Kuna chembechembe ya damu
zinazokonekti kwa Wana wa Israeli na Kabila la Wachaga ambalo linapatikana Mkoa wa Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania. Yapo madai kwamba, Wachaga asili yao ni Wafalasha waliyokuwa na wanaoishi nchini Ethiopia.
Inadaiwa kuwa, Wachaga hao walitokana na uzao kati ya Malkia wa Sheba (Ethiopia) na Mfalme Sulemani. Inadaiwa kuna nyakati, Malkia alikwenda Yerusalemu kumtembelea Suleimani, wakakutana kimwili na kumzaa mtoto aliyeitwa Maneliki aliyekuja kuwa mfalme wa pili Ethiopia baada ya kifo cha mama yake (aliitwa Mfalme Meneliki II) mwaka 1889.
Kizazi cha Meneliki kingine kiliendelea kuishi Ethiopia kingine KILISHUKA na kuingia Kaskazini mwa Tanzania, Kilimanjaro na kuishi hapo kwa desturi walizoingia nazo huku wakijulikana kwa jina la Wachaggy, maana yake WALIYOSHUKA.
Sasa inaelezwa kwamba, hata mila na desturi za Wachaga zinafanana kwa kiasi kikubwa na Wafalasha ambao wana damu ya Waisraeli kwa sababu, ni kizazi cha Mfalme Suleimani. Yaani kuna utamaduni au desturi za Kichaga zinafungamana na desturi au mila za Kiisraeli kama ifuatavyo:
1. UTARATIBU WA KUOA MDOGO MTU KABLA YA DADA YAKE
Inaelezwa kuwa, mwanaume yeyote awe Mchaga au asiwe, akitaka kuoa binti wa Kichaga wakati binti huyo ana dada yake wa kuzaliwa na hajaolewa, hufanyika utaratibu wa kimila ili kupatikane ruhusa ya binti huyo kuolewa kabla ya dada mtu. Kwa vile haitakiwi na wala si mila kwa binti wa Kichaga kuolewa kabla ya dada yake.
Kwa mujibu wa mzee Nathaniel Tarimo ambaye ni Mchaga, yeye alisema huwa hivi:
"Mwanaume akishaleta posa Uchagani huwa tunaangalia, je! Binti aliyeletewa posa hana mkubwa wake?Kama yupo, tunaangalia je, ameolewa au bado? Kama hajaolewa, basi tunamwelekeza kijana na
binti kufanya mambo fulani ili kukamilisha mila na desturi ili binti aweze kuolewa kabla ya dada yake."
Ukiingia kwenye Biblia kwa wana Israeli utakutana na hili; MWANZO 29:23-26…
"Ikawa kulipokucha asubuhi, kumbe ni Lea. Yakobo akamwambia Labani (baba mkwe wake) nini hii uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa…”
Makabila mengi nchini Tanzania hayana utamaduni huo, kila mtu na bahati yake. Akianza mdogo sawa, akianza mkubwa poa tu ilimradi 'wenyewe wamependana.'
2. UTAMADUNI WA KURUDI UCHAGANI KILA MWAKA (KUHESABIWA)
Imezoeleka kuona Wachaga wakitengeneza misafara kila Desemba ya kila mwaka kwenda uchagani kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na hata Mwaka Mpya.Wenyewe husema wanakwenda kuhesabiwa.
Na wapo Wachaga huko kwao, Moshi wanapaita Yerusalemu ya Afrika.
Ni kipindi ambacho hata usafari wa kutoka Dar kwenda Moshi (hata Arusha) huwa wa shida. Ni adha kubwa. Licha ya kuwepo kwa mabasi mengi na serikali kuongeza usafiri wa treni mwaka, 2019 lakini bado
shida ipo.
Wachaga kurudi kwao kila mwaka ni tabia iliyojengwa au kujengeka na desturi za tangu asili.Japokuwa siyo wote, lakini karibu asilimia 57 ya Wachaga hurudi Kilimanjaro kila Desemba ya kila mwaka kufuata mila zao. Na kwa kawaida, Mchaga asiyekwenda mwaka huu, atakwenda mwakani.
