Ukweli ni kwamba wanaume tumekuwa wahanga wa kusingiziwa na wanawake na jamii ikaamini ni kweli, inapotokea mwanaume ukasingiziwa na mwanamke kuhusu jambo lolote lile jamii huwa inamwaamini mwanamke kwa haraka sana.
Binafsi toka utotoni nimewahi kusingiziwa na wanawake mara nyingi sana na jamii ikaamini ni kweli nimefanya na wanawake kwa kujua udhaifu huu wamekuwa wakiutumia kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wanaume.
Nakumbuka kipindi nipo sekondari niliimpiga binti tuliyekuwa tunasoma nae kwa kauli yake chafu lakini alipoenda kwa walimu aliwaambia nimemtongoza amekataa ndio maana nimempiga staff walinigawana na shule nzima ikaamini uongo wa yule binti.
Nilipokuwa nimehitimu kidato cha sita kuna shule niliyeenda kujitolea, kuna binti alikuwa mkorofi sana nilimshuhudia akimpiga mwenzake, nikamuita nikamuonya lakini alipotoka ofsini alimpiga tena yule binti nikamuita nikamchapa fimbo tatu, yule binti alikimbia mpaka kwao akamwambia mzazi wake nimemtongoza amekataa ndio maana namnyanyasa shuleni, wakati hata nilikuwa sijawahi kuwaza kutongoza mwanafunzi pale shuleni.
Tukio lingine lilitokea nikiwa chuo mwaka wa pili, nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi la majadiliano, kuna binti alikuwa hahudhurii kwenye mijadala yeye anasubiri mmalize asaini, siku moja tukaamua kama kundi asiandikwe kwenye kazi, yule binti alivyojua hakuandikwa akakimbilia kwa mwadili wa chuo na kumwambia nimemtongoza amekataa namnyanyasa kwenye kundi, mwadili akamwaamini na hata wale wanakundi baadhi waliamini uongo wa yule binti.
Kipo kisa kingine kinamhusu rafiki yangu ambae ni mkuu wa shule kuna binti alikuwa ni mwalimu shuleni pale alikuwa mvivu, mkorofi, alikuwa anachelewa, utoro wa mara kwa mara na hatimizi majukumu yake ipasavyo mkuu wa shule akamkanya sana lakini hakusikia akaamua kulisogeza ngazi juu, cha ajabu yule binti mbele ya kikao cha walimu na maafsa toka wilaya alisimama akasema mkuu anamfuata fuata kwa sababu alimtongoza akakataa, yule mkuu siku ile aliaibishwa sana wale maafsa walimgeuka na kumsema yeye.
Ifike mahali jamii isiwaamini wanawake, wanatumia jinsi yao kuwanyanyasa wanaume sana na mara nyingi wanaume wakisingiziwa huwa hawana mtetezi na hata ukijitetea hakuna wa kukuamini.