Wadukuzi waingilia mifumo ya kompyuta duniani wadai fidia ya dola milioni 300 kwa fedha ya bitcoin

Naomba Mungu nchi yetu isiguswe maana sijui kama kuna mana tunaweza kujilinda na hili


Kugawanyika kwetu ndiko kunatufanya tuwe kwenye risk,
  • tulitakiwa kuwa kitu kimoja, tuachane na kutofautiana kiitikadi, kiimani nk
  • tufikirie kujenga uchumi imara
  • tuwekeze kwenye elimu zaidi ili kuwa na wataalamu mahiri
  • muda wetu wote tuifikirie Tanzania kabla ya kitu kingine chochote
  • tuwawezeshe wataalamu wetu wa ndani kuipigania nchi yetu kwa kutumia teknolojia
  • tupunguze uwekezezaji kwenye siasa na kuelekeza rasilimali zetu kwenye tafiti zaidi
  • tutumie hoja katika kutatua tofauti zetu badala ya vitisho, mipasho, kejeli na vijembe
  • etc
 
Kaspersky Lab, a Russian cybersecurity firm, said Russia was the worst-hit, followed by Ukraine, India and Taiwan. Reports of attacks also came from Latin America and Africa.
 
Hii vita ya udukuzi kimtandao ni kubwa na ngumu kuliko zote zilizowaho kutokea. Kuathiri nchi zaidi ya 100 kwa wakati mmoja sio jambo jepesi. Mbaya zaidi hata nchi zinazojulikana kwa hila za udukuzi kama Urusi hazijapona na Urusi ni moja ya nchi aliyoathirika zaidi. Hivyo ni vita ambayo muhusika hajulikani na wanachohangaika wataalamu kwa sasa ni kuokoa maisha kwanza na sio kumtafuta mchawi.

Mfumo wa wa computer wa idara ya Afya wa UK (NHS) ni moja ya mifumo imara na ya kisasa kabia lakini imeumia.

Tatizo hili limewapata kwa wingi zaidi watumiaji wa windows na hasa wale ambao ndani ya miezi miwili iliyopita hawajafanya windows updates. Uvamizi huu ulianza taratibu na kuna hospitals kubwa hasa US zililazimka kulipa millions kurudishiwa data zao..hivyo taadhari ilikuwepo ila hatua stahiki hazikuchukuliwa.

Naomba Mungu nchi yetu isiguswe maana sijui kama kuna mana tunaweza kujilinda na hili

Tatizo kubwa la taasisi nyingi duniani zinabana matumizi kupita kiasi na idara za IT zinajikuta ziko nyuma katika masuala ya ulinzi wa mitandao.

Utakuta kuna taasisi au makampuni mengi bado yanatumia Windows XP na hawajawahi kufanya "updates" wala usafi wa kompyuta hivyo kuwa katika hatari ya kushambuliwa.

Kwa mfano mapema mwaka huu Microsoft walitoa kiraka cha ulinzi yaani "security patch" ambacho unapaswa kukiingiza katika kompyuta yako ili kufanya sasishi (updates) lakini makampuni na taasisi nyingi hawajafanya hivyo.

Microsoft pia waliacha kutoa hivyo viraka za ulinzi miaka zaidi ya mitatu ilopita hivyo kuifanya XP kuwa hatarini.

Unatakiwa kuwa hatua moja mbele dhidi ya mashambulizi katika haya masuala ya teknolojia.
 
nani katengeneza hawa wa dudu

Mwezi April kundi linalojiita Shadow Brokers lilitoa kifungu cha kirusi cha Ransomware na kutahadharisha kwamba taasisi ya ulinzi ya Marekani NSA haikuwa salama baada ya kuidukua.

Inasemwa kwamba kundi hili limegawanyika duniani na wanashambulia kwa kutoa na kusambaza barua pepe zaidi ya milioni 5 kwa saa.

Jina halisi la kirusi ni WCry, lakini wataalam wanaamini kwamba kimejigawa kwa kutumia majina mbalimbali kama WannaCry, WanaCrypt0r, WannaCrypt, na Wana Decrypt0r.
 
Hawa mbwa kweli, nawakumbuka walivyoifanya computer yangu iliyokua na zaidi ya 300gb za mafaili ya kutengenezea simu.

