Hatimaye sasa rasmi taswira ya CHADEMA mpya chini ya Lowasa inavaa gamba kwa kasi baada ya kucheza ngoma wasioijuwa. Kama inavyojulikana Mh.Charles Kitwanga tokea ateuliwe kuwa Waziri wa mambo ya ndani tumeshuhudia wauza unga wakubwa kwa wadogo wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hili limekuwa pigo lililodhihiri kuwaumiza wazungu wa unga wakiwamo waliofadhili harakati za UKAWA ili kumuwezesha mamvi kuikalia ikulu.
Hii ni kutokana na umbumbu na hasa kumuhusisha Mh.Kitwanga ambaye hakuwahi kuhudumu wizara ya mambo ya ndani kipindi mkataba baina ya Lugumi na jeshi la polisi ukisainiwa na kutekelezwa.Ieleweke tu madudu ya mkataba huo yamegunduliwa na CAG na ripoti imekabidhiwa kamati ya mambo ya nje na usalama ili ijadiliwe kama sheria na kanuni za bunge zinavyotaka.
Ushauri:CHADEMA kabla ya kufanya kazi za genge la 4UM lililochini "raisi ya mioyo yenu"..mjiridhishe kwanza na sio kutumika kulenga kivuli badala ya ndege.
NB:Naunga mkono wote wanaotaka kujua ukweli wa Lugumi kwa maslahi ya taifa.
Nawasilisha.
Itakua ni tatizo kifaa chako unachotumia mbona kwangu imefungujaHiyo attachment haifunguki
Kwahiyo mnataka mtuaminishe kuwa Kuna watu hawakosei au kufanya mipango ya wizi? Tena kwenye awamu hii ya tano. Kama amehusika na ufisadi awajibishwe tu. Sheria ni msumeno. Eti kisa anapambana na wauza madawa, basi aonekane lulu akikosea asiwajibishwe. Piga chini wote wezi.Wabunge wa upinzani na kumuhujumu magufuli linawezekana hili
Hatimaye sasa rasmi taswira ya chadema mpya chini ya Luwasa inavaa gamba kwa kasi baada ya kucheza ngoma wasioijuwa.Kama inavyojulikana Mh.Charles Kitwanga tokea ateuliwe kuwa Waziri wa mambo ya ndani tumeshuhudia wauza unga wakubwa kwa wadogo wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hili limekuwa pigo lililodhihiri kuwaumiza wazungu wa unga wakiwamo waliofadhili harakati za ukawa ili kumuwezesha mamvi kuikalia ikulu.
Hii ni kutokana na umbumbu na hasa kumuhusisha Mh.Kitwanga ambaye hakuwahi kuhudumu wizara ya mambo ya ndani kipindi mkataba baina ya Lugumi na jeshi la polisi ukisainiwa na kutekelezwa.Ieleweke tu madudu ya mkataba huo yamegunduliwa na CAG na ripoti imekabidhiwa kamati ya mambo ya nje na usalama ili ijadiliwe kama sheria na kanuni za bunge zinavyotaka.
Ushauri:Chadema kabla ya kufanya kazi za genge la 4UM lililochini "raisi ya mioyo yenu"..mjiridhishe kwanza na sio kutumika kulenga kivuli badala ya ndege.
NB:Naunga mkono wote wanaotaka kujua ukweli wa Lugumi kwa maslahi ya taifa.
Nawasilisha.
Mara Lugumi,mara Infosys...hamna msimamo...hadi majambazi yamejaa humu JF!Acheni porojo. Kitwanga atuambie juu ya uhusika wa Infosys kwenye ufisadi wa pesa za umma sio blaablaa za nani mchawi aliye mchongea kwa umma.