Wapo Wanaokwenda kila mwaka. Pia wapo ambao hawajawahi kwenda hata mwaka mmoja.Mara nyingi wasiowahi kwenda tangu walipotoka Uchagani ni wale ambao 'hawajatoboa' kimaisha.
Ukiingia ndani ya Biblia utakutana na hii; LUKA2:1…
”Siku zile, Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa. Hivyo,Yusufu alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria…”
Hapa pia tunaona desturi nyingine ya Wachaga inayofanana na Wana
wa Israeli. Na utaratibu huu ulikuwa wa kila mwaka bila kukosa wala kusahau kama wanavyofanya Wachaga miaka hii.
3. MOYO WA KUPENDA MUZIKI WA REGE
Muziki wa Rege hupendwa zaidi na jamii ya watu wenye imani ya kirastafari, yaani Rastafariani. Hata marehemu Bob Marley, Lucky Dube na wengine wengi walio hai ambao wanaimba muziki wa Rege
ni marastafari.
Utambulisho wao wa nje ni kusokota nywele, rasta. Utambulisho wao wa ndani ni kutokula nyama zaidi ya mbogamboga.
Sasa kama historia inavyoeleza kuwa, katika nchi ya Ethiopia miaka ya nyuma kuna mfalme aliyeitwa Maneliki II (yule mtoto wa Malkia wa Sheba aliyedaiwa kuzaa na Mfalme Sulemani).Baada ya kifo cha huyu Maneliki II, ufalme uliendelea kurithishana kiukoo hadi kufika kwa Mfalme Haile Selassie.
Haile Selassie kabla ya kuwa mfalme aliitwa Ras Tafari Makonnen. Jina la Haile Selasse ni la kifalme likiwa na maana ya
Utukufu wa Utatu (Mtakatifu). Pia anafahamika kwa jina la Simba wa
Yuda au Mfalme wa Wafalme. Alikuwa Mkristo wa Madhehebu ya Kanisa la Orthodoksi nchini Ethiopia.
Haile Selasse alipoanza utawala, habari zake zikaenea kote duniani kutokana na misimamo yake na ikasababisha kutokea kwa dini mpya ya Rastafari iliyopokea jina kutoka kwake, ingawa mwenyewe alibaki kuwa muumini wa Kanisa la Orthodoksi, akiwa na daraja la ushemasi.
Watu weusi kisiwani Jamaika, waliyokuwa wajukuu wa watumwa wenye asili ya Afrika, waliposikia kwa mara ya kwanza kwamba kuna Mwafrika anaitwa Haile Selasse na kwamba anaheshimiwa na hata wafalme wa Ulaya, wakaamini yeye Haile Selasse ni mwokozi wa Mungu aliyerudi duniani kwa ajili ya watu weusi. Ndipo wakaanza kumwamini.
Sasa kitendo cha Wachaga wengi kupenda muziki wa Rege ambao unatokana na jamii ya Rastafariani ambao wanaamini katika Haile Selassie aliye pia kizazi cha Meneliki, mtoto wa mfalme Sulemani ni jambo lingine ambalo linaifanya jamii hii kufanana na desturi za Rastafari ambao wanaamini katika Israeli.
Zamani za hivi karibuni sikuamini nilipokuwa nikisikia kuwa, harusi za Wachaga au sherehe zao nyingi haziwezi kumalizika bila kupigwa muziki wa Rege.
Novemba mwaka 2019, nilibahatika kuhudhuria Send Off ya binti mmoja wa Kimarangu kutoka kenye koo ya Makundi, Ukumbi wa PoliceMass, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa nyimbo zilizopigwa katika sherehe hiyo ni muziki wa Rege uliopigwa na hayati Bob Marley, wimbo uitwao One Love.
Nilishangaa sana kuwaona Wachaga, vijana kwa wazee wakisimama na kuingia kati kucheza, wakiwemo wale ambao tangu sherehe hiyo iinaanza hawakutoka kwenye viti kwenda kucheza hata zilipopigwa nyimbo za dini.
