Wananchi wa Uganda wasaini waraka ili Rais Museveni afikishwe kwenye Mahakama ya ICC

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,170
5,528
ZAIDI ya wananchi 800 wa Uganda wamesaini waraka wa kushinikiza kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.

Kampeni hiyo inayokusudia kukusanya kwa takriban saini milioni mbili inaongozwa na kinara wa upinzani nchini humo Dakta Kizza Besigye, ambaye alikuwa mkuu wa chama cha Forum for Democratic Party (FDC).

Iwapo watafanikiwa kukusanya sahihi hizo, watawasilisha waraka huo kwa mwendesha mashitaka wa ICC, ili kuanzisha mchakato wa kufunguliwa faili la jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu dhidi ya Museveni katika mahakama hiyo iliyoko mjini The Hague nchini Uholanzi.

Baadhi ya ushahidi dhidi ya Museveni ambao wapinzani wanategemea kwenye kesi hiyo, ni mauaji ya watu 100 wakati maafisa usalama walipovamia makazi ya mfalme wa kitamaduni, Omusinga Charles Wesley Mumbere katika mji wa Kasese miezi kadhaa iliyopita.

Wapinzani nchini Uganda wanalalamika na kuituhumu serikali ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kwamba, imekuwa ikiendesha siasa za mkono wa chuma dhidi ya mrengo wa upinzani, hatua ambayo wanaitaja kuwa, inakandamiza na kubinya demokrasia katika nchi hiyo.

Rais Museveni ambaye amekuwa akiongoza Uganda tangu mwaka 1986 anatazamiwa kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 na kuendelea hadi mwaka 2026, baada ya bunge la nchi hiyo kufuta kipengele cha sheria juu ya ukomo wa umri wa kugombea urais nchini humo.


Chanzo: Pars Today
 
Suley2019,

Na hapo Museven ameacha huru kidogo bunge, mahakama na vyama vya siasa! Huyu wa kwetu atahakikisha anatuchapa shaba wote kabla hata hatujaanza kusaini!!
 
Back
Top Bottom