Vituko vya X zangu, Kwenye Harusi yangu

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
506
3,134
Hata kabla sijatangaza kuwa naoa, nilikuwa na hofu kuhusu Ma X zangu wawili, nilijua kutokana na Ukaribu wa familia zetu lazima habari zingewafikia na lazima wangekuwepo siku ya Harusi yangu.

Kilichokuwa kikinipa mawazo ni kwamba hawa Ma X zangu hatukuachana vizuri. Halafu akili zao mbovu nazijua. Baadhi ya wana, familia na Marafiki walikuwa wakiwajua.

Mfano, mmoja Kati yao ilinibidi niachane nae kinguvu mwezi mmoja kabla ya Kutangaza Kikao cha Kwanza cha Harusi. Alivyosikia naoa alinipigia simu na kuniahidi lazima atakuja kufanya varangati, nakumbuka alinipigia simu na kuniambia “Wewe si kidume, Jiandae kudhalilika Baba”

Nikiri wazi kuwa huyu demu alikuwa akinipenda sana, hata kuachana kwetu nilifanya kazi sana, hakuridhika.

Kwa hiyo wakati wote wa Vikao, hili swala lilikuwa likinipa vimawazo vya hapa na pale. Nilijua lazima watakuwepo, Je nitawakabili kwa macho ya aina gani pale mbele? Hawa mademu wao walikuwa hawajuani.

Huyo mwengine sikuwa na hofu nae sana sababu nilijua siku ya harusi lazima wazazi wake watakuwepo, kwa hiyo niliamini hatoweza kufanya drama mbele ya wazazi wake, lakini pia kwa heshima ya kazi yake Serikalini niliamini asingeweza kufanya utoto wowote. Nilijipa moyo.

Ebhana siku hazigandi, mara siku ya harusi ikafika. Kuondoa mawazo na ile aibu, tulivyotoka tu Kanisani na Bibie, kwenye gari tuliyopanda kuna mhuni wangu mmoja nilimwambia aniwekee Serengeti Light za Kutosha kwenye gari.

Wakati tupo Beach watu wanapiga mapicha, Mimi akili yangu haikuwepo pale kabisa, nilikuwa natoka narudi, natoka narudi hadi kwenye gari, nakunywa pombe zangu kwa siri kisha narudi kupiga picha, nakumbuka mpaka Dereva wetu alinishangaa. Nakumbuka aliniambia “Vipi Mzee uko sawa, angalia usije Kuzima”

Kwa kifupi nilikuwa nawawaza sana wale mademu. Kila muda ulivyosogea hofu ilinizidi, Tukamaliza kupiga mapicha picha pale hao, safari hadi Ukumbini.

Ule muda tunasubiri watu wote waingie Ukumbini ndo Maharusi tushuke kwenye gari, Mimi nilikuwa busy kunywa pombe zangu. Mpaka wife alikuwa ananishangaa. Nilikuwa na mdanganya kuwa bila kunywa pombe sitaweza kucheza mziki vizuri mbele za watu. Aliniamini.

Mara ule muda wa maharusi kuingia ukumbini ukawadia. Hao tukaingia huku tunacheza. Watu wote walikuwa wamesimama kutushangilia maharusi. Baada ya kuzipita Meza kama mbili tatu, Macho yangu yakatua kwa X wa kwanza, yule Mfanyakazi wa Serikali, kutokana na pombe nilizokuwa nazo kichwani sikujali sana, nikajikaza.

Kufika mbele, bado nikiwa na Bibie tunacheza nashangaa X wangu wa Pili amekaa kwenye Meza Kuu ya Wazazi wangu. Dah

Kitendo cha kumuona pale Mbele kilinishtua sana na kunitoa nje ya Mchezo. Pale mbele tayari Wasindikizaji wetu (Mates) 12 walikuwepo, Mziki ukafunguliwa pale tukaendelea kucheza.

Watu wote wakaungana na sisi katika kucheza. Wakati tunaendelea kucheza nikamstua rafiki yangu mmoja, nikamwambia nisaidie vitu viwili, chukua glass pita kimya kimya kaniwekee pombe bila mtu yoyote kujua. Nilimwomba hivi sababu nilijua kama pombe ingeisha kichwani nisingeweza kuwakabili hawa watu wawili.

Jamaa alifanya kama nilivyomuomba. Huyu jamaa angu alikuwa anajua kila kilichokuwa kikiendelea. Katikati ya kucheza mziki, ghafla namuona X wangu yule wa Kitengo huyu hapa pamoja na Wazazi wake. Nikawa nazuga zuga tu pale. Moyoni nikawa nasema hapa bila pombe sitoboi, hata kucheza mziki ni kama nilianza kupoteza step.

Jamaa yangu alivyorudi na kunikabidhi glass ya pombe kiaina bila watu kujua, nikamwambia jamaa yangu sikia, ebhana fanya kila unavyoweza kamtoe fulani pale kwenye Meza ya Wazazi. Ongea nae kwa namna utakayoweza wewe lakini pale atoke. Jamaa angu akatikisa kichwa na kuondoka.

Baada ya nyimbo mbili tatu, watu wote wakarudi zao Kukaa. Sasa shughuli ndo inaanza rasmi, sara na utambulisho. Kutupa Jicho pale meza Kuu, namuona Bibie bado amekaa pale pale.

Moyoni nikasema huyu anataka kuniaribia shughuli, anataka kunikosesha furaha tu na mimi siwezi kukubali kukosa furaha kwenye siku yangu kubwa kama hii. Hapo tayari pombe zimekubali kichwani. Nawaza tu kama nitaweza hata kutambulisha watu vizuri kwa mpangilio mzuri.

Nikajikaza nikaanza kutambulisha waliokaa Meza Kuu. Meza kuu kulikuwa na watu wanafika hata 15 pamoja na ndugu zangu waliotoka Mikoani na Vijijini.

Nikaanza kutambulisha pale, Bibie alikuwa amekaa pembeni ya Bibi yangu mzaa Baba, utambulisho ulivyofika kwake nikamruka nikaendelea kutambulisha wageni wengine mpaka nikamaliza watu wote. Nashukuru Mungu zoezi la Kutambulisha watu lilipita salama, japo mdomo ulikuwa mzito kidogo kutokana na nilikuwa nimeshalewa. Ila nadhani wadau hawakujua.

Ratiba nyengine zikaendelea mle Ukumbini. sasa kutokana na pombe nilizokuwa nimeanza kunywa tangu Beach, nilijisikia hali ya kwenda toi. Nikamshtua Bibi Harusi.

Watu wakati wanaendelea kucheza Mziki nikatoroka kidogo kwenda Toi.

Kumbe yule demu ni kama muda wote alikuwa ananiangalia mimi, maana nilivyotoka tu Toi huyu hapa. Kanifata na kunishika Mkono, amekunja sura, nikamuomba twende pembeni tukaongee.

Watu