Wanaoomba michango ya harusi majasiri sana

Unakuta mtu hamjawasiliana hata miaka mitano lakini ikikaribia harusi yake unashangaa kuona simu zake akiomba mchango. mambo kama hayo yanahitaji ujasiri. Ni vyema kujitahidi kukumbuka watu nyakati zote. Mwingine tuliachana form VI, baada ya miaka mitano ananitafuta anataka mchango.

mtu unafurahi kwamba jamaa kakukumbuka halafu unashangaa anaingizia mchango, inakata sana stimu.
Sababu kuu ni ubinafsi,iweje hata kutafutana kuje wakati wa kutaka michango.....?
 
Mara ya mwisho kuchangia ilikuwa July 2016. nitawachangia wadogo zangu siku wakioa au kuolewa.

wengine tumeni tu kadi lkn sitatoa. ova
 
Back
Top Bottom