Wanawake wanajua kupiga shangwe, Bahati Keneth Ndingo aapa kiapo cha uaminifu jimbo la Mbarali

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,662
8,787

Leo bungeni, mbunge wa Mbarali ameapa kiapo cha uaminifu baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mbarali. Jimbo hilo liliingia kwenye uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mbunge wake, Francis Leonard kufariki dunia Julai Mosi, 2023.

Wabunge wanawake wa chama cha mapinduzi walijifunga kibwebwe na kumfikisha Ndingo pale inapokaa siha ya Bunge na kula kiapo hicho.
 
Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Bahati Ndingo amekula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson wakati wa kikao cha Bunge leo October 31 Jijini Dodoma.

Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge umeanza ambapo shughuli ya kwanza katika Kikao cha Kwanza cilikuwa ni Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kumuapisha Mhe. Bahati Ndigo ambaye alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo

Bahati alitangazwa Mshindi wa nafasi hiyo September 20 mwaka huu mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Francis Mtega.

F9wZvdea8AA_Xy-.jpg
F9wZzBbawAATGNQ.jpg
F9wZwjAbMAAvLJ6.jpg
F9wZxxwawAAsZnH.jpg
 
Na nani amekula kiapo juu ya Ripoti ya Wizi wa kutisha ya CAG?
 
Back
Top Bottom