Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Nimesoma degree OUT na nilipata supp y masomo mawili.Sikukutana na mwalimu zaidi ya vitabu na internet na discussion no wakati wa mitihani ambapo unapata nafadi ya kuwajua wenzio.Si rahisi kama mnavyosema na nimeshuhudia MTU akisoma degree moja miaka mitano achilia mbali wanaokimbia.Dharau kwa watanzania in jambo LA kawaida lkn akija mweupe watu wananyenyekea kama wamemuona malaika.Tumezoa.
 
Hakuna Profesa yeyote makini atakayetaka kujioanisha (associate) na Chuo kama OPEN UNIVERSITY maana huko kutamporomeshea hadhi yake. We hujiulizi chuo kikuu cha umma kinakwepa kutoa kozi za uhitaji mkubwa hapa nchini kama MEDICINE, PHARMACY na nyininezo nyingi za mrengo wa SAYANSI ANGAVU (PURE SCIENCES) wao wamekalia BBA, SOCIAL WORK, PSYCHOLOGY na TOURISM ndo ujue pale kuna tatizo!!! Poleni Open University.
 
Ah, mbona wapo wengi tu makazini wanaheshimika mkuu. Wanapewa kazi za kupanga magari na wanamudu. Degree ya open university sawa na nyingine tu.
 
Ninachojua lecturers wa open university sometimes ndo hao hao wa Udsm, Mzumbe, udom etc. tatizo la open university ni kudekezwa tu na wahadhiri wao ili wasionekane kwamba hawafundishi na hawafaulishi, ukienda chuo kama Mzumbe ambapo nimesoma pale hawakubembelezi ukifeli umefeli na supplementally utafanya tu hutaki acha, ukidisco ndo bye bye...sisi mwaka wetu mtoto wa kigogo wa CCM alidisco Mzumbe pamoja na baba yake kufanya juhudi kubwa kumuokoa mwanaye wapiii!!! hata kaka yake ambaye leo ni waziri wa wizara ile ya M..u..u..n..g..a..n..o alifanya juhudi wapiiiiii......!! lakini ingekuwa open ....????
 
chuo chenyewe umeshasema ni OPEN so kila mtu anaeingia lazima amalize tena kwa GPA kuubwa lazima mtaendelea kudharaulika
 
Mtadharaulika tu maana chuo chenu hakina hadhi hebu fikiria namna walimu/wahadhiri wenu mainly kwa kujuana, pili PROMOTION CRETERIA zenu ni kichekesho Muhadhiri akiandika makala gazetini na kutoa pamphlet(s) kama Nyangwine huyoo tayari Professor, Master/PhD presentation zenu mnafanya kisiri siri kwa hiyo hata Public haijui/haishirikishwi, Wahadhiri wenu wavivu na hawaonekani kwenye Majarida ya kitaalauma ya kimataifa (International Peer-reviewed Academic Journals) unategemea nini. Nyinyi mmekaa kisiasa kuwapatia digrii watu fulani ambao hawauwezi muziki wa UDSM. Asante.

Pumbavu Sana.
 
Tatizo la Open University linaanza na inferiority complex waliyonayo wahitimu, wahadhili na wanafunzi. Ushauli wangu ni kwambba ondoeni kwanza inferiority complex mliyonayo, msiwe watu wa kujihami na kutojiamini, mkiweza hilo itawasaidia.
 
Hapo kwenye interview nyingi wanaangalia nini unajua kulingana na aina ya skills yanayihitaji toka kwa mlengwa, chuo ulichosoma sio kigezo kikubwa, kama huja waimpress nn unategemea?
 
Nlimaliza udom thoz yearz, nimemaliza program ingine open universty recently, mziki wa open usipime, Nlidhan open ni lelemamaa hakika sio, nlichokisomea hakijadharaulika na kimeniinua kiasi, mentality ya kudharau OUT ipo cha muhim ni kutambua malengo yako na kuyasimamia.
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................
You have satisified your "self". We KIPANGA tuambie kwa nini first degree usome OUT (kama ulisoma first degree OUT). Fanya tafiti ufahamu ni kwa nini 99% ya wahadhiri wenu wamesoma na bado wengine wanasoma UDSM, SUA, MZUMBE etc katika level za Masters na PhD!!!

