Waooo! 'Instruction' imeshatoka na bilioni 10 imeshatua TBA. What a life style!

Nyie kandarasi mlitutesa sana...mmepandisha bei za nyumba mkatengeneza faida kubwa imagine nyumba dar zinauzwa hadi dolla 400,000 wakati SA au Dubai unapata nyumba kali kwa chini ya dolla 150,000...wezi sana nyie jirekebisheni
 
Hivi, ni maaskari tu ndio wenye shida za makazi? Waalimu hawhitaji huduma za makazi bora na yaliyo jirani na shule? Au wao huduma zao sio muhimu kama za maaskari? Nauliza tu ndugu mtoa maelekezo.
Ingelikuwa vyema kama nyumba za nhc kipaumbele cha kwanza kiwe walimu na wapangiwe kodi elekezi badala ya nyumba hizo kuwaweka wafanyabiashara wenye uwezo wa kujenga zao. Hebu anza na DAR kwa hili kama litakupendeza.
Enzi za mwalimu wafanyakazi wa umma walipangishwa nyumba hizi na kodi kukatwa kutoka kwenye mishahara yao. Hili linakushindeni nini sasa?
 
unaongea kwa ujasiri sana

jengo la ewura washindani walisema watajenga kati ya bilioni 25 mpaka 34 tu

TBA alisema atajenga kwa bilioni 45

acha kuishi kwa hisia

utajikuta unaingia period
Lengo ni kupata value for money, kama TBA wakija na bidding kubwa acha kampuni nyingine zichukue tenda ila hii lia lia eti TBA wasipewe tenda wapewe kampuni binafsi tu ndio propaganda tunazozipinga.
 
CRB (Bodi ya usajili wa makandarasi ) ifutwe kwa sababu hakuna haja ya kusajili makandarasi kama kila kazi itafanywa na TBA.

Wananchi wanatakazunguko wa pesa na ajira kukua ,vyote hivyo vitatoka wapi kama serikali haiingizi pesa kwa watu wake?

Wanasema wanaolia pesa hakuna ni "wapiga deal" leo makampuni binafsi hauapewi zabuni pesa zitasambaaje mtaani ?
 
Wala usiumie. Lengo ni kujenga na kuiendeleza nchi. Kupitia procurement wizi a.k.a dili ndio huwa zinachezwa. Kama huna rafiki ambaye anafanya kazi hizo basi mtafute atakujuza namna walivyokuwa wanalitia hasara taifa kwa kigezo cha hiyo sheria ya manunuzi. JPM yupo serikalini long time anajua michezo yote iliyokuwa inachezwa.

Nitakupa mfano mmoja mwepesi kuelewa.

Mfano mie ni mtu wa procurement nipo kwenye G SAM Inv Co Ltd, Boss unanijuza kuwa tununue Laptop mpya za wafanyakazi. Then mie na kitengo changu tunatangaza tenda kufuata hako kasheria, watu/kampuni zina bid mie na timu yangu tunakaa kuzichambua na tunawachagua watatu waliobid kwa pesa ndogo, tunawaita kuwasikiliza kupata uhakika wa service tunayotaka, kisha mie na wenzangu tunaanza kujadiriana na kila kampuni kivyake vyake kutaka kamisheni ili tuwape tenda, kwahiyo kwa pamoja kama A ilikuwa imekubali kutuletea kila laptop kwa laki 8 tunaiambia ibadiri invoice iweke 1M, kampuni B nayo kama ilitaja laki 8 na nusu tunaiambia ibadiri invoice na iweke labda 1M tena na kampuni C nayo kama ilitaja laki9 nayo tunaipeleka kwenye 1.1M. Wanabadirisha then wanatukabidhi wao kazi yao inabaki kusubiri majibu ya nani kapitishwa. Mie na timu yangu ambao tuko na mamlaka hayo tunazipele kwa Mkurugenzi au kitengo husika kuwa hawa watatu ndio wenye sifa. Boss GSAM na kabineti yako mnakaa kuchagua mmoja. Sie yetu macho kwani yeyote mtakaye mchagua sie tumeshaongeza cha juu tayari.

Then Boss GSAM anarejesha jina la kampuni waliyoipitisha yeye na bodi yake. Sie huku tunachekelea, tayari tumesha iumiza GSAM Inv Co Ltd kupitia hiyo sheria unayoipigia chapuo.

Na the same laptop tunayokuletea kupitia hao waliochaguliwa ukienda posta unakuta inauzwa laki 8, GSAM anajikuta anailipia pesa nyingi sana.