4. MAJINA, MANENO YA KICHAGA YANAYOFANANA NA YA WAISRAELI
Kama nilivyosema kwamba, Wachaga wana
desturi nyingi znazofanana na Wana wa Israeli. Hapa nitaonesha maneno yenye
maana zinazofanana.
*Yave (hili ni neno la Kichaga lenye maana jina la Mungu). Kiisraeli
pia, Mungu wao wanamwita Yahwe.
*Lakini pia, Kiisraeli kuna neno linatamkwa Eli. Eli maana yake ni Mungu. Kichaga pia, Eli maana yake ni Mungu. Kwa kuthibitisha kufanana kwao lugha, ndiyo maana majina mengi ya Kichaga yana Eli mwisho wa jina au mwanzoni mwa jina. Haya majina yenye Eli, Wachaga wenyewe wanasema kuwa, walianza kuyatumia hata kabla ya Ukristo haujaingia Kilimanjaro. Kwa hiyo hawakuyatoa ndani ya Biblia bali ni asili yao.
5. MAJINA YA KICHAGA YENYE ELI MWISHO;
Sifaeli, Aikaeli, Wangaeli, Shafuraeli, Apaeli, Aikaeli, Rumishaeli, Pendaeli, Anaeli n.k.
6. MAJINA YA KICHAGA YENYE ELI MWANZONI;
Elinganya, Eliufoo, Elisaria, Elibariki, Elinaja, Eliakimu, Elisante, Eliatosha, Elinawinga, n.k.
7. MAJINA YA KIISRAELI YENYE ELI MWISHO;
Israeli, Panueli, Mishaeli, Magodieli, Gamalieli, Malikieli, Nethanaeli,
Shelumieli, Surieli, Uzieli, Laeli, Yaleeli, Deueli, Pagieli, Reueli, Amieli,n.k.
8. MAJINA YA KIISRAELI YENYE ELI MWANZO;
Eliasafu, Elia, Elimeleki, Elisha, Elisuri, Elishama, Eliabu, Eliudi, Elisafani n.k.
9. UKOO WA MUSHI UPO NDANI YA BIBLIA
Nilipoliona jina la Mushi kwenye Biblia, nilirudia mara mbilimbili kusoma
nikiwa siamini. Watanzania wengi tunajua Mushi ni jina la ukoo Uchagani, tena ni ukoo unaotokea Machame.
Soma Mwanzo 6:18-19...
"Na wana wa Kohathini Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli, na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia na thelathini na mitatu. Na wana wa Merarini Mali na Mushi..."
10. UTAMADUNI WA KWENDA KUZIKA MAKWAO;
Bado naendelea kuonesha jinsi desturi au tamaduni nyingi za Wachaga zinavyofanana na Wana wa Israeli.Hapa naelezea kwa nini
Wachaga wanaelemewa na moyo wa kwenda kuzika mili ya
marehemu wao Uchagani.
Mzee Kimei, yeye ni mkazi wa Bonyokwa, Dar es Salaam, anasema:
"Sisi Wachaga kubeba maiti za ndugu zetu kwenda kuzika Uchagani siyo ombi, ni lazima.Japokuwa wapo marehemu wanaozikwa ugenini, lakini hata familia yake haiwi na amani.
Ndiyo maana mfano, Mchaga akifia hapa Dar halafu pesa za kusafirisha mwili wa marehemu zinasumbua kupatikana, mwili
unaweza kukaa mochwari hata siku kumi na tano.Mpaka pesa ipatikane."
Waisraeli, soma Mwanzo49:29-...
"Akawaamuru, akasema mimi nakwenda kukusanywa (kufa) pamoja na watu wangu, mnizike pamoja na baba zangu katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti. Katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya
Kanani..."
Yakobo ambaye ndiye Israeli, anamwagiza mwanaye Yusufu kwamba akifa mwili wake usafirishwe kutoka nchi ya Misri walikokuwa
wakiishi na kwenda kuzikwa nchi yao ya ahadi, Kanani.
Mwisho