20PROFF
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 8,147
- 7,128
Ni siku mpya. Ilete baraka na mabadiliko chanya, Ona na visualize ukifakiwa, (Sema Amen).
Niwape kisa kimoja, kiwe funzo na chachu ya kujiongeza next time, maana watu tunakurupuka na hizi silaha zetu tulizo nazo.
Jana nilikuwa ktk daladala moja naelekea Karume. Konda na dereva wake, wote walikuwa wachaga (lafudhi yao). Wachaga muda wote wapo serious na hela, konda na abiria mmoja wakapisha kauli. Dereva na konda ni kama meno ya mbwa hayaumani, dereva aka mpa back up ya maneno yule konda wake.
Yule abiria alionekana kuchoka, mavazi, hata sura imefubaa. Kwa kumsoma utajua nature ya kazi yake ni ngumu ngumu, hao watu wanakuwaga kama mti mkavu, au tuseme chuma cha reli kidogo lakin ubeba treni.
Kisa cha utata jamaa alipitishwa kituo kwa utata tu wa konda basi ntakushusha mbele, hakuwa anajali. Utarudi nyuma tembea ufanye zoezi we mwanaume. Jamaa akadai nauli yake ,ndio kukawaka moto.
Dereva akaweka maneno yake, kosa likawa kusimamisha gari. Dereva si akatoa rungu ampe konda, akisema shika mchape nalo.
Yule jamaa, akashushwa chini, konda anataka amchezesha na rungu, Kwa ushikaji wake tu unajua fika huyu hajui ishu za marungu, wana kaa nayo kutishia tu.
Kilicho fata, before hara rungu halija nyanyuliwa vizuri, konda anapiga yowe huko kawekwa mtu kati, dereva akashuka na silaha nyingine , wote wakawekwa mtu kati, wanaishia kutukana tu.
Hivi kweli mwanaume unatangaza kwa nguvu konda chukua rungu hili mpige na mhusika anasikia. Na huyo konda eti anamnyooshea eti, unarungu hili! Huku akichimba mabiti.
Kama hujui kuitumia silaha, usiende nayo ktk ugomvi itageuka faida kwa adui yalo na hasara kwako. Ficha uwepo wa silaha yako, iweke vyema iwe kama sehemu ya mwili wako kama mkono wako wa ziada.
Gari zima likabaki kuwa cheka.