Uchaguzi 2020 Wanachama wa CHADEMA kuchukua fomu za Urais kupambana na Mbowe, lakini kutifanya hivyo katika kuwania uenyekiti wa chama ni ishara gani?

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,617
Ninapata taabu kidogo kuelewa falsafa ya CHADEMA katika hili. Miaka yote ya nyuma hadi uchaguzi mkuu wa chama cha CHADEMA uliofanyika mwaka Jana, ulionyesha kwamba, kiongozi mmoja anayeaminika na chama hicho, ndiye anakua mgombea pekee kuwania nafasi za juu za Chama na Uchaguzi mkuu wa nchi.

Haijawahi kutokea pale ambao Chama cha Upinzani kina lengo na uhakika wa kutoa upinzani mkubwa, na uwezekano wa kushinda kiti cha Urais, kukawa na wagombea wengi wanajitokeza ndani ya Chama kuchukua fomu kama ilivyojitokeza kipindi hiki, Mara zote chama huwa na mtu mmoja wanayomuamini, na wanachana wengine wote huwa nyuma yake, kamwe hawatokei wengine kuchukua fomu kupinga na naye.

Falsafa hii ya kumuachia mtu mmoja mwenye nguvu na uwezo katika nafasi kubwa katika chama(Kama ilivyofanya CHADEMA katika nafasi ya uenyekiti wa chama kwa kumuachia Mbowe), japo katika mtazamo wa demokrasia haipendezi, lakini inasaidia sana kujenga umoja ndani ya Chama, Mara nyingi baada ya uchaguzi wale walioshindwa hubaki na kinyongo, na wengi ujitoa katika chama, au kuna kuwepo na mgawanyiko ndani ya Chama, kama ilivyotokea katika uchaguzi wa CCM kumpata mgombea wao wa Urais mwaka 2015, na ndani ya Chadema ambapo mzee Sumaye alijitoa.

Jambo linaloleta ukakasi kwa sasa ndani ya CHADEMA ni kwamba, miezi kadhaa nyuma, CHADEMA ilifanya uchaguzi wao mkuu wa chama, ambapo wanachama waliamua kutochukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama kwa madai kwamba, Mbowe ana uwezo mkubwa hivyo hakuna sababu ya kumpinga, lakini katika nafasi ya urais wa nchi, wameibuka wana chama wengi wa CHADEMA wanaodhani wao wanao uwezo mkubwa zaidi ya Mbowe, hivyo wanaomba wanachama wa CHADEMA wawapitishe na kuwapa ridhaa waweze kupeperusha bendera ya CHADEMA, kwa maana ingine waachane na Mbowe.

Maswali ya kujiuliza;

Je ni kweli kwamba Mbowe anao uwezo mkubwa wa kuongoza CHADEMA kuliko mwanachama yeyote hivyo kustahili kutopingwa katika uchaguzi wa Chama?.

Je ni kweli kwamba Mbowe hana uwezo wa kipekee katika nafasi ya urais wa nchi, hivyo abastahili kupingwa na wanachama wengine?

Inawezekanaje demokrasia ya kugombea nafasi za juu kwa wana chama wengi kujaza fomu za kuomba nafasi ya urais kupitia CHADEMA, imetokea kipindi hiki ambacho ni wazi kwamba nguvu za vyama vya upinzani kwasababu moja au nyingine ni kama haipo?.

Je ni dalili kwamba upinzani umeona uwezekano wa kushinda urais haupo kwahiyo wanataka kutumia uchaguzi huu kama zoezi la kujifunza demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyao?.

Naomba kuwakilisha.
 
Back
Top Bottom