Vyeti feki: Daktari Mkuu Morogoro akumbwa, ni msomi toka Urusi aliyekaribia kustaafu

Nilicheka sana nilipomsikia Tundu Lissu anakomelea msumari kwenye uhakiki wa vyeti vya wakuu wa wilaya na mikoa (wanasiasa). Tundu amesema hao ndiyo ni wanasiasa sawa kwa vile wanatambuliwa kwenye katiba ya CCM, lakini katiba ya JMT inawatambua kama watumishi wa umma. Hivyo utetezi wa kwamba hao wantakiwa kujua kusoma na kuandika tu ni utetezi wa kijinga na aliyeutoa ni mjinga!!
 
Wengi wao pia walipata kazi kwa ile ya kujuana au kuchomekwa, na hata kuhonga.
 
Hakuna aliyeonewa bro katika hili
Trust me
Kuna mtu nilisoma nae o level nikakuta jina lake ikabidi nimuuulize akanambia ukweli aliuza cheti kwa mtu na yy hakwenda kuhakik kipindi kile na alikua na div2
So ina usiri mwingi sana ndani yake
Lazima kuna kitu fulan ndani yake na anayejua huo ukweli ni muhusika ,thank god serikali imetoa 2 chance ndio anafuatilia sasa hivi akaseme ukweli
 
Halafu mwanawani wale ndugu zetu wa kule juu...hili fagio limeondoka nawo wengi sijui kwanini...wale wanafiki wao naona mioyo yao kwatu sasa...mliotumbuliwa muombeni mkuu wa kaya angalau awape ata "kifao" kidogo cha kwenda kuanzisha mradi wa kuku...hamna jinsi sasa...
Waswahili wanasema mchuma janga ula na wa kwao.
 
Duuh kazi ipo sasa yawezekana kuna uonevu mkubwa la sivyo nchi imeoza

Hili zoezi madudu matupu mwanzo mwisho. Watanzania wengi watakuwa wameonewa katika zoezi hili. Hata kuhakiki vyeti tu Serikali imeshindwa! Sijui ni mabilioni mangapi yameyeyuka kwenye hili zoezi na walichukua toka fungu lipi.

Hapa kuna ukiritimba fulani wa serikaliumefanyika watu kibao wameaibishwa kwamba wana vyeti feki wakati tatizoni mfumo tu umekaa haueleweki.

Mtu kaolewa, kabadili jina, hajafuata sijui mchakato gani, serikali badala ya kujiridhisha imemlundika kwenye wenye vyeti feki.

By the time ana clear jina lake kashaanikwamitandao yote.

Siiamini serikali hii ambayo inateua watu bila kuwafanyia uhakiki wala mahojiano kwamba inaweza kupitia watu karibu 10,000 kwa umakini unaotakiwa.

kuna gazeti nilisoma kuna mwingine wa kigoma analalamika ametajwa kuwa ana cheti feki cha form4 wakati yeye hakupeleka vyeti vya form4 kwasababu hakusoma secondary kabisa aliishia darasa la saba la enzi za mwalimu akaenda kusomea ualimu maana ilikuwa inaruhusiwa enzi hizo

hili zoezi ni madudu matupu hii ndio inaitwa funika kombe.....
 
Kuna Doctor hapa morogoro alikuwa analalamikiwa sana kuwa amefoji veti tena alikuwa namcheo, ila pamoja na kulipotiwa/kelele zote lakini hakuna kilichofanyika, sasa nazani atakuwa ni yeye.
 
kuna gazeti nilisoma kuna mwingine wa kigoma analalamika ametajwa kuwa ana cheti feki cha form4 wakati yeye hakupeleka vyeti vya form4 kwasababu hakusoma secondary kabisa aliishia darasa la saba la enzi za mwalimu akaenda kusomea ualimu maana ilikuwa inaruhusiwa enzi hizo

hili zoezi ni madudu matupu hii ndio inaitwa funika kombe.....
Basi hapa walikua wanakisia tu.

Hili zoezi madudu matupu.

Ila hawa waliobakiza muda kidogo kustaafu, wawaache tu coz walipiga kazi safi japo kuwa na vyeti feki
 
Hili zoezi madudu matupu mwanzo mwisho. Watanzania wengi watakuwa wameonewa katika zoezi hili. Hata kuhakiki vyeti tu Serikali imeshindwa! Sijui ni mabilioni mangapi yameyeyuka kwenye hili zoezi na walichukua toka fungu lipi.
Hili swali hawawezi kujibu

Pesa ilitoka fungu lipi?

Kimsingi, hii serikali imekua ikifanya mambo mengi ya kutumia pesa nyingi ambazo hazijahidhinishwa na bunge.

