Wako wapi Man Dojo na Domokaya?

enzi yao imeisha.sidhan kama wana mpango wa kutoa nyimbo.ila kiukweli walikuwa wakali.wazee wa taswira.
warudi tuu maana wana fanbase kubwa kuliko maana vijana wa mika ya 90 na kuendelea ndo tunawafahamu na ndio vijana wenye nguvu kwa sasa.
 
Kiukweli hapo umenena mkuu....
Siku zile jamaa walikua wabunifu na wajuvi wa mitengenezo ya mirindimo kwa kupangilia sauti zao aiseeee.....
kuacha sauti tuu hata ujumbe ndani ya ngoma zao vilikua ni chachu ya maadili ya vijana wengi
 
Hawa jamaa ni ndugu au ni urafiki tuu? Maana mpaka leo wapo pamoja tena wanashirikiana kwenye biashara pia!

Hapa kuna funzo la kujifunza kutoka kwa hawa jamaa aisee! Wako pamoja bega kwa bega kwa muda mrefu sasa!
 
Ni marafiki tuu ila walisomaga wote
 
Hawa jamaa ni ndugu au ni urafiki tuu? Maana mpaka leo wapo pamoja tena wanashirikiana kwenye biashara pia!

Hapa kuna funzo la kujifunza kutoka kwa hawa jamaa aisee! Wako pamoja bega kwa bega kwa muda mrefu sasa!

Kuna mdau kadondoka kwamba pamekuepo na uzi kadhaa hapa jf zikiwatanabaisha na kuwasema walipo, pia leo yao ya jana
 
muda mwingine mziki ni swaga za utotoni tuu mtu akikua anaacha....game lenyewe hili hutoki mpaka umezeshwe kete za ngada
ni kujituma hamna namna mbona Diamond anapasua kila kukicha na Ana maisha mazuri tofauti na wasanii wengine
 
Wameongea mengi
We unataka kujua kusuhu lipi

Mkuu....
Hapa jf tupo kwaajili ya kupeana taatifa/ habari sahihi, tena kwa ukamilifu
Lakini jf haitoweza songa kama kila mmoja atakua na tabia za kijuaji kama wewe.
Kimsingi namaanisha kwamba.... kilicho zungumziwa na wasaanii hao ndicho nimeomba tupashwe habari kwa faida ya jf member wote.

Ivo
 
Wanafiki nafiki watu wa kupakazia yasowahusu wao kuingilia, maneno yao ni kama ya Simba ukiyafikiria lazima utaangamia
Wanok nok watu wa.......
Nimewamiss sana, nimesikitika kuwa kumbe wanakula ile kitu
 
Back
Top Bottom