Ukilifahamu hili hutaona shida ni kwa nini kuwe na tofauti katika hili. Muhimu tu ni kuwa elimu ya mtu huchangiwa kwa kiasi fulani, labda asilimia 50, na mazingira aliyosoma. Kinachobaki ni uwezo wa mtu kiakili. Wengi wa wanaosoma Open (usinitukane tu tafadhari) ni wale mabingwa wa kuunga unga elimu. Leo utasikia cheti, mara diploma, mara degree (hata Mbunge wangu wa Musoma Mjini aliyewahi kuangukia pua kwa Ndalichako) aliunga unga huko kwenu OUT na sasa ana degree teh teh teh.

Mfano wa mwisho ninaoukupa ni wa LAWYER anayejipambanua kubobea kwenye sheria Mh. Waziri wa Tamisemi Ndg. Simbachawene. Ukifuatilia arguments zake za kisheria na kuzilinganisha na watu kama Tundu Antipasi Lissu, Halima Mdee na wengine waliokamua msuli FoL utagundua kuwa kwa kiasi kikubwa degree yake ni ya kuandikiwa na washikaji.

Kuna usemi unasema GO EAST OR WEST, HOME IS THE BEST. Endelea kutetea kwako nasi tuendelee kutetea kwetu. Japo mwisho wa siku wote tunapaswa kutumia vi-marifa tuvipatavyo kwenye hivyo vyuo kulisaidia taifa. Ila mmmmmhhhhhhhhhh...OUT
 
Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania? Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!
nadhani hujasoma open university ila umeleta uzi kwa sababu binafsi kukashifu mojawapo ya vyuo bora nchini.
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi

Hii sio kweli hata kidogo kusoma mtu atakavyo haichangii kumfanya mtu kuwa incompetent
 
Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania? Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!

Mkuu nikupongeze kwa ujasiri wa kuleta huu uzi hapa na kuonyesha kuwa wewe ni mhitimu wa OUT,
Ukweli ukisemwa vizuri utakiponya chuo hicho, binafsi nili appy kusoma hapo MBA jioni, nikawa admitted kila kitu, sasa kihoja ni kuwa eti kwenye dissertation nitafute mwalimu yeyote mwenye Phd anisimamie popote, provided tu yupo chuo chochote kilichosajiliwa na TCU... the question comes how do you justify my perfomance? na vipi uhusiano wangu na huyo mwalimu utaathiri vip uwezo wangu wa kujitegemea had ninapo submit hiyo pepa.

Kingine, Open imekaa kama tuition centre... it doesnt look like a university or even a college, walimu wenyewe ni kama wamekata tamaa, vip wakikutana na wanafunzi wenye ushawishi wa fedha watakuwa fair kwa kias gani?


OUT has been there for more than 20 years now, wajirekebishe badala ya kusingizia watanzania kudharau elimu za masafa and bla bla.....zaid nawahurumia watu wenye sifa wanaopoteza muda wao hapo...look somewhere else.
Japo kwa MBA OUT inaweza kuwa bora kuliko mzumbe mara elfu kumi bila kupinga kuwa UDSM ndio mama wa kila kitu.
 
Open University ni chuo ambacho kikiachwa kiendelee hiv kitazalisha wataalamu wa kuiteketeza hii nchi. Tena la ajabu hata wenyewe wahitimu wanalijua hili. Fuatilia usanii unaofanyika kila mahafali yao lazima wamchomeke mtu maarufu anayehitimu ili kuvutia watu kujiunga na chuo chao. Watu makini (ikiwemo JPM, Mwigulu n.k.) wamejipambanua kwa vyuo walivyosoma, UDSM na si OUT. Inshort programu za OUT ni tia maji tia maji.
NB: Kuna mbegu ya UDINI (hasa programu za Social Science, KISWAHILI kuna wavaa vipedo mule wanajazana uji,nga na kupeana marks bila mpangilio) PACHUNGUZWE!!!
 
Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania? Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!
Mkuu usiwe na wasiwasi,ajila ziko nyingi sana mimi mwenyewe nimesoma bachelor open na nikawashinda wao unaowasema wa vyuo vingine,na kuna jamaa angu nimesoma nae na sasa ni anafundisha mzumbe university sheria.
 
Back
Top Bottom