Vodacom mmesababisha ndugu yangu kufariki, nawaletea maiti ofisini

Mbaya zaidi unakuta niwapiga dili.tu ndani ya hiyo ofisi ndo wanafanya haya mambo. Pasipo kuelewa hela nyingine zinapita humo kunusuru maisha ya wengine yaliyo hatarini.

Mungu awalaani kabisa kama kuna yeyote aliyeingia katika kutumia hiyo hela kwa lengo la kukukuibia wakati ni ya kumnusuru dada yako. Hiyo dhambi itawaandama milele
 
Mkuu nakushauri nenda tcra kafaili kesi .... Nakusisitiza tena nenda tcra kafaili kesi utapata stahiki zako zote, achana nao hao Voda chamoto watakiona ....

Najua utabeza huu ushauri ila najua ninachokwambia na wewe ndio utakuwa mfano kwa watanzania Wote wasiwe wanakaa kimya kwa upuuzi wa makampuni...

Nenda tcra
 
Wanaboa sana hawa Vodacom, wiki 2 unasubr hela yako MWENYEWE! Huu usenge cjui vp!

Bora Anko magu awashughulikie, miamala mingi lakn hata kwa magu haichangii! Mi nilishawahi kuwatolea maneno machafu maana wanaboa!
 
Naandika haya kwa uchungu dhidi ya huu mtandao wa vodacom.Tarehe 25/4 saa 7 na robo mchana nilipigiwa simu dada kazidiwa tena kutoka kwa majirani, niliwaomba watafute gari wamkimbize hospital mimi niombe ruhusu kibaruani nitawakuta huko.

Kwenye akaunti yangu ya mpesa nilikuwa nina 416,000 tena niliiweka mda mfupi tu baada ya kupewa haki yangu ya mwezi na boss hivyo ikanipasa nimrushie 400,000dada kwenye no yake ili walipie usafili na matibabu,nilipotuma ile hela vodacom wakanitumia ujumbe kuwa "Samahani, muhamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi"japo hela kwenye akaunti yangu haikuonekana tena wala nilikotuma hakufika.

Baada ya masaa kadhaa wahospital wananipigia wameshafika hela haijafika ikabidi nipige voda huduma kwa wateja nilijibiwa kuna tatizo la mtandao mafundi wanashughulikia hela itafika nilikotuma nisiwe na wasiwasi, ikabidi niwaambie wale wa hospital kule nilichojibiwa ikabidi wajipapase wao wamlipe wa gari maana mimi sikuwa na hata senti tena,Nashukuru hospital alipokelewa vyema na kuanza matibabu japo mchana wa leo Mungu kamuita.

Tangu tarehe 25/4 hadi leo tarehe 3/5/2017 hiyo hela haikufika sehemu husika wala kwenye akaunti yangu haikurudishwa licha ya juhudi kubwa niliyoifanya ya kuwapigia kila siku bila mafanikio zaidi ya kuniahidi niwe mvumilivu.Leo asubuhi nilipopiga tena wamenitumia meseji hii"Tumepokea ombi lako lenye namba A7-TTEB-RF7L4 . Tutakujulisha punde litakapotatuliwa kabla ya 11-MAY-17 . Piga *106# kuhakiki usajili wa laini yako."

Kusudio la hela ilikuwa kumsaidia dada lakini VODACOM mkaamua kuikalia,sawa sina la kuwafanya basi naiomba mnirudishie itumike kwenye taratibu za kumpumzisha au niwaleteeni maiti ofisini mkamzike wenyewe?.
Pole sana ndugu. Basi voda nao watakuwa wameanza tabia za Togo.
 
Imenigusa. Sana suruhisho. Layote. Fungua kesi. Mahakamani. Kwanza. Nenda Tcra. Toa. Mashitaka. Pare. Wataitwa. Naukiona. Hakiiaitendeki. Nenda. Mahakamani. Andaa. Ushahidi. Waizo. SMS. Walizo. Kutumia. Uwepia. Nacheti. Chakifo. Kuonyesha. Umempoteza. Dada. Kwauzembe. Wa. Vodacom
 
Pole sana ndugu!...haya ma mitandao ya simu yanaponikeraga ni hapo tu,yaani inatokea shids unarusha hela wanakaa nayo eti tatizo la ufundi,zinapita siku mpk wiki,kudadadeki zenu nyie vodacom na wengine
 
pole sana mkuu, ndio tabu ya mitandao yetu hii, tatizo kubwa hatuna pa kusemea ila huwa wanakera sana hawa jamaa, yaan kuna kipindi fln nilikuwa nafanya malipo ya bingo kupitia kampun iyo iyo uliyoitaja, cha ajabu miamala yote niliyokuwa nikiifanya ilikuwa ina fail na kubaki hewan, hali iliyopelekea mm kufungiwa mashine zangu na kunikosesha pesa na ukiwapigia majibu yao ni mepes kama wako choon vile, yan wanakera sana hawa mbwa
 
Hawa watu tukisema hizi hela wanafanyia biashara kwamuda wote huo halafu wanaturudishia tutakuwa tunakosea?

Kwa nini hela ipotee muda wote huo?
 
Naandika haya kwa uchungu dhidi ya huu mtandao wa vodacom.Tarehe 25/4 saa 7 na robo mchana nilipigiwa simu dada kazidiwa tena kutoka kwa majirani, niliwaomba watafute gari wamkimbize hospital mimi niombe ruhusu kibaruani nitawakuta huko.

Kwenye akaunti yangu ya mpesa nilikuwa nina 416,000 tena niliiweka mda mfupi tu baada ya kupewa haki yangu ya mwezi na boss hivyo ikanipasa nimrushie 400,000dada kwenye no yake ili walipie usafili na matibabu,nilipotuma ile hela vodacom wakanitumia ujumbe kuwa "Samahani, muhamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi"japo hela kwenye akaunti yangu haikuonekana tena wala nilikotuma hakufika.

Baada ya masaa kadhaa wahospital wananipigia wameshafika hela haijafika ikabidi nipige voda huduma kwa wateja nilijibiwa kuna tatizo la mtandao mafundi wanashughulikia hela itafika nilikotuma nisiwe na wasiwasi, ikabidi niwaambie wale wa hospital kule nilichojibiwa ikabidi wajipapase wao wamlipe wa gari maana mimi sikuwa na hata senti tena,Nashukuru hospital alipokelewa vyema na kuanza matibabu japo mchana wa leo Mungu kamuita.

Tangu tarehe 25/4 hadi leo tarehe 3/5/2017 hiyo hela haikufika sehemu husika wala kwenye akaunti yangu haikurudishwa licha ya juhudi kubwa niliyoifanya ya kuwapigia kila siku bila mafanikio zaidi ya kuniahidi niwe mvumilivu.Leo asubuhi nilipopiga tena wamenitumia meseji hii"Tumepokea ombi lako lenye namba A7-TTEB-RF7L4 . Tutakujulisha punde litakapotatuliwa kabla ya 11-MAY-17 . Piga *106# kuhakiki usajili wa laini yako."

Kusudio la hela ilikuwa kumsaidia dada lakini VODACOM mkaamua kuikalia,sawa sina la kuwafanya basi naiomba mnirudishie itumike kwenye taratibu za kumpumzisha au niwaleteeni maiti ofisini mkamzike wenyewe?.
Pole Sana mkuu.....fikisha malalamiko yako TCRA.
 
Back
Top Bottom