Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,912
Zitto ni mpinzani, mpambanaji au msaliti?Wapinzani nchi hii ni wengi lakini wapambanaji miongoni mwao ni wache kitu ambacho ni hatari kwa upinzani unaokusudia kushika dola.
Kwa mfano,kuna wabunge wa upinzani tangu Bunge la November liishe hawajasikika popote wakati kuna mengi tu ya kuyasemea,kuhoji na kukosoa.Hili hali haipaswi kuendelea.
Baadhi tutawasikia katika Bunge linaloanza mwezi huu mwishoni na likiisha hutawasikia tena mpaka Bunge la April!
Miongoni mwa mambo yaliyopaswa kuhojiwa na wapinzani ni pamoja na haya
1.Wanafunzi kukosa mikopo
2.Wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kusitishwa ufadhili wa masomo na serikali
3.Hatima ya zoezi la uhakiki wa watumishi(litaishi lini)
4.Swala la kulipa stahiki/madai ya watumishi
5.Uwepo wa taarifa kuwa waliositishiwa ajira miezi 6 iliyopita kupisha uhakiki ajira zao zimefutwa na watatakiwa kuomba upya
6.Sababu za TRA kutotangaza mapato ya Novembe na December kama walivyokuwa wakifanya kwa miezi ya nyuma(hii taarifa ya makusanyo ya miezi 6 waliyotoa leo hata wasingetoa kulikuwa hakuna wa kuhoji zaidi ya sisi huku mitandaoni)
7.Ni lini serikali itaanza kutoa ajira na sio tu kutoa matamko ya kuajiri bila kutoa timeframe ya utekelezaji.
Hayo ni baadhi ya mambo miongoni mwa mengine mengi ambayo wapinzani walipaswa kuyahoji kama alivyofanya waziri Kivuli wa Afya pale alipotoa tamko kuhoji/kuongelea swala la upungufu wa madawa mwaka jani mwezi wa 9 au wa 10 kama sikosei.
Wapinzani ambao wamekuwa active/ wapambanaji kwa sasa na wanasaidi serikali kujirekebisha/kujitafakari ni Lema,Lissu,Zitto na Kafulila lakini wengine wanaendesha soft politics tu na wengine ni kama wako likizo!
Niwambie tu hata hili swala la chakula mngekaa kimya kama mlivyokaa kimya kuhusu haya mambo mengine,leo sidhani kama mngesikia serikali inajipanga kuanza kusambaza chakula maana walishaonyesha nia ya kutofanya hivyo lakini kelele za Zitto na uamuzi wa CHADEMA kutaka kugawa chakula ndio bila shaka utakuwa umeishitua serikali.
Nina haikia hata haya matatizo mengine hayashuhulikiwa kwasababu yamekosa msukumo kutoka kwa wanasiasa na watu wengine wenye kuheshimika katika jamii.
Kumbukeni hata baada ya Lissu kukomaa kuhusu hoja ya kusitisha mikutano ya kisiasa mpaka 2020,ndio angalau likaja tamko tata kuwa mtaruhusiwa kufanya mikutano kwenye maeneo miochaguliwa tu na si vinginevyo.
Hivi sasa kampeni za udiwani zinaendelea lakini anaetumia mikutano hiyo kuongelea maswala mazito ya kitaifa amekuwa ni Zitto tu wengine hata hamsikiki.
Endeleeni hivyo hivyo mtaona matokeo yake japo jamaa kila siku anaharibu.
Pamoja na yote haya ila kwa sasa amesaidia na anastahili pongezi.Zitto ni mpinzani, mpambanaji au msaliti?
Nyumbu ni nyinyi msioweza kukosoa yanayofanwa na chama chenu na badala yake kutetea na kuunga mkono kila jambo hata kama kuna mengine ya kipuuzi.Salary slip ameanza kupona unyumbu
Wanasubiri bunge liveWapinzani nchi hii ni wengi lakini wapambanaji miongoni mwao ni wache kitu ambacho ni hatari kwa upinzani unaokusudia kushika dola.
Kwa mfano,kuna wabunge wa upinzani tangu Bunge la November liishe hawajasikika popote wakati kuna mengi tu ya kuyasemea,kuhoji na kukosoa.Hali hii haipaswi kuendelea kama kwelo tunataka kushika dola na zaidi kama tunaka wananchi waelewe madhaifu ya hii serikali.
Baadhi tutawasikia katika Bunge linaloanza mwezi huu mwishoni na likiisha hutawasikia tena mpaka Bunge la April!
