Wanyonge wasikilizwe

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Nimesikia redioni leo wakazi wa baadhi za wilaya mkoani Dodoma wanalalamika hawana sukari, mwezi mzima. Wanasema ikipatikana wanauziwa kwa tzs 2,600 kwa kilo!

Nani atawasikiliza hawa? Maana nchi nzima tumetekwa na nani anatumbuliwa leo jioni, nani atatumbuliwa kesho, nani yuko kwenye benchi la ufundi anasubiri kutumbuliwa! Tukitoka usingizini tutakuta kilo ya sukari ni tzs 3,000 na muda huo chai ni anasa!

Tumbua baba, tumbua tu! Lakini bei elekezi ya kilo ya sukari mlisema ni tzs 1,800!Tuendelee na utumbuzi, utumbuaji na unyumbulishaji mwingine wa neno hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…