Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,172
- 5,531
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mjadala wa Muswada wa Ulinzi wa Taarifa binafsi wametoa hoja zao huku wengi wao wakionekana kuunga mkono kuundwa kwa sheria hiyo.
Aidha katika kuongeza nguvu hoja Wabunge wengi wanaonesha kwamba ni muhimu katika uundaji wa sheria hiyo liongezwe neno falagha ili kufanya sheria hiyo izidi kuwa na tija kama itapitishwa.
Wakitoa maoni yao Mbunge Ally Mlagila Jumbe anaeleza kuwa "kwenye jina la taarifa hii kuna kitu kinapungua, tunaposema tu ulinzi wa taarifa haitoshi, inabidi iwe ulinzi wa taarifa na faragha, nchi nyingine wameshafanya hivyo sisi tunasita nini?
"Kwa kuwa mtu anaweza simama tu hadharani akakuuliza jina, unaishi wapi badala ya kukuuliza kwa faragha, inabidi tunapotoa taarifa kuwe faragha na kama neno hili kwa kiswahili ni zito basi tutafute neno lingine lenye maana hii."
"Lakini pia mtu akifariki inabidi taarifa zilindwe sio kubaki zikizagaa inabidi tuone jinsi ya kulinda taarifa za marehemu."
kwa upande wao, Stella Fiyao Mbunge viti maalumu CHADEMA na Mwanaisha Ulenge Mbunge viti maalumu CCM nao wameshauri kuwa kwenye muswada huu ni muhimu likaongezwa neno falagha ili kuipa uzito sheria husika.
Naye, Mbunge Ahmed Abdulwakil amesema kuwa Sheria hiyo ni muhimu na endapo itapitishwa na Bunge italinda utu, heshima na faragha ya wananchi.
Kutokana na Tanzania kutokuwa na sheria hii watu wengi wamekuwa wahanga wa taarifa zao binafsi kutumiwa kiholela, mfano kwa baadhi ya Wabunge ambao taarifa za mazungumzo yao binafsi zilitolewa hadharani bila ridhaa yao.
Muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utakomesha matumizi mabaya ya taarifa binfasi na watu watakuwa na amani linapokuja swala la taarifa zao na faragha zao kuwa salama.