Miongoni mwa mambo yaliyopaswa kuhojiwa na wapinzani ni pamoja na haya
1.Wanafunzi kukosa mikopo
2.Wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kusitishwa ufadhili wa masomo na serikali
3.Hatima ya zoezi la uhakiki wa watumishi(litaishi lini)
4.Swala la kulipa stahiki/madai ya watumishi
5.Uwepo wa taarifa kuwa waliositishiwa ajira miezi 6 iliyopita kupisha uhakiki ajira zao zimefutwa na watatakiwa kuomba upya
6.Sababu za TRA kutotangaza mapato ya Novembe na December kama walivyokuwa wakifanya kwa miezi ya nyuma(hii taarifa ya makusanyo ya miezi 6 waliyotoa leo hata wasingetoa kulikuwa hakuna wa kuhoji zaidi ya sisi huku mitandaoni)
7.Ni lini serikali itaanza kutoa ajira na sio tu kutoa matamko ya kuajiri bila kutoa timeframe ya utekelezaji.
Hayo ni baadhi ya mambo miongoni mwa mengine mengi ambayo wapinzani walipaswa kuyahoji kama alivyofanya Waziri Kivuli wa Afya pale alipotoa tamko kuhoji/kuongelea swala la upungufu wa madawa mwaka jani mwezi wa 9 au wa 10 kama sikosei.
Wapinzani ambao wamekuwa active/ wapambanaji kwa sasa na wanasaidi serikali kujirekebisha/kujitafakari ni Lema,Lissu,Zitto na Kafulila lakini wengine wanaendesha soft politics tu na wengine ni kama wako likizo!
Niwambie tu hata hili swala la chakula mngekaa kimya kama mlivyokaa kimya kuhusu haya mambo mengine,leo sidhani kama mngesikia serikali inajipanga kuanza kusambaza chakula maana walishaonyesha nia ya kutofanya hivyo lakini kelele za Zitto na uamuzi wa CHADEMA kutaka kugawa chakula ndio bila shaka utakuwa umeishitua serikali.
Nina haikia hata haya matatizo mengine hayashuhulikiwa kwasababu yamekosa msukumo kutoka kwa wanasiasa na watu wengine wenye kuheshimika katika jamii.
Kumbukeni hata baada ya Lissu kukomaa kuhusu hoja ya kusitisha mikutano ya kisiasa mpaka 2020,ndio angalau likaja tamko tata kuwa mtaruhusiwa kufanya mikutano kwenye maeneo miochaguliwa tu na si vinginevyo.
Hivi sasa kampeni za udiwani zinaendelea lakini anaetumia mikutano hiyo kuongelea maswala mazito ya kitaifa amekuwa ni Zitto tu wengine hata hamsikiki.
Endeleeni hivyo hivyo mtaona matokeo yake japo jamaa kila siku anaharibu.
Hivi ukiitisha press conference au ukitoa press release kuhoji ni kwanini serikali imesitisha ufadhili wa serikali kwa watanzania wanaosoma nje ya nchi utakamtwa?Hata ndani ya upinzani kuna wachumia tumbo. ukiona mpinzani kakaa kimya ni mchumia tumbo tu. anaogopa nini? mpinzani wa kweli haogopi mahabusu, haogopi polisi wala virungu vyao. hawamuoni Kiza Besigye na Godbless Lema?
Awamu hii bila umoja na mshikamano ni shiida.Wanapima upepo mkinyweya wanawaburuza.Yaani wabunge wa upinzani wamezidiwa ujasiri hata na wenyeviti wa serikali za mitaa!!?
maana wametia presha serikali mpk imekubali yaishe.
umoja ni nguvu, wanapogawanyika na kubaki wachache tu ndiyo wanazungumza, hao wachache wanaonekana wachochezi.
Hivi ukiitisha press conference au ukitoa press release kuhoji ni kwanini serikali imesitisha ufadhili wa serikali kwa watanzania wanaosoma nje ya nchi utakamtwa?
Leo hii serikali ikitangaza kusitisha posho za wabunge watakaa kimya?
Hawa kina Lissu inawezekana hata wao hali hii ya wenzao kukaa kimya inawakatisha tamaa na pengine inawaumiza ila wanakaa kimya tu ili kutoleta mvuvurugano kwenye vyama vyao.
Chadema tokea wamsafishe fisadi Lowasa hawatakuja kuaminika tena mbele ya macho ya watanzania.
Watabaki kushabikiwa na malofa tu.
Hebu mkosoe mfalme Mbowe ukione cha motoNyumbu ni nyinyi msioweza kukosoa yanayofanwa na chama chenu na badala yake kutetea na kuunga mkono kila jambo hata kama kuna mengine ya kipuuzi.