Wakuu, ushauri na mawazo yenu yanahitajika

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,806
9,300
wakuu habari zenu

Msaada wenu unahitajika sana,
Nina mdogo wangu amesoma famasi ana diploma yake na kutokana na ugumu wamaisha kupata ajira imekua shughuli pevu mdogo wangu huyu ameamua kujiajiri kwa kutafuta kaeneo kake afungue angalau duka la dawa muhimu.

Mimi kama kaka yake nimekuballiana naye vizuri tu juu ya maamuzi yake ya kujiajiri kwa kufungua duka la dawa, lakin shida inakuja kwenye kutafuta eneo zuri linalofaa kwa biashara hiyo

Kwa shida hiyo yani mdogo wangu amekuwa akizurula tu kutafuta eneo la biashara na sehemu zote anazoenda anasema hapafai anaweza asipige pesa, na mwisho anajikuta akichagua chagua tu na kuacha bila kufanya hatua nyingine

Kwa hiyo ndugu zangu wa jf, naombeni ushauri wenu.

Kwanza; kwenye eneo, ni maeneo / mazingira gani yanafaa kwa biashara hiyo ya duka la dawa.

Pili; naombeni ushauri wenu na mawazo pia kwenye swala zima la hii biashara ya duka la dawa.

Wakuu, nisaidieni mimi na mimi nikamsaidie dogo na dogo aje kunisaidia mimi badae then the circle continue...

Nawasilisha.
 
Biashara ya dawa inalipa sana, ila kwa upande wa eneo subiri wenyeji waje. Hata hivyo naona umeweka taarifa hafifu, hujasema eneo ambalo huyo mdogo wako yupo
 
Tukusaidie,ukamsaidie halafu aje akusaidie na wewe uje utusaidie......

Biashara zote ni Ngumu.Eneo linalofaa kwa biashara hii ni maeneo ya karibu na Hosp au karibu ni makazi ya watu.Kwa sababu amesoma Pharmacy najua hatashindwa ila cha muhimu kiwango cha mtaji.
 
yeye anaishi dar es salaam wilaya ya temeke, mbagala.. lakini fursa inaangaliwa popote mkuu.
 
Kanuni za ufunguaji DLDM ni kwamba unatakiwa ufungue Duka baada ya nyumba zaidi ya kumi upande wa kulia na kushoto sehemu yoyote unauza hasa uswahilini ambapo kuna mazingira hatarishi ya kiafya
 
Tukusaidie,ukamsaidie halafu aje akusaidie na wewe uje utusaidie......

Biashara zote ni Ngumu.Eneo linalofaa kwa biashara hii ni maeneo ya karibu na Hosp au karibu ni makazi ya watu.Kwa sababu amesoma Pharmacy najua hatashindwa ila cha muhimu kiwango cha mtaji.
haha naona umeielewa circle ya kusaidiana

Asante kwa ushauri wako.
 
wakuu habari zenu

Msaada wenu unahitajika sana,
Nina mdogo wangu amesoma famasi ana diploma yake na kutokana na ugumu wamaisha kupata ajira imekua shughuli pevu mdogo wangu huyu ameamua kujiajiri kwa kutafuta kaeneo kake afungue angalau duka la dawa muhimu.

Mimi kama kaka yake nimekuballiana naye vizuri tu juu ya maamuzi yake ya kujiajiri kwa kufungua duka la dawa, lakin shida inakuja kwenye kutafuta eneo zuri linalofaa kwa biashara hiyo

Kwa shida hiyo yani mdogo wangu amekuwa akizurula tu kutafuta eneo la biashara na sehemu zote anazoenda anasema hapafai anaweza asipige pesa, na mwisho anajikuta akichagua chagua tu na kuacha bila kufanya hatua nyingine

Kwa hiyo ndugu zangu wa jf, naombeni ushauri wenu.

Kwanza; kwenye eneo, ni maeneo / mazingira gani yanafaa kwa biashara hiyo ya duka la dawa.

Pili; naombeni ushauri wenu na mawazo pia kwenye swala zima la hii biashara ya duka la dawa.

Wakuu, nisaidieni mimi na mimi nikamsaidie dogo na dogo aje kunisaidia mimi badae then the circle continue...

Nawasilisha.
Atafute eneole lenye wakazi wengi,ikiwezekana karibu na shule,chuo,soko nk
 
Back
Top Bottom