Wabeba lawama tukutane hapa!

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,537
31,692
Wakuu bila shaka ni wazima, bila shaka wote tunaelewa maisha yalivyojaa changamoto za kila aina.
Kuna watu ni wepesi kueleza yale yanayowasibu, ila kuna akina sisi ambao huwa tunakufa na tai shingoni!

Kifupi kwa upande wangu sina maisha hayo ambayo ndugu na jamaa wanayafikiria, lakini lawama zimekuwa haziishi kwamba sina msaada wowote kwao ihali mwanzo nilikuwa nawapiga tafu pale inapowezekana.

Hapa karibuni kuna hali imenishtua unakuta mtu mzima tena mwanaume, mkizoena kidogo tu anataka umpe hela, mi huwa najiuliza mbona mimi huwa napambana na ya kwangu mwenyewe, hawa wanaahindwa vipi, na sio kwamba mtu anataka kukopa hapana anataka apewe bure bure tu.

Ukimwambia pengine na wewe una hali mbaya basi urafiki unaishia hapo, ananuna na hautamuona tena. Vipi nyie mnakabiliana vipi na hawa watoa lawama, maana kuna muda huwa nakuta wananivuruga kabisa, tena kipindi hicho unakuta na mimi mambo yangu mengi hayaendi kabisa.
 
Ishi ulaumiwe, kufa usifiwe.
images (23).jpeg
 
Play in your limits mkuu fanya unalo ona ni sahihi , fanya kinachokupa furaha wewe sio wengine, wakishindwa kuendana na itikadi zako isiwabembeleze waache waende, ulikuja duniani mwenyewe utaondoka duniani mwenyewe
 
Kuna jamaa alinitumia mkeka mrefu una bajeti ya mtaji anaohitaji ili afungue biashara yake kwahiyo anaomba nimpe hela (sio kukopa eti nimpe tu kumsapoti) aisee nilistaajabu sana. Nilimpotezea akanichunia naona juzi tena katuma sms ndefu ya lawama na maombi juu
 
Wakuu bila shaka ni wazima, bila shaka wote tunaelewa maisha yalivyojaa changamoto za kila aina.
Kuna watu ni wepesi kueleza yale yanayowasibu, ila kuna akina sisi ambao huwa tunakufa na tai shingoni!

Kifupi kwa upande wangu sina maisha hayo ambayo ndugu na jamaa wanayafikiria, lakini lawama zimekuwa haziishi kwamba sina msaada wowote kwao ihali mwanzo nilikuwa nawapiga tafu pale inapowezekana.

Hapa karibuni kuna hali imenishtua unakuta mtu mzima tena mwanaume, mkizoena kidogo tu anataka umpe hela, mi huwa najiuliza mbona mimi huwa napambana na ya kwangu mwenyewe, hawa wanaahindwa vipi, na sio kwamba mtu anataka kukopa hapana anataka apewe bure bure tu.

Ukimwambia pengine na wewe una hali mbaya basi urafiki unaishia hapo, ananuna na hautamuona tena. Vipi nyie mnakabiliana vipi na hawa watoa lawama, maana kuna muda huwa nakuta wananivuruga kabisa, tena kipindi hicho unakuta na mimi mambo yangu mengi hayaendi kabisa.
Mambo nishapitiaga mkuu.

Sasa hivi nikikwambia Hali yangu haiko poa kiuchumi alafu ukaninunia basi utakaa pembeni tu.

Nishasema Kwa sasa napokea lawama zote sababu hazinikatishi mikono Wala miguu.

Mkuu skia nikwambie kitu ukipendwa sana wee tambua unatengeneza mazingira ya kuzikwa na watu wengi tu pale utakapokufa lakini sio kwenye kusaidiwa kiuchumi.

Nishajitoa Sana Kwa Wana misaada ya kipesa misaada ya kikazi Sasa hivi sipo vizuri basi wote wananikataa kinoma noma.

Kati ya Hao Wana mmoja tu ndio tunaongea lakini wote kummke wapo busy Na mambo yao.

Kuwasaidia kifedha na kwenda Kula pombe Na pesa yangu walikuwa mstari wa mbele kinoma lakini Sasa hivi ni noma.

Wana wamebaki wananiongelea mabaya Sina kitu nimefulia nimepauka Sina Maisha tena huku wakisahau nilivyowatoa Enzi hizo na wamesahau kwamba bado nipo hapa duniani kwenye kumega hii cake.

USIOGOPE LAWAMA MKUU
LAWAMA HAPEWI MBUZI ANAPEWA MWANADAMU.
 
Shida kuna watu wanaamimi mtu unazo muda wote, na usipowapa ni roho mbaya na umewanyima tu, kitu ambacho sio kweli!
Usiwatilie maanani, huwezi saidia kila mtu kila wakati. Na hata ungeweza kufanya hivyo, bado lawama huwezi kuziepuka. Binadamu huwezi kuturidhisha mkuu.
 
Tunaishi Mara 1 Mzee wangu ISHI ili UFE unaweza ukafa KESHO hao HAO unawanyima TAG ndio watakaokuchimbia Kaburi hao HAO unawanyima ndio watakaoanza kuzunguka kutafuta Pesa za michango kwa ajili ya Sanda na Jeneza lako wakati HUO Wewe umelala usingizi mzito wa KIFO, that's all

GNya'al
 
Yeye hata kama asipozikwa ataweza kuwalalamikia kuwa hawajamfanyia fare?

Laiti mfu angekuwa anaweza kulalamika basi hili unalosema tungeweza kulizingatia.
 
Tunaishi Mara 1 Mzee wangu ISHI ili UFE unaweza ukafa KESHO hao HAO unawanyima TAG ndio watakaokuchimbia Kaburi hao HAO unawanyima ndio watakaoanza kuzunguka kutafuta Pesa za michango kwa ajili ya Sanda na Jeneza lako wakati HUO Wewe umelala usingizi mzito wa KIFO, that's all

GNya'al
Na wao watachimbiwa kaburi na nani, mbona hela zao hawagawi?
 
Back
Top Bottom