Vodacom mmesababisha ndugu yangu kufariki, nawaletea maiti ofisini

Hilo tatizo si kwa Voda tu...hata tiGo pia wako hivyo.....ilinitokea kama ilivyo mtokea ndugu yangu huyo....nilipo waeleza wakanitaka nivumilie mpaka masaa sabini na mbili ili hali pesa ilikuwa ikihitajika siku hiyo kwa minajiri ya marejesho ya mkopo....hakuna siku niliyo ichukia mitandao ya cm kama siku hiyo....pesa ni yako tatizo ni lao alafu wakutake ukae masaa 72 ili hali we mambo yako yame simama na wao wakizarisha faida kwa pesa yako....hovyo sana aise...
 
Naandika haya kwa uchungu dhidi ya huu mtandao wa vodacom.Tarehe 25/4 saa 7 na robo mchana nilipigiwa simu dada kazidiwa tena kutoka kwa majirani, niliwaomba watafute gari wamkimbize hospital mimi niombe ruhusu kibaruani nitawakuta huko.

Kwenye akaunti yangu ya mpesa nilikuwa nina 416,000 tena niliiweka mda mfupi tu baada ya kupewa haki yangu ya mwezi na boss hivyo ikanipasa nimrushie 400,000dada kwenye no yake ili walipie usafili na matibabu,nilipotuma ile hela vodacom wakanitumia ujumbe kuwa "Samahani, muhamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi"japo hela kwenye akaunti yangu haikuonekana tena wala nilikotuma hakufika.

Baada ya masaa kadhaa wahospital wananipigia wameshafika hela haijafika ikabidi nipige voda huduma kwa wateja nilijibiwa kuna tatizo la mtandao mafundi wanashughulikia hela itafika nilikotuma nisiwe na wasiwasi, ikabidi niwaambie wale wa hospital kule nilichojibiwa ikabidi wajipapase wao wamlipe wa gari maana mimi sikuwa na hata senti tena,Nashukuru hospital alipokelewa vyema na kuanza matibabu japo mchana wa leo Mungu kamuita.

Tangu tarehe 25/4 hadi leo tarehe 3/5/2017 hiyo hela haikufika sehemu husika wala kwenye akaunti yangu haikurudishwa licha ya juhudi kubwa niliyoifanya ya kuwapigia kila siku bila mafanikio zaidi ya kuniahidi niwe mvumilivu.Leo asubuhi nilipopiga tena wamenitumia meseji hii"Tumepokea ombi lako lenye namba A7-TTEB-RF7L4 . Tutakujulisha punde litakapotatuliwa kabla ya 11-MAY-17 . Piga *106# kuhakiki usajili wa laini yako."

Kusudio la hela ilikuwa kumsaidia dada lakini VODACOM mkaamua kuikalia,sawa sina la kuwafanya basi naiomba mnirudishie itumike kwenye taratibu za kumpumzisha au niwaleteeni maiti ofisini mkamzike wenyewe?.
Andaa lawyer
Andaa ushahidi
Wapeleke kortini kudai fidia
Thats all
 
Ila Mkuu sijaelewa kitu kimoja kwenye andiko lako hiyo hela laki nne ulituma kwa ajili ya usafiri na matibabu? Wakati ndio ya salary yako yote? Au umekosea tarakimu?
 
Mkuu sijaelewa,so hospital hakupewa huduma,na hela ingefika huenda angepona sio
Kila jambo linamakusudio ya mungu kwahiyo siwezi kusema angepona lakini kwa macho ya kibinadamu labda hela wasingeishikilia ingesaidia sana
 
Imenigusa. Sana suruhisho. Layote. Fungua kesi. Mahakamani. Kwanza. Nenda Tcra. Toa. Mashitaka. Pare. Wataitwa. Naukiona. Hakiiaitendeki. Nenda. Mahakamani. Andaa. Ushahidi. Waizo. SMS. Walizo. Kutumia. Uwepia. Nacheti. Chakifo. Kuonyesha. Umempoteza. Dada. Kwauzembe. Wa. Vodacom
Huu uandishi wa wapi?!!!! This is too much oo!!
 
