Wanafunzi Waliohitimu kidato cha sita Mwaka 2022 waitwa JKT

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena amewaita vijana wote waliohitimu kidato cha sita 2022 kutoka shule zote za Tanzania Bara kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali Mabena ametoa wito huo leo Jumanne Mei 31, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo kwa mwaka huu, akiwataka kuanza kuripoti kuanzia Juni 3 hadi 17 katika makambi waliopangiwa.

Kwa mujibu Brigedia Mabena, vijana hao wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma, Msange, Ruvu, Mpwapwa, Makutupora, Mafinga, Makuyuni, Kanembwa, Itaka, Mlale, Mgambo, Oljoro, Milundikwa, Nachingwea, Kibiti Bulombwa na Maramba.

"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Kambi hii ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hii.

"Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele awakaribisha vijana wote walioitwa ili kujiungna katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi na maisha, utayari kulijenga na kulitumikia Taifa,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
 
Back
Top Bottom