So the same example and more ujanja ujanja maprocurer hutumia kuliibia Taifa. Lakini kwa style hii kitu unakipata kwa thamani halisi ndio maana TBA pale UDSM wametoa flat nyingi na bora kwa pesa hiyo hiyo. Ile ngoma ungewapa procurer isingekuwa 10B ungeambiwa 500B

nakumbuka na ile ya upanuzi wa bandari ya dar. get ... no sijui ngapi jamaa waliweka 600b , mwakembe akashtukia hilo dili la kampuni ya china construction machant,ndio ilishinda hilo dili la 600b na yule mwanasheria mbumbu mbuu wa serika warema akaingilia kati kuwa , mkataba umeshaasaniwa na kuuvunja ni hasara mwakembe akasema hakuna hata yeye ni mwanasheria jamaa akawatosa wakakumbia , kampuni nyingine ikasema itafanya hiyo kazi kwa 250b tu .
 
CRB (Bodi ya usajili wa makandarasi ) ifutwe kwa sababu hakuna haja ya kusajili makandarasi kama kila kazi itafanywa na TBA.

Wananchi wanatakazunguko wa pesa na ajira kukua ,vyote hivyo vitatoka wapi kama serikali haiingizi pesa kwa watu wake?

Wanasema wanaolia pesa hakuna ni "wapiga deal" leo makampuni binafsi hauapewi zabuni pesa zitasambaaje mtaani ?

TBA nao wanahitaji wakandarasi kwani shida nin hapo
 
tapatalk_1512336483301.jpeg

tapatalk_1512319565619.jpeg
tapatalk_1512319561468.jpeg

tapatalk_1512319557831.jpeg

tapatalk_1512319425915.jpeg


Mengine huwa nafanya kwa frustration zangu tu
 
Watetezi wa TBA, endeleeni kushangilia utendaji mzuri.
Wakati hauongopi ,utakuja kutuumbua muda si mrefu.
 
Huyu Mzee leo mtamuua kwa shinikizo la damu....
Naomba nikupongeze sana ewe mkuu sana na kiongozi wetu rais John Pombe Magufuli. Naona sasa tender zote za ujenzi ni TBA. Ushauri na uchoraji ni BICO. Umeme na ufundi ni TEMESA! Hivyo vikampuni vingine vya ukandarasi na ushauri elekezi tupa kule kwanza vinatozatoza tu wakati hela yako haiendi bure bure!!

Naona tayari kule Ukonga mambo bwerere na fedha zote zipo TBA tayari kwa kujenga maflat ya askari kama ulivyosema utatoa "instruction" kwa chief secretary! Hakuna cha bajeti, kutangaza tenda wala nini!

Hapa kazi tu!

Hili ni swali gumu wenyewe wana majibu.
Zitakufaje kwani zilianzishwa kwa ajili ya kujenga majengo ya serikali tu? Na wakati zinaanzishwa makampuni ya serikali hayakuwepo? Ile interchange ya mbagala inajengwa na serikali? Uwanja wa ndege wa chato unajengwa na serikali?

Hii ni shughuli pevu....
Hujaenda tenda ya uwanja wa ndege? Ungependa makampuni ya serikali yasipate kazi? Kumbuka toka enzi za nyerere makampuni ya serikali yalipewa kandarasi kubwa kubwa kwa mfano mecco imejenga barabara nyingi nchini imejenga ghorofa la kitega uchumi dar imejenga soko la kariakoo nk kumbuka kwamba sio rahisi kampuni ya serikali kupata tender ya kujenga mradi wa mtu binafsi lkn ni rais kampuni bunafsi kupata tender serikalini na sekta binafsi hivyo aliyekuwa anachezewa rafu kwa muda mrefu ni makampuni ya ujenzi ya serikali kwa sasa anayayewezesha lkn na watu binafsi nao wana nafasi yao kwa sab serikali haina makampuni ya kutosha na kila eneo la uhandisi lazima sekta binafsi itahusishwa tu.

Hapa sina cha kuchangia....sijakuelewa mkuu Chibolo..

PPRA na visheria vyao vya manunuzi tupa kule mara oooh tenda itangazwe miezi mitatu...mara mikataba ipitiwe na mwanasheria wa silikareee.....mara sjui vikao vipitie hakuna....nasema hakuna hapa mi ndio nampendea mzee wa kazi tu....

"Nikapiga simu TBA nikawauliza, kwani nyie mtatoza shiringi ngapi? Wakajibu birioni 13 nikawaambia washushe mpaka birioni 10 wakakubari nikawapa mradi wa mafrat ya UDSM"

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

L. P. 3021,
11410 – DAR ES SALAAM

JUMAMOSI, DESEMBA 24, 2016
 
Back
Top Bottom