Wasanii wa bongo movie msiniharibie mahusiano yangu

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
228
210
Hi everyone in here,

Naandika huu uzi nikiwa nimejawa na huzuni na sononeko moyoni. Tangu jana mpenzi wangu Linda hataki kuja kunitembelea hapa nyumbani, chanzo kikubwa ni hawa wasanii wetu wa michezo ya kuigiza. Issue yenyewe ilikuwa ndogo ila kwa sasa inazidi kuwa too hot. Issue yenyewe ilianza hivi...

Mimi na girlfriend wangu Linda (mtoto wa kiyahudi) tulitoka kama wiki mbili hivi zimeshapita. Tulienda kwenye Wasafi Festival kwa ajili ya kupumuzisha kidogo akili zetu. Nakumbuka tuliingia mida ya saa 1 hivi usiku.

Kwa kuwa Linda hapendi watu wanaopiga kelele hasahasa kelele za kiswahili, tuliamua kukata tiketi za backstage za Tsh. 500,000 kila mmoja. Nakumbuka tulikaribishwa vizuri na Kule tukakutana na watu mbalimbali mashuhuli wa nyumbani Tanzania.

Kumbe bhana tuliepuke kelele za VIP na VVIP tukaangukia kwa manyakunyaku. Sikutegemea kama wasanii ambao ni vioo vya jamii kuanza kujikanyaga kanyaga kwetu kiasi kile. Hii tabia ilinitoa kwenye mood.

Nakumbuka walikuja wadada wawili mastaa wa bongo movie kwenye meza yetu wakaomba watupe company tukawakubalia.Tumekula nao na kucheza nao.Badae katika kuagana waliniomba namba nikawapa. Sasa jana mmoja wao kanitumia sms za ajabu sana zenye maudhui ya kimahaba. Halafu kanitumia mida hiyo simu yangu alikuwa nayo Sweetheart wangu, Linda.

Nikiwa zangu sebuleni nasoma diary yangu kujua Leo nakutana na nani, ntaenda wapi, ntwtumia gari gani, mara Linda anaingia kafula. Hasira zimemjaa mpaka uso wake ukageuka mwekundu.( kwa walioa wayahudi watanielewa zaidi). Akafika akanionesha sms...akaanza kuniuliza ni nani aliyenitext. Mi nikamwambia huyu ni mmoja ya wale wacheza simema tuliokutana nao Wasafi. Kwa hasira alitupa simu yangu chini ikapasuka. Nilikasirika sana.

Sikukasirika kwa sababu kavunja simu ( Kwani milioni 6kitu gani kununua simu nyingine) Nilikasirika kwa sababu huwa sipendi kulaumiwa kwa kosa ambalo sijafanya. Kwa sababu ya hasira nilimsukuma Linda kwenye Sofa za pale seating room na kuanza mrushia maneno makali ya kingereza. Nitatafasiri kwa faida ya waliokomea la saba( maana napokea ushauri kutoka kwa wote)

" Iweje unilaumu mimi na wakati kosa sio langu! Huyu dada sio mtu wangu. Aliwahi kuwa mpenzi wa rafiki yangu. ( msanii mkubwa) iweje leo awe mpenzi wangu" (Mwisho wa kunukuu)

Linda alitoka pale sebuleni akachukua gari yake akaenda kwa ndugu zake ubalozi wa Marekani. Ilibidi kitu cha kwanza nimtumie email shangazi yake ili amtulize asije akajizulu. Watoto hawa wakizungu wanapenda sana. Mpaka mida huu namalizia uzi huu Linda hapokei simu yangu.

Ushauri wangu:

Enyi wanawake wa kitanzania. Ukiona mwanaume yupo kwenye mahusiano, usimuzoe ovyo ovyo. Sasa unapojipendekeza kwake unataka amuache ampendaye akupende wewe?

Kabla ya kuingilia katikati ya wapendanao jiulize gharama za kurudisha mahusiano ya hao waliopendana siku nyingi. Usidhani unapoharibu mahusiano ya wawili walioshibana unawaaribia wao tu. Unaweza sababisha mataifa mawili yakachukiana bure kisa ujinga wako.

Ni bora uingilie mahusiano ya wabongo ila sio ya wale tunao-date mabinti wanaotoka nchi za wadau na wahisani wa maendeleo. Kaeni mkijua kuniharibia mimi ni kutenganisha uhusiano baina ya nchi yetu na taifa la wayahudi. Kurudisha itawagharimu.

Jambo Tanzania.
 
Samahani ningetuma hiyo sms ya mcheza sinema ila kwa hii simu mpya nilionunua ina sense threats za mitandaoni. Ngoja nijaribu ikiwezekana nitawawakea.
Asanteni.
 
Jamaa moja aliota a.eomota mfuko wa hela , mara zikawa zinadondoka kwenye tundu akaziba tundu na mkono wa kushoto, alupoziba zikaanza kutokea kwa juu akafunika na mkono wa kulia .

Alishtuka akiwa ameunyea mkono na kutapikia ule mwingine pia.

Ndoto bhana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom