Wanaonishi Dar vijijini hawa hapa

Mleta Uzi bila shaka wewe dar umekuja majuzi, huenda upo chuo first year NA dar huijui. Lakini pia kama umekaa mda mrefu dar na unayaandika haya basi utakua hata darasa la 7 hukufika, hapa namanisha umefanya research ya kitoto NA ume conclude uongo. Ni sehemu gan dar wanawake hawabandiki nywele bandia?
Ni eneo lipi dar mvua ikinyesha panapitika kirahisi japo si mafuriko kote ila Maji hujaa barabarani NA hata kuzamisha magari?
Ni eneo gan dar lisilotumia boda boda au bajaji?

Fine, kwa point yako wewe naeza kukubali kua wote tunaoishi hapa twaish vijijin.

Lakini pia, nani alikuambia kua vijijini kuna mafuriko?
Hv kati ya mjin NA kijijin wap wanatumia zaid nywele bandia?
Hope ulikurupuka, next tym ulete Uzi unaoendana NA jukwaa hili , hapa siyo FB!!
Halafu pia kwenye somo la Uraia majiji na sehemu za mijini hakuna vijiji Kuna Mitaa
 
Anae taka kuishi mjin kama o,bay,masak,posta,k/koo,mbezi beach n.k ataishi kwa kupanga sawa ueanda ukawa na harufu ya kuishi mjini,

Na nawapa big up woote waishio kwenye mijengo yao hata kama ni kijijini.
 
Kama eneo unalo ishi lipo hapa basi unaishi Dar vijijini

1. Mtaani kwako usiku wanacheza ngoma za kizaramo.

2. Hakuna plan ya kufikiwa na mradi wa BRT.

3. Mnapopanda daladala mnaingilia dirishani.

4. Ukitaka kwenda kwenu toka mjini unavizia daladala la mjini kisha unageuza nalo.

5. Eneo unalo ishi kuna bar nyingi kuliko supermarket.

6. Unatumia zaidi ya saa 1 barabarani kufika unakoishi toka mjini.

7. Eneo unalo ishi bajaji na bodaboda ni nyingi kuliko magari.

8. Kondakta wa daladala la eneo lako anatembea na kidumu cha maji ya kuoshea uso kuondoa vumbi.

9. Wanawake wanaovaa nywele bandia na kucha bandia ni wengi kuliko wanawake wasio jipamba wa vitu bandia.

10. 10 % au zaidi ya wanaoishi eneo lako hawana sehemu ya kupark magari yao wanapark kwa majirani.

11. Mvua zikinyesha basi mafuriko hayakosi.
I'm very proud kuishi USWAHILINI...Ww kakae tu Masaki kwenu kwenye ukuta na geti km Segerea
 
Huyu mleta mada anaishi maeneo hayo anayoyaita dar vijijini maana ana uuelewa mkubwa sana na mambo ya uswazi kuliko waswaz wenyewe.
Tunaishi nae jirani hapa Tandale sema tu anazuga.......
 
Sinza kuna bar nyingi kuliko sehemu yoyote hapa dar/ sinza brt haijafika! Kwa akili yako ndogo unataka kutuaminisha kuwa nako ni kijijini?
 
Kama eneo unalo ishi lipo hapa basi unaishi Dar vijijini

1. Mtaani kwako usiku wanacheza ngoma za kizaramo.

2. Hakuna plan ya kufikiwa na mradi wa BRT.

3. Mnapopanda daladala mnaingilia dirishani.

4. Ukitaka kwenda kwenu toka mjini unavizia daladala la mjini kisha unageuza nalo.

5. Eneo unalo ishi kuna bar nyingi kuliko supermarket.

6. Unatumia zaidi ya saa 1 barabarani kufika unakoishi toka mjini.

7. Eneo unalo ishi bajaji na bodaboda ni nyingi kuliko magari.

8. Kondakta wa daladala la eneo lako anatembea na kidumu cha maji ya kuoshea uso kuondoa vumbi.

9. Wanawake wanaovaa nywele bandia na kucha bandia ni wengi kuliko wanawake wasio jipamba wa vitu bandia.

10. 10 % au zaidi ya wanaoishi eneo lako hawana sehemu ya kupark magari yao wanapark kwa majirani.

11. Mvua zikinyesha basi mafuriko hayakosi.
Uwo no mtazamo wako tu,et sehemu ikipigwa ngoma ya kizaramo uswahilini,km aujui hili jiji la Dar wenyewe wazaramo sasa unataka waende wakacheze ngoma yao mbeya au Kilimanjaro??
 
mliochangia wote mmefeli..........tizameni namba 6, anasema unatumia saa moja na zaidi toka mjini

muulizeni kuanzia hapo sasa
 
Anae taka kuishi mjin kama o,bay,masak,posta,k/koo,mbezi beach n.k ataishi kwa kupanga sawa ueanda ukawa na harufu ya kuishi mjini,

Na nawapa big up woote waishio kwenye mijengo yao hata kama ni kijijini.

Na huko pembeni ndo watu wanaishi kwenye makazi yaliyojengwa kiuhakika, siyo mtu uko Tandale unasema uko mjini. Utaishije mjini kwenye kelele nyingi mtu unayejitambua, mjini watu wanakwenda kwa mahitaji tu. Ujanja ni kujenga nje ya miji huko unapata hewa safi na utulivu. Mijini ni maofisi na sehemu za biashara.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom