Ni kweli website ya bunge ina mapungufu mengi sana.
1 .Hansard nyingi zinachelewa kuwekwa kwenye website ya bunge hivyo tunashindwa kuzi access bunge lililopita hansard za kila siku bungeni zilikuwa zinapatikana siku hiyo hiyo.
2. Order papers za bunge zinawekwa baada ya bunge kukaa vikao hivyo inakuwa ngumu kujua bunge leo linajadili nini, bunge lililopita order paper za bunge zilikuwa zinapatikana kwa urahisi zaidi.
3. Parliamentary proceedings websites mpaka wiki iliyopita ilikuwa inaonyesha orodha ya shughuli za bunge la kumi.
4. Kuna wakati mwingine websites haifanyi kazi vizuri hivyo tunashindwa kuaccess documents ambazo ni accessible na public.
5. Documents za wapinzani hazionekani mfano hotuba zote za kamati za kambi za upinzani na hotuba ya kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani hazipatikani toka bunge la kumi na moja linaanza.
6 .Ministerial statements nyingi ni za bunge la kumi wakati ministers wameshatoa matamko mengi tu bungeni kwenye bunge hili la kumi. Ministerial statement iliyopo ni ya Nape kuzuia bunge kuonyeshwa live, je zingine siyo muhimu.
Kwa mara ya mwisho nimevisit bunge leo tu.
Maoni
Bunge lianzishe utaratibu wa newsletter watu tuweze kupata taarifa za shughuli za bunge kwa urahisi zaidi bila kusubiria kuingia website au edited TV programs.