Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,787
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.
=====
Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.
Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.
Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.
Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.
Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.
Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.
Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.
Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.
Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.
Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.
Pia, Soma;
=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum
=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi
=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!