Nijambo la kusikitisha sana, cha msingi brother kama unaweza fanya hivi!.
Hakikisha ushahidi wote unao alkadhalika wa hospital na tarehe za maongezi,na vibari vya mapokezi hospital.Kisha mtafute wakili mwenye kuweza kukupangia utaratibu wa kufungua kesi.KWA MTAZAMO WA MBALI HAPO KUNA HELA YA FIDIA SIO KITOTO,MAANA NI WEWE TUU!
 
1. Tafuta lawyer, andika formal complaints pamoja na viambatanisho vyote kwenda baraza la walaji pale TCRA, ili vodacom wakulipe na usumbufu.
2. Lisiposhughulikiwa ndani ya muda tajwa, andaa ushahidi, wapeleke mahakamani, dai fidia.
 
Mkuu nakushauri nenda tcra kafaili kesi .... Nakusisitiza tena nenda tcra kafaili kesi utapata stahiki zako zote, achana nao hao Voda chamoto watakiona ....

Najua utabeza huu ushauri ila najua ninachokwambia na wewe ndio utakuwa mfano kwa watanzania Wote wasiwe wanakaa kimya kwa upuuzi wa makampuni...

Nenda tcra
Naungana na wewe kwa huu ushari
 
Kila jambo linamakusudio ya mungu kwahiyo siwezi kusema angepona lakini kwa macho ya kibinadamu labda hela wasingeishikilia ingesaidia sana
Kwenye maandiko yako umesema alipokelewa vizuri na matibabu yalianza bahati mbaya Mungu akamchukua. Kwa maana hio kuchelewa kwa hela hakukumkosesha matibabu. Pamoja na yote pole sana.
 
1. Tafuta lawyer, andika formal complaints pamoja na viambatanisho vyote kwenda baraza la walaji pale TCRA, ili vodacom wakulipe na usumbufu.
2. Lisiposhughulikiwa ndani ya muda tajwa, andaa ushahidi, wapeleke mahakamani, dai fidia.
Mkuu kampumzishe dada, halafu ukisha maliza taratibu za msiba fanyia kazi huu ushauri.
 
Pole sana ,Mungu akutie nguvu na hao VODACOM WACHUKULIWE HATUA INAYOWASTAHILI,APUMZIKE KWA AMANI DADA
 
Aise kumbe kweli mie hudhani stori kama hizi watu hutunga tu, pole sana. Mie kwa uzoefu wangu Huduma bora za miamala ya kifedha ni Tigo tu, hao voda hamna kitu, tupa hiyo line jiunge tigo, halafu mhudumu anakuuliza eti uliwapigia Airtel wakati wewe ni mteja wao Sasa hao Airtel wanakuhusu nini, Swali la kipuuzi kabisa
 
Pole sana sana.

Nimesikiliza hizo audio, huyo ni kama ulikuwa unamsumbua kwa jinsi anavyoongea sio kazini.
 
Kwenye maandiko yako umesema alipokelewa vizuri na matibabu yalianza bahati mbaya Mungu akamchukua. Kwa maana hio kuchelewa kwa hela hakukumkosesha matibabu. Pamoja na yote pole sana.

Ndio.. ila unajua kuna ambayo mtu huwezi kupata kama hauna pesa mkononi. Nafikiri hasingeandika kama hizo pesa ameona zisingesaidia. Amekaa siku 6 umesikiliza audio...!!! Duh...hata vipi ilibidi Voda wangemshauri cha kufanya, ipo kama vile wanaibia wateja.

BTW sitaki kufikiria walikuwaje siku zote kusubiria pesa hata kwa matibabu zaidi, na pesa imekwama then mgonjwa anafariki. Kwa lolote inasikitisha bora hata kujijua hamna hizo pesa.
 
Nadhani chini ya jua sidhani kama mahali huduma mbovu za customer care kama hapa nchini....

Yaani muhudumu anaongea utadhani yupo chumbani na hawara yake....!!!
 
Back
Top Bottom