Wadau,
Kwanza nipongeze hatua ya kuweka ulinzi eneo la daraja na kwenye barabara zinazotoka na kuelekea Nyerere Bridge. Naamini Lengo na madhumuni yalikuwa kwa manufaa ya watumuaji wa daraja.
Cha kushangaza walinzi wa SUMA JKT wamekuwa kero badala ya msaada.
Kwa mara kadhaa nimeshuhudia walinzi hawa wakisimamisha magari na pikipiki na kuanza kukagua. Kwa wanaoelewa huwaeleza kuwa hiyo si kazi yao na huwaachia bahati mbaya wapo wasiolewa, hawa huingia kwenye mtego.
Nimesaidia watu watatu baada ya kukamatwa na niliamua kusimama na kuuliza kinachoendelea, ndipo nikawaeleza walinzi hao kuwa wanachofanya sio sawa. Na niliamua kutoa taarifa kwa trafiki waliopo eneo la barabara ya Mandela, sijui hatua walizochukua.
Jana saa 12.20 jioni ndipo nikashihudia jambo baya zaidi, kijana mwendesha bodaboda akiwa anatokea Kurasini kuelekea darajani alikuwa anasimamishwa ghafla na mlinzi wa SUMA JKT na kwa kuwa Ilikuwa ghafla hakuweza kusimama na ndipo Mlinzi huyu alimfuta mwendesha pikipiki huyu aliposimama na kuaza kumpiga mateke akiwa juu ya pikipiki na hatimaye kijana huyu yeye na abiria wake wakaanguka.
Mlinzi huyu alikuwa akidai kwanini mwendesha pikipiki amesimama mbali. Nilishuka kwenye gari na kuamua kumzuia huyu mlinzi kumpiga Dereva wa bodaboda.
Niliamua kufikisha malalamiko yangu kituo cha Polisi Darajani Kama mita 150 kutoka eneo la tukio cha ajabu Polisi alinijibu kuwa hayo mambo Mimi hayanihusu niwaachie Wao watashughulikia.
Ninapoandika hapa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya Dereva wa bodaboda kuambia aende akajitibie na kesi imeishia hapo.
Naona jambo moja hapa, hawa walinzi kuvaa sare zenye jina la SUMA -JKT inawafanya baadhi ya Wananchi wasiojua kudhani kwamba hawa ni askari wa Jeshi la Kujenga taifa hivyo kuheshimu kila wanachoambiwa hata Kama ni kinyume na taratibu.
Hili halitaishia hapa nina appointment na mmoja wa wakuu pale wizara ya mambo ya ndani Ili kufikisha malamiko yangu.