Wananchi wapagawa baada ya Bomoa bomoa kuwapitia Pugu

nimeangalia hapa naona mmejaza usiasa tu. iliyobomoa si ccm ni mmiliki wa eneo ndo kabomoa.
 
Tunatekeleza amri ya mahakama. Kwani mahakama ziko chini ya ccm ? Ninyi watu vipi ? Kuna mihimili mitatu au mkiwa na jazba mnasahau ???
 
Serikali ya ajabu hii badala ya kuwajengea watu nyumba badala yake inawabomolea
 
Hakuna mahali serikali itaacha kubomoa kama sehem za waz tunaziingilia halafu mnajenga mabanda ya kufanya biashara,,haiwezekan tusiangalie upande mmoja tu washilingi
Mbona machinga tunawaacha wafanye biashara barabarani ksbu ni wanyonge kwani wanatofauti gani na hao kinamama
 
Kila MTU atabeba msalaba wake kamsemo fulani kalitolewa juzi huko kagera.
 
Wanadhulumiwa haki yao ? Daaaah 2020 watu wanahasira .milion 6 vs million 8.
Hata kama wakawa na hasira za nyoka koboko mwenye kichwa cha kufanana na jeneza kwa katiba hii hata aje nani labda Yesu arudi ndo mtalitoa dubwasha sisiemu madarakani!!!
 
Ni lazima Watanzania waishi kama mashetani THANKS to dikteta uchwara.


Zaidi ya mabanda 30 ya wafanyabiasahara wa eneo la Pugu Bombani yamebomolewa majira ya usiku wa saa tisa na nusu kuamkia leo kufuatia mgogoro wa muda mrefu kuhusu umiliki wa eneo hilo.
 
Kila Mtu abebe Msalaba wake... Kama eneo sio lao kwanini waligoma kuondoka? Je na wao watakubali watu waje kwenye eneo lao wajenge na kufanya biashara? hapo unakuta walishabembelezwa zaidi hata ya mara mbili...

Ila hawa sio Machinga sidhani kama Magu atawasikiliza...
 

Zaidi ya mabanda 30 ya wafanyabiasahara wa eneo la Pugu Bombani yamebomolewa majira ya usiku wa saa tisa na nusu kuamkia leo kufuatia mgogoro wa muda mrefu kuhusu umiliki wa eneo hilo.

Hata kama eneo si lao ni sawa,,lakini kwanini wabomoe usiku na siyo mchana..Ili hali watu wanabidhaa katika vibanda vyao,,ifike sehemu tutambue haki ya kila binadamu,,pasipo kujali uchumi wake...
 
Kama nikweli wamebomolewa usiku,basi kuna nia ovu juu ya ubomoaji huo.

Hivi imeshindikana kumaliza hili swala la bomoabomoa kwanjia za kistarabu kwa miaka nenda rudi!,kila kukicha ni bomoa bomoa tuu tena kwenye maeneo ya akina pangu pakavu tuu.

Mbezi beach kwa vigogo waliojenga hadi ufukweni mwa bahari hakuguswi,kazi mikwara tuuu.
 
Back
Top Bottom