Baada ya Rc wa Dar kufanya uvamizi katika kituo cha habari cha clouds, kulifuatiwa kikao cha bodi ya wahariri kulaani vikali kitendo hicho na kutangaza hatua za kutokurushwa au kuripoti habari inayomuhusu mkuu huyo sehemu yoyote ile katika vyombo vya habari na kwa namna yoyote!
Hapo jana tarehe 29 march 2017, kiapo na makubaliano ya wahariri yalivunjwa!
Uvumilivu uliwashinda na kuamua kumtangaza mkuu wa mkoa bwana Paul Makonda almaarufu kama Bashite
Hii ilifuatiwa kuhusika kwake kuitikia wito wa kamati ya bunge
Hiyo jana haikua ITV wala media zingine, zote zilimpa mkuu hui air time ya kutosha
bila shaka hata magazeti yote ya tareh 30 leo yataipa habari hii kipaumbele
Je huu ndio utakua mwisho wa makubaliano ya wahariri kuhusu kutokurusha habari yoyote ya Makonda?
Ni nini kimewakuta wahariri kiasi kwamba wanayumbishwa na kukosa msimamo kusimamia wanayoafikiana?
Mkuuu wewe ndio umetoa povu zaidiInawezekana utekelezaji wa yale maamuzi ya TEF na MOAT hukuyaelewa Mkuu hivyo nikusihi tu tuliza akili zako yatafute kisha naamini ukiyasoma na kuyaelewa vizuri hutorudia tena kupovuka hivi.
Waswahili bhana!!!!!!!
Kwa mantiki hiyo basi Makonda hakwepeki na wanahabari!Mimi nilielewa tofauti: nadhani kilichosemwa ni kwamba habari zinazomhusu RC Makonda yeye kama yeye hazitaandikwa (mfano kama anazindua mradi, kama anahutubia mkutano etc), lakini habari zinazohusu (mfano kamati ya bunge ya maadili kumhoji) hizi zitaandikwa kwa sababu focus ni hiyo kamati na mahojiano naye. Ndivyo nilivyokuwa nimeelewa mimi wakati wanahabari wanatangaza kususia kuripoti habari zake.
Kasome front page magazeti ya leo kama utaona bunge kwa haraka haraka tu pitia yoteKwa uelewa wangu..nilielewa hawata andika issue za Makonda kama yeye..ila zinazoelezea makosa yake wata report tu...mfano makonda anaenda kuzindua kisima..Awataandikia, ila Makonda kakamatwa na police watandika...ndo.maana issue ya kuojiqa na Bunge wameandika. Kwa ufupi hawata andika issue zinazo mpa positive impact ila Negative tu..
Habari ni ya RC Mkakonda na sio ya Bunge. Polisi wakikamata bangi habari huwa ni bangi iliyokamatwa na sio polisi waliokamata.Wewe unavyoona hii habari ni ya RC au ni bunge?
Kwa mantiki hiyo basi Makonda hakwepeki na wanahabari!
Yale maamuzi yalikuwa ya kukurupuka yatazamwe upya