Waliokuwa wakisema mkataba wa DP World uko sawa kwa sasa wana maoni gani baada ya mkataba kurekebishwa?

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
495
773
Takribani miezi michache iliyopita baadhi ya wachumia tumbo bila ya kusikiliza maoni ya wananchi walikuwa wa kwanza kusema kuwa mkataba wa DP world uko safi na kuutangaza Kwa gharama yoyote Ile ili watu waamini kuwa ulikuwa safi Kwa maslahi ya taifa.

Jana umesainiwa mkataba uliofanyiwa maboresho kufuatia malalamiko na maoni ya wananchi wakiwemo wasomi, waraka wa kanisa mama katoliki la Mitume.

Sasa naomba kujua wale wanafiki, wachumia tumbo, chawa Wana maoni gani tena juu ya huu mkataba uliosainiwa kwa kuzingatia maoni ya wananchi?
 
Sijajua uliporekebishwa ni wapi ila nachojua na nachokumbuka ni kwamba Serikali ilisema wazi kwamba hakuna atakayepoteza Ajira na mikataba ya kazi itasema ukomo wa utekelezwaji Sasa wale wengine wa Nchi imeuzwa, tumepigwa mnada ndio watueleze umerekebishwa sehemu zipi?
 
Hawakusema ufutwe, walisema vipengele vya kimangungo virekebishwe
Huenda wewe ulikua huendi kudhuria ibaada za kanisani na kusikiliza waraka unasomwa vizuri........vipengere vi bomvi vilikua zaidi ya 15, wamesemea 7 tu hapo kwenye marekebisho vip vingine?
 
Ni mikataba 3 tofauti kenge wewe.
Mkataba wa gati 0 hadi 4, mikataba wa gati 5 hadi....... na mkataba wa.......!
Hiyo ni mikataba na si maboresho
 
Takribani miezi michache iliyopita baadhi ya wachumia tumbo bila ya kusikiliza maoni ya wananchi walikuwa wa kwanza kusema kuwa mkataba wa DP world uko safi na kuutangaza Kwa gharama yoyote Ile ili watu waamini kuwa ulikuwa safi Kwa maslahi ya taifa.

Jana umesainiwa mkataba uliofanyiwa maboresho kufuatia malalamiko na maoni ya wananchi wakiwemo wasomi , waraka wa kanisa mama katoliki la Mitume.

Sasa naomba kujua wale wanafiki, wachumia tumbo, chawa Wana maoni gani tena juu ya huu mkataba uliosainiwa kwa kuzingatia maoni ya wananchi?.
Wewehuelewi unachokiandika, mikataba iliyosainiwa jana haikuwepo kabla, ule mama wa IGA upo pale pale.

Tatizo nini?
 
Unge anza kuuliza wale walio sema kwamba mkataba wote haufai ufutwe sasa wako wapi?
Hao hawana mamlaka kwenye serikali tuanze na wenye mamlaka waliosema mkataba upo sawa hao wengine wameshika kwenye makali kelele zao ni sawa na bure.
 
Hao hawana mamlaka kwenye serikali tuanze na wenye mamlaka waliosema mkataba upo sawa hao wengine wameshika kwenye makali kelele zao ni sawa na bure.
Unawakika kweli kwamba IGA imebadilishwa? Uliona mabadiliko yana pelekwa bungeni, au na wewe ni layman......umenswa kwenye danganya toto.
 
Kama vipengele vipi? Ujue nyie Suku gang na Machadema Huwa mnaropoka na kupayuka hovyo.

Tena mbaya zaidi likawa la kidini watu wakaanza kupinga Waarabu badala ya mkataba
Professor Mruma alibisha hivi hivi kuwa vifungu vya mkataba vipo sawa juzi tumelipishwa mabilion ya hela kwa mikataba mibovu tumerogwa na nani kwenye kesi za mikataba hakuna hata kesi moja tuliyowahi kushinda siku hili bomu likilipuka tushakuwa wazee tayari.
 
Kwani tumelipishwa kwa kuwa vifungu havipo sawa?

Tumelipishwa kwa kujimwabafai. Kama ulikuwa huelewi.
 
Unawakika kweli kwamba IGA imebadilishwa? Uliona mabadiliko yana pelekwa bungeni, au na wewe ni layman......umenswa kwenye danganya toto.
Ipo siku tutaongea lugha moja kwani mikataba mingapi ccm mnasema iko sawa halafu bomu likija kulipuka tunatozwa mabilion ya hela ya fidia watu washakula hela za udalali ulitegemea waanze upya sisi yetu macho mungu atupe uzima tutarudi tena hapa kuujadili huu mkataba bomu likilipuka siku moja kiufupi mikataba yote tunayoingia kama nchi tumepigwa.
 
Kwani tumelipishwa kwa kuwa vifungu havipo sawa?

Tumelipishwa kwa kujimwabafai. Kama ulikuwa huelewi.
Lakini source ni mkataba mibovu ambayo ni professional rubbish njaa mbele taifa nyuma ila hii nchi sijui kwa nn lile bomu la hamas wasingelipiga pale kwenye kijani tuanze upya mtu ana miaka 70 bado anawaza ufisadi badala ya kuwaza next generation itaishije
 
Back
Top Bottom