Wakurugenzi TANESCO wasimamishwa kazi, mmoja ajiuzulu!

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Safisha safisha bado inaendelea katika serikali hii, ambapo leo wakurugenzi wote Tanesco wamesimamishwa kazi ili kuondoa uozo uliokuwepo ndani ya shirika hilo

[HASHTAG]#Hongera[/HASHTAG] Muhongo
[HASHTAG]#Hongera[/HASHTAG] Dr. Tito Mwinuka

======

=====
Hali si shwari ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambapo ikiwa ni siku chache tangu Rais Dkt Magufuli alipotengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba kufuatia ongezeko la gharama za umeme kwa asilimia 8.5 mabadiliko mengine ya uongozi yamefanyika ndani ya shirika hilo.

Wakurugenzi watatu waliokuwa wakihusika katika vitengo mbalimbali ndani ya shirika hilo wameshushwa vyeo na kuhamishia katika chuo cha TANESCO (TSS) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Walioshushwa vyeo na kuhamishwa vituo vya kazi ni pamoja na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji na Huduma kwa Wateja, Mhandisi Sophia Mgonja ambaye nafasi yake imechukuliwa na Joyce Ngahyoma, mwingine ni aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usafirishaji, Mhandisi Declan Mhaiki ambaye nafasi yake imechukuliwa na Kahitwa Bashaija.

Mkurugenzi wa tatu aliyekumbwa na panga hili ni aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji, Nazir Kachwamba ambaye nafasi yake imechukuliwa na Abdallah Ikwasa. Wakati huo huo, aliyekuwa mratibu wa ujenzi wa mradi mpya wa umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga amechukua nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uwekezaji.

Katika hatua nyingine, inaelezwa kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu, Watson Mwakyusa ameamua kuachia ngazi mwenyewe.

Chanzo: Swahili
 
Kwa ninavyomuelewa Mwinuka labda kashawishiwa na Muhongo.
 
Na bado tumeshaona nini?
kilichoniacha kinywa wazi ni ile kupandishwa kwa bei ya umeme na kuja nyuma kusitisha

Maswali yangu je huo mchakato ulikuwa wa kimya kimya? jibu hapana swali kulikuwa na sababu gani kutoisitisha huko anasubiri itanganzwe aje asitishe jibu sijui

hapo hapo Mramba mkataba ukasitishwa TOBA!!!!! tutayaoa mengi kwa kweli

Mungu tupe afya

"wonders never end"
 
Tanesco inatakiwa kusafishwa kabisa wala hilo halina ujanja.......

Muhongo nayeye simwamini toka alivyowakutanisha Rugemalila na Singa Singa........

Tanesco ni most corrupt govn institution in Tanzania..........

Magufuli akiendelea kuwachekea iptl na kuwalipa Milioni 400 kwa siku ..........

Kuna siku Tanesco itafilisi nchi.......
 
Tunatukuza umaskini, anaye UA yanesco ni muhongo. Tanesco walikua na miradi lukuki hydro, wind, solar, gas, lakini ameua yote umebaki was gas na kununua umeme toka Ethiopia.
 
Safisha safisha bado inaendelea katika serikali hii, ambapo leo wakurugenzi wote Tanesco wamesimamishwa kazi ili kuondoa uozo uliokuwepo ndani ya shirika hilo

[HASHTAG]#Hongera[/HASHTAG] Muhongo
[HASHTAG]#Hongera[/HASHTAG] Dr. Tito Mwinuka
Uzur wa kusimamishwa kazi unaendelea kupokea mtonyo,na unapewa nafas ya kuendelea na mishe zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…