Sijui tunaenda wapi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu na wenyewe wanajua ni madudu sasa wanaruhusiwa eti kukata rufaa! Hao wanaoshughulikia hizo rufaa ni akina nani wamechaguliwa na nani? Je, wako huru kufanya kazi yao bila woga? Je, wako tayari kuhojiwa na vyombo vya habari? Na hao waliokamilisha hili zoezi walikuwa hawana vingunge wao? Kama kulikuwa na hao viongozi wa hili zoezi ni wakati muafaka kwa wao kujitokeza hadharani ili wawekwe kwenye kiti moto kuhusu zoezi hili lote na madudu yake. Wasiendelee kufichwa hawa na wanafichwa kwa maslahi ya nani!?

kuna gazeti nilisoma kuna mwingine wa kigoma analalamika ametajwa kuwa ana cheti feki cha form4 wakati yeye hakupeleka vyeti vya form4 kwasababu hakusoma secondary kabisa aliishia darasa la saba la enzi za mwalimu akaenda kusomea ualimu maana ilikuwa inaruhusiwa enzi hizo

hili zoezi ni madudu matupu hii ndio inaitwa funika kombe.....
 
Hivi Serikali itaweza kuwalipa hawa watu ikithibitika hawana tatizo...
 
kuna gazeti nilisoma kuna mwingine wa kigoma analalamika ametajwa kuwa ana cheti feki cha form4 wakati yeye hakupeleka vyeti vya form4 kwasababu hakusoma secondary kabisa aliishia darasa la saba la enzi za mwalimu akaenda kusomea ualimu maana ilikuwa inaruhusiwa enzi hizo

hili zoezi ni madudu matupu hii ndio inaitwa funika kombe.....
Sio Kigoma,ni Dodoma
 
View attachment 504671

Mara ya kwanza kumfahamu ni miaka kadhaa iliyopita,ambapo ndugu na jamaa yangu wa karibu alipata ajali eneo la Doma Morogoro na kwenda kufia katika hospital ya mkoa wa Morogoro.

Wakati huo,bila ya shaka na kwa uhakika wa karibu,Daktari Mkuu wa Hospital ya Mkoa alikuwa Mahizo.Alituhudumia kwa upole na ukarimu.Mjuzi na mweledi katika fani yake,akitoa ushauri wa kitaalam na hatimaye kutupatia rufaa kwa baadhi ya majeruhi kufika Muhimbili.

Baadae akawa jamaa na rafiki wa hapa na pale sbb ya msaada na majitoleo yake kwa siku ile.Ndipo nilipofahamu kupitia yeye na marafiki zake kuwa amesoma Urusi.Ni daktari mbobezi na mweledi katika fani yake.Huyu alipasua na kutahiri,alipima na kuandika dawa.Ni dokta kwelikweli aliyevuka mipaka mpaka Ulaya ya Mashariki kuitafuta elimu.Msomi wa Urusi,ile Urusi ya Kisoviet ya Mwalimu Nyerere

Sasa naliona jina lake no4972 katika mtiririko wa majina matatu kama mmoja ya wenye "vyeti feki".Najiuliza kwa kunong'ona,huyu aliwezaje kufika chuo?Ilikuwaje mpaka alivuka mipaka,akasoma na kufaulu kwa "cheti feki?"Ilikuwaje akapata madaraka makubwa kwa ngazi ya kada yake bila kujulikana?Iweje akawa "bingwa"?akapasua na kutahiri bila "cheti orijino?"

Mwaka huu alikuwa astaafu na aendelee na mambo yake,fagio la JPM limemkumba.Najiuliza iliwezekanaje mpaka kufikia huko juu bila kugundulika?Hili la vyeti limetushangaza wengi,lkn limetufunza pia...
 
kuna gazeti nilisoma kuna mwingine wa kigoma analalamika ametajwa kuwa ana cheti feki cha form4 wakati yeye hakupeleka vyeti vya form4 kwasababu hakusoma secondary kabisa aliishia darasa la saba la enzi za mwalimu akaenda kusomea ualimu maana ilikuwa inaruhusiwa enzi hizo

hili zoezi ni madudu matupu hii ndio inaitwa funika kombe.....

Na wewe unaamini moja kwa moja hicho alichokiongea huyo mwana Kigoma....??
 
Hili swali hawawezi kujibu

Pesa ilitoka fungu lipi?

Kimsingi, hii serikali imekua ikifanya mambo mengi ya kutumia pesa nyingi ambazo hazijahidhinishwa na bunge.

Sijui tunaenda wapi

Hizo zilizokuwa zikiidhinishwa na bunge kwa muda wote zimetufikisha wapi.....!!??
 
Back
Top Bottom