Wakuu, vazi la kanzu ni kwa ajili ya Waislam au watu wote?

Kazu

Kanzu sio vazi takatifu, ni vazi la kale kwa jamii ya mashariki ya mbali na mashariki ya kati, ni vazi la kawaida tu, hata wahaya ni vazi lao la kitamaduni, hakuna uhusiano wowote wa Kanzu na dini kwani ukienda msikitini hujavaa kanzu swala yako inakuwa batili?, mtakuja sema kuwa tende ni matunda ya kiisilamu kwamaana yanapatikana sana wakati wa mfungo wa ramadhani, kisha mtesema kuwa tende ni matunda matakatifu. Kuhusu usahili ukiwa umvaa kanzu. Hii inaoneka ni ajabu kwaajili ya mfumo wa kimagharibu uloingia vichwani mwa watu, ukienda nchi za kiarabu vazi hili ni kama utamaduni tu.
Hivi umeambiwa ni vazi la Kiislam au vazi takatifu?! Mbona umeganda sana kwenye Uislamu hadi unatoa mifano ya tende?! Hata Bible yenyewe wakati inazungumzia mavazi ya Haruni; moja wapo halikuwa ni kanzu na hatimae kuyaita mavazi takatifu?!

"Na mavazi watakayoyafanya ni haya: Kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo, na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Harun nduguyo, na wanawe; mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya Ukuhani. (Kutoka 28:4)"
 
Kanzu siyo vazi takatifu ni vazi la utamaduni watu wa mashariki ya kati soma historia utaelewa ilo ni vazi tu ambalo tumeiga utamaduni wa watu kutoka mashariki ya kati
 
Aisee kweli hii inaonyesha hata Upande wa pili Nyumba za Ibada hawajui nini kinaongelewa wala kuijua hiyo yao Dini ilivyo na historia ya Mitume na maisha yao.Ila sishangai,maana ukienda umelewa unategema utaelewa jambo kweli.
Sasa pale kanisani huwa mnavaa Blauzi au Bambino lile
 
Mbona sadam alikuwa havai kanzu? Mbona gadafi alikuwa anavaa joho na si kanzu?
 
e7d074873a3ec4ac518c42f430d63e2d.jpg

Mimi ni mkristo, juzi nilivaa kanzu...ndugu yangu mmoja akashangazwa sana...akaniambia naogopa utapotea..nilimshangaa maneno yake ya kibaguzi kwa hoja kuwa;

Kanzu ni vazi takatifu ambalo hata yesu na mitume walivaa

Ushauri wenu wakuu...je dada yangu yupo sawa au yeye ndio kapotea?

Hakuna mahali pasipo na misikiti, if ur serious why don't you go in one of them and get authentic answer?
 
Dada yako hayupo sahihi, kanzu ni va heshima na takatifu ndio maana watu kama wahaya wanalithamini hata wasipokuwa waislamu kwao ni vazi maalum la kutolea mahari na kuvaa shereheni, ni vazi heshima maana hata Yesu na Mtume walivaa mavazi haya na hayakufanyi kuwa muislam maana dini ni imani
Hata Waganda kwao ni vazi la heshima
 
Hata yesu ambae ni kinara wa wakristo alikuwa anavaa kanzu mkuu ila simaanishi kuwa kanzu ni vazi la kila mtu bali namaanisha kanzu ni vazi la kitamaduni zaidi!
 
Kanzu ni vazi la watu wa uarabuni (Jangwani)....

Kanzu haina uhusiano na imani ya dini...Kama ilivyo mgolole kaniki na hata rubega kwa makabila yetu ya kiafrica.....

Hitimisho:- Kanzu ni vazi...Ila kwa vile wenzetu waislamu wameliteuwa kuwa vazi la kuendea kuabudu mungu basi lipewe heshima kwa sie tusiokuwa waislam tusilivae na kuenda nalo sehemu zisizostahili kama ma baa na ma guest hauzi.
Kama waarabu wa China ehn
 
Vaeni na Magome maana hata Mtume wenu Adam alivaa Magome ni Mavazi matakatifu...
 
kanzu ni vazi la kawaida lilikuwepo kabla ya uislamu na ukristo, watu wengi walikuwa wana vaa kwani kipindi hicho kulikuwa hakuna nguo zingine nzuri za heshima zaidi ya kanzu. Tuondoa fikra za kukalili
 
e7d074873a3ec4ac518c42f430d63e2d.jpg

Mimi ni mkristo, juzi nilivaa kanzu...ndugu yangu mmoja akashangazwa sana...akaniambia naogopa utapotea..nilimshangaa maneno yake ya kibaguzi kwa hoja kuwa;

Kanzu ni vazi takatifu ambalo hata yesu na mitume walivaa

Ushauri wenu wakuu...je dada yangu yupo sawa au yeye ndio kapotea?
1. Wanaume wasio mitume walivaa vazi lipi?
2. Tangu lini utakatifu unakaa kwenye vazi?
3. Wewe sio mkristo
 
Dada yako hayupo sahihi, kanzu ni va heshima na takatifu ndio maana watu kama wahaya wanalithamini hata wasipokuwa waislamu kwao ni vazi maalum la kutolea mahari na kuvaa shereheni, ni vazi heshima maana hata Yesu na Mtume walivaa mavazi haya na hayakufanyi kuwa muislam maana dini ni imani
Ukivaa kanzu lazima uvae baragashia kama alivyidai yule mbunge wa CCM?
 
Back
Top Bottom