Wapakistan 12 Wanaokabiliwa na Kesi ya Kusafirisha Dawa za Kulevya Wameomba Wapigwe Risasi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,860
5,801
[h=2]Friday, April 24, 2015[/h][h=3]Wapakistan 12 Wanaokabiliwa na Kesi ya Kusafirisha Dawa za Kulevya Wameomba Wapigwe Risasi Baada ya Kesi yao Kuzungushwa Kisutu ‪[/h]

1.jpg


Raia 12 wa Iran na Pakistan wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin kilo 200.5, zenye thamani ya sh. bilioni 9.02, wamelalamikia kucheleweshwa kwa kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Washtakiwa hao ni Kapteni Ayoub Mohamed, Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Khalid Ally, Abdul Somad, Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad, wote raia wa Iran ambao walikamatwa kwenye Bahari ya Tanzania.


Wengine ni Buksh Mohamed, Rahim Baksh na Abdul Bakashi kutoka Pakistan ambao wote ni wavuvi.


Mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda, Wakili wa Serikali Janeth Kitali, alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa.


Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa wa kwanza Ayoub ambaye alikuwa nahodha wa meli iliyokutwa na shehena ya dawa hizo, alidai bora wapigwe risasi wafe kuliko kucheleweshewa hukumu yao.


Alisema kila wanapofikishwa mahakamani hapo, wanaambiwa upelelezi haujakamilika na muda unakwenda wakizidi kuteseka gerezani ambako mazingira yake si mazuri.


Hata hivyo, Hakimu Kaluyenda aliahirisha shauri hilo hadi Mei 5, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao walirudishwa rumande.


Inadaiwa Februari 4, 2014, washtakiwa hao walikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin kilo 200.5, zikiwa na thamani ya sh. bilioni 9.2, wakizisafirisha kwa njia ya bahari.


at 3:20 PM - Vijimambo



 
Watu wamekutwa na madawa ya kulevya, halafu waendesha mashtaka wanadai uchunguzi haujakamilika, wanataka ushahidi gani tena? Kesi tangu mwaka jana kama wanawaonea aibu kuwapa hukumu wanayostahili wawaachie huru.
 
Hii ni tz tu,
Mtu anashikwa na vithibiti(ushahidi) kesi inazungushwa.

Mbn kule china watz wanaodakwa huwa wanasekwa selo mvua za kutosha tu.

Mie nafikiri ucheleweshwaji huu unajenga mazingira ya kupokea rushwa.
Hii sheria mpya inaanza lini kutumika??
 
Nakumbuka pia hadi yulek kijana walilyemuua kwenye fence kisutu akijaribu kutoroka mwaka jana naye ilikuwa ni ucheleweshaji wa kesi hivi hivi. Wanaushahdi mikononi, halafu wanasema upelelezi haujakamililka. Mkuu wanchi ana majina ya vigogo wa madawa ya kulevya, mahakuma siku wamechukuliwa hatua richa ya kutangazwa tu. Kuna uhusiano gani kati ya madawa ya kulevya na serikali ya Tanzania kiasi kwamba, serikalil na mahakama zinapata kigugugmizi kuchukua hatua kwa wahusika wakuu wa madawa ya kulevya?

Kwa ni ni tusiamini kwamba watuhumiwa wanaokamatwa na madawa ya kulevya na mahakama kushindwa kutoa hukumu zao kuna mkono wa vigogo ambao wanalindwa na serikali?
 
Back
Top Bottom