kwa nini hakuna hata mmoja anayenusurika ili akashtakiwe? Kwa nini hatusikii askari kauawa katika mapambano? Tena walijuaje hao majambazi ndo walihusika na katika tukio tajwa? Kwa hiyo siku hizi polisi ndio wakamataji, waendesha mashtaka, mahakimu/majaji, na tena watekeleza hukumu (kunyonga). Hapa utawala wa kisheria uko wapi?
hata mimi na mashaka na kutokamatwa wakiwa hai, iliwaeleze waliwachinja kwa sababu zipi,haiwezekani uchinje watu bila sababu lazima kulikuwa na kisa,kisha wapigwe risasi baada ya kutoka mahakamani
 
Back
Top Bottom