Wanasaikolojia nisaidieni: Nimeota nimeua kwa bahati mbaya, maana yake nini?

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,136
3,924
Nimeota Jana nimeua bahati mbaya. Niliota tukiwa sokoni ghafla mwizi kwenye asili ya kiarabu akichomoa simu nikamuona na kuanza kumpiga akaanguka chini kujigonga kwenye ngazi na kufa. Nikakimbia watu wakanifukuza ila mmoja alinikamata na kuniambia potea. Ghafla nkaamka.

Hii ina maana gani Leo kutwa nzima sina raha.
 
Labda ulivimbiwa mkuu, jitahidi kula chakula kiasi kidogo usiku, pia epuka kufikiria sana muda mfupi kabla ya kuingia kulala. Ndoto nyingi ni matokeo ya uchovu na marudio ya yale unayozungumza, kusikia na kuona kwenye mazingira yanayokuzunguka.
 
puuzia itapita hiyo, nishaotaga ndoto nyingi za kutisha ila hadi leo hamna hata chochote,
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…