Rais wangu Daktari John Pombe Magufuli, ninakuandikia maneno haya machache kama furaha yangu kuwa na rais kama wewe ambaye taifa lilimsubiri kwa miongo kadhaa, Wakati nikikupongeza kwa ustahimilivu na uchapakazi wako hasa kwakutowasikiliza wapiga kelele dhidi ya msaidizi wako mpendwa mkuu wa mkoa wa Dar, nashawishika kukwambia kwamba video hii hapa chini ni ya mkuu wa mkoa wa Dar iliyorekodiwa kwa kutumia kamera za kiusalama (cctv).
Video inaelezwa hapo ni kituo cha tv cha Clouds na kwamba mkuu wako wa Mkoa alivamia kituo hicho kwalengo alijualo yeye, yaani amevamia kwatumia jeshi letu linalotumia kodi za wananchi kwa mambo yanayodhaniwa ni binafsi. Kibaya zaidi amevamia kituo chako pendwa kabisa cha tv hasa kile kipindi cha Shilawadu.
Mimi nakutazama lakini nina akili timamu nafahamu kwamba vyeti feki vya Daudi Bashite anayejiita Paul C. Makonda KAMWE havitamtumbua, na njia sahihi ni hii ya "kuleta vurugu uraiani", naitafakari simu yako kwa Shilawadu, yule anakutamaza, wale wanakutazama na Dunia inakutazama mh rais, watanzania wanakutamaza mh rais, Katiba imekupa mamlaka ya nusu uungu rais wangu, fanya jambo watu wa tanzania na dunia wajue wewe ni nani. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mpo wapi? Ninani katika ardhi ya jamhuri hii ambaye yupo juu ya sheria na katiba za nchi yetu?
Kama tukio hili ni uvamizi bila shaka runinga ya clouds itafungua kesi dhidi ya wavamizi, na hilo tunalisubiri...Lakini kwa mamlaka ya kirais, Mh Makonda amepoteza sifa za kuwa msaidizi wa Rais kwa nafasi yoyote ile....
Ikupendezavyo mheshimiwa rais, katiba inakupa nguvu kwamba hutatenda kazi yako ya urais kwakulazimishwa kushauriwa na mtu yeyote au kikundi chochote.
Wewe ndiye rais wetu, uliwazalo na ulitendalo lidumu daima mheshimiwa rais.
Nikutakie jumapili njema!
Na Yericko Nyerere