Wananchi jukumu letu ni lipi kwa sasa?

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Naona watanzania tumeendeleza malumbano ya kampeni hata baada ya miezi 6 ya serikali mpya!

Nilichogundua ni mkwamo uleule wa miaka 10 ya kumbishia kikwete na utawala wake ambako naona mchezo unaendelea!

Kususia au kuchukia tawala kumeiangusha sana nchi yetu, inawezekana kabisà katika kipindi cha miaka 20 iliyopita tumeendelea kwa kiasi kikubwa ingawa ninaamini kuwa kwa kipimo chochote kile, hatua tuliyoipiga bado ni fupi kuliko tuliyostahili kwenda!

Kwa wenye chuki au wanaosusa, bado wamekuwa hawashiriki kutoa michango yenye tija, wengi tumebaki kukosoa! Kitu ambacho kina uzuri wake, lkn kinapozidi kipimo huwa hakina tija kwa kuwa lawama huwa zinapunguza morally lkn pia hamu ya kumsikiliza mkosowaji kila siku hupungua kwa kadri unavyojiona kuwa hufaidiki na lawama!
Lakini ukosoaji pia umekuwa wa kubeza na unaoambatana na matusi au dharau, mfano. Raisi aliyemaliza muda wake mh. Jakaya Kikwete aliambulia matusi na kebehi, kuna udhaifu ktk serikali yake, lakini zuri lipi ambalo lilitukuzwa ili kumuandaa raisi aliyemfuata alienzi?

Utagundua kuwa kila alilolifanya watu wanaomchukia au waliosusia waliona kuwa halifai na ni bora tu jamaa aende zake, leo kuna vilio vinavyoashiria makosa yetu!

Wakati huu wa awamu ya tano, tumeanza tena kufanya yaleyale, tumesahau wosia wa baba wa taifa wa kuwa kiongozi huwa anafanya mambo mema na ya kijinga, hebu tushike Yale yaliyo mema! Haya yasiyo na tija tuyafanyie kazi pamoja! Tumkosoe Magufuli kwa sehemu anazoonesha udhaifu, lakini tusisahau kusifu penye mambo mazuri!

Lakini kama raia wa nchi hii, ni wajibu wetu namba moja kutenda yaliyo mema kwa taifa letu na si kukaa kama fisi kusubiria kuona serikali itakosea wapi ili tuuze magazeti au tupate story kijiweni!

Mimi naanza kwa kusifu uwajibikaji ktk awamu hii, usimamizi wa baadhi ya sheria, kusimamia kodi hasa ktk makusanyo na kulinda rasilimali za nchi zisichezewe! Hii ni hatua kubwa sana mheshimiwa!

Shida kubwa tunaona ktk elimu na gharama kubwa za bidhaa madukani na masokoni! Bidhaa ina factor nyingi mchakato wake ni mgumu maana unahitaji maridhiano pia na wafanyabiashara, lakini hili la elimu nadhani ni la haraka na limo ndani ya watendaji wa serikali!

Tunahitaji kuzijengea ubora shule zetu!
Kama tulivyoanza na shule za kata, sasa quality ijengwe kwa shule za kanda ambapo kila mkoa ungepaswa utengeneze angalau shule moja itakayokuwa special na kila kanda iwe na idadi kadhaa ya special schools kulingana na idadi ya mikoa ndani ya zone!

Hizi shule ziboreshwe kwa level ya mzumbe, tabora msalato etc za enzi hizo! Wale wenye ufaulu wa juu ktk zone waende shule hizo na kila mwaka ziongezwe taratibu hadi tutakapo stabilise kila idara! Ubora wa shule hizi uwe ni idadi ya walimu, maabara, library, vitabu na mazingira!

Kwa sasa tupo wazazi ambao ada ya serikali sio shida Ila shule za umma ndio hamna, yaani huwezi kupeleka mtoto kwa bure maana inakuwa bure kila kitu hata elimu yenyewe ni bure tu hamna kitu kabisa!
 
Uchaguzi umekwisha na Magufuli ndiye rais wetu tuliyemchagua, tuachane wachumia tumbo wanaofata siasa za matukio , watanzani tuchape kazi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…