Wagonjwa wa Kibiongo 50 hadi 60 wanapokelewa MOI kwa Mwaka

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Katika kuendelea kuhakikisha huduma za matibabu ya kibingwa zinapatikana Nchini, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeandaa program ya Upasuaji Mkubwa wa Kunyoosha Migongo iliyopinda ‘vibiongo’ (Scoliosis).

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amesema “Malengo ya Serikali ni kuhakikisha huduma kama hizo zinapatikana, hivyo taasisi kama MOI ndio jukumu lake kuhakikisha hilo linatimia.”
Kibiongo 1.JPG

Amebainisha kuwa katika taasisi ya MOI wanapokea wagonjwa nne hadi watano kwa mwezi na kwa Mwaka wanapokea wagonjwa 50 hadi 60.

Amebainisha kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, wamepokea wataalam ngazi ya Profesa kutoka Nchini Marekani na Italia ambao wanaoongoza majukumu hayo ya kufundisha madaktari na watakuwepo hadi Aprili 29, 2023.
Kibiongo 3.JPG

Katika kipindi hicho cha mafunzo maalum wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa watano hadi sita chini ya Wataalam wanaoongoza mafunzo hayo ni Massimo Balsano na Alaa Azmi Ahmad.

Amesema “Baada ya mafunzo hayo tunaamini wataalam wetu watakuwa na uwezo wa kuongoza upasuaji huo na kupeleka ufundi kwa wenzao.”
Kibiongo 2.JPG

Kibiongo34.JPG

Amesema kuwa ugonjwa huo una tiba na kushauri unapowatokea Watoto wazazi au walezi wanatakiwa kuwapeleka hospitali kwa kuwa wanapopata tiba mapema ni rahisi kuliko wanapokuwa watu wazima.

“Chini ya miaka 10 mtoto hafanyiwi upasuaji, kuanzia umri huo na kuendelea wanakuwa wanafanyiwa upasuaji.

“Zamani upasuaji kama huu ulikuwa unafanyika nje ya nchi na gharama zilikuwa kubwa na gharama yake ilikuwa inafika hati Tsh. Milioni 50, lakni kwa hapa ndani gharama yake ni hadi Tsh. Milioni 12,” anasema Dkt. Boniface.

CHANZO CHA UGONJWA
Upande wa Daktari Bingwa wa Mifupa MOI, Dkt. Bryson Mcharo amesema “Tunapozungumzia ugonjwa huo tunamaanisha mgongo ambao umepinda upande, lengo la upasuaji huo ni kujenga uwezo wa madaktari wa Taasisi ili kutoa huduma bora kwa wenye changamoto hiyo.

“Sababu za kibiongo kwa asilimia kubwa hazijulikani, japokuwa kuna nadharia nyingi zinazotajwa kuhusishwa na ugonjwa huo, mfano inadaiwa kuna kemikali zilizopo mwilini ambazo zinasababisha Watoto wakike kupata ugonjwa huo.

“Pia inadaiwa kuna dhana ya kurithisha, mfano familia ikiwa na Mtoto mwenye kibiongo kuna uwezekano wa kupata wingine mwenye changamoto hiyo.

“Kibiongo kinachotokea kwa mtoto ambaye ana umri wa chini ya miaka 10 kinaweza kuwa na sababu kadhaa zikiwemo;

“Kuzaliwa akiwa na mifumo ambayo haijakamilika, kuzaliwa akiwa na matatizo ya misuli na mishipa ya fahamu, pia kuna magonjwa ambayo yanaweza kufuatana na kibiongo kama mtindio wa ubongo, wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya kuvunjika vunjika.

“Kama mgonjwa hatapata matibabu vizuri anaweza kuwa na tatizo la kutopumua vizuri, kushindwa kula vizuri, kwa kuwa mgongo ukipinda unaathiri mapafu na kutopata hewa ya oksijeni ya kutosha.

“Ukiwa na kibongo pia hauonekani vizuri, mwonekano kutokuwa sawa.”

Ameongeza baada ya mafunzo hayo wataendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa wapya na wengine ambao walifika MOI awali lakini hawakupata matibabu.
 
Back
Top Bottom