Mimi waliniua na kirusi kinaitwa .CERBER3.. nakumbuka yale maumivu ya kuformat laptop yanu huku nikwazia kudownload file mpya
 
Hawa mbwa kweli, nawakumbuka walivyoifanya computer yangu iliyokua na zaidi ya 300gb za mafaili ya kutengenezea simu.

Mimi waliniua na kirusi kinaitwa .CERBER3.. nakumbuka yale maumivu ya kuformat laptop yanu huku nikwazia kudownload file mpya

Hakikisha unafanya backup kwa kuwa na External HDD ambapo unafanya copying ya HDD yako na mafaili yote.

Prevention is better than cure.
 
Haya mambo mengine yahitaji tuition!
Wanaojua:
madhara ya hao virusi kwa nchi ni yap? Kwa mfano,
 
Haya mambo mengine yahitaji tuition!
Wanaojua:
madhara ya hao virusi kwa nchi ni yap? Kwa mfano,

Madhara yake ni makubwa sana hasa kama una taasisi ambayo inahifadhi taarifa mbalimbali za watu na kumbukumbu.

Kama tunazungumzia taasisi kama vile NSSF, TRA, makampuni ya simu, na zingine kama DAWASCO, TANESCO na zingine za jinsi hiyo.

Ni kwamba kama hazichukui hatua za kujilinda basi taarifa zote zinakuwa mashakani kupotezwa.

Ni pale utakapohitajika kuanza upya kila kitu ndipo utakapotambua umuhimu wake.
 
Madhara yake ni makubwa sana hasa kama una taasisi ambayo inahifadhi taarifa mbalimbali za watu na kumbukumbu.

Kama tunazungumzia taasisi kama vile NSSF, TRA, makampuni ya simu, na zingine kama DAWASCO, TANESCO na zingine za jinsi hiyo.

Ni kwamba kama hazichukui hatua za kujilinda basi taarifa zote zinakuwa mashakani kupotezwa.

Ni pale utakapohitajika kuanza upya kila kitu ndipo utakapotambua umuhimu wake.
Thanx a lot!
Kwa hiyo hivyo virus wanatengeneza binadamu ili wajipatie pesa au vip? Bado naumwa ndugu!
 
Bitcoin ni njia ya kulipia malipo yao... ni kama vile Paypal..... Ukitumia Bitcoin naskia haikatwi kodi inaenda kama ilivyo... Kama nimekosea nipo tayari kusahihishwa

nintchdbpict000306226106.jpg


Bitcoin ni inatumika kwasababu ni vigumu kuifuatilia chanzo cha anaelipa na mwisho kwa anaechukua hiyo fedha.

Malipo yanafanyika bila kuwepo mtu wa kati na pia hakuna tozo na wala anaelipa hakitajiki kutoa jina lake.

Nilielezea kidogo humu katika moja ya michango yangu kuhusu namna mambo yanavyofanyika lakini kwa kifupi ni kwamba ni njia ya malipo isiyotumia majina halisi na haiwezi kuingiliwa na serikali kwani ipo katika ulimwengu wa kufikirika yaani "virtual world".

Kuna tovuti moja ilifungwa mwaka 2013 ambayo ilikuwa ikijulikana kama Silk Road ambayo ilikuwa ikiruhusu malipo hata yale ya wauzaji madawa ya kulevya na wahalifu wengine kama wale wanaonunua picha za ngono.

Hii tovuti ya Silk Road ni miongoni mwa tvuti nyingi ambazo huwa zinatumia njia inayoitwa Dark Web ambapo hizi tovuti zinakuwa zimefungwa kwa walimwengu wa nje na wala huwezi kutumia google kuzitafuta na kuzipata bali unatakiwa utumie njia iitwayo Tor ambayo inafanana na VPN yaani ile tunayoitambua rasmi.

Hizi tovuti za Dark web unaweza kuzitembelea lakini wamiliki wake hawajulikani.

Nikirudi kwenye suali lako la msingi ni kwamba ni njia isiyo rasmi lakini katika nchi nyingi duniani njia hii ya malipo imeanza kukubalika na kuna sehemu watu wananunua Pizza kwa kutumia Bitcoin.
 
Mhh sasa huku ulimwengu wa tatu si ndo tutaathirika zaidi?
Hamna mbabe kwenye hii vita.... Urus kachezewa rafu sembuse huku Africa...... Vita ya kimtandao ni ngumu sana ukijipanga na hiki wao wanakuja na njia nyingine
 
Back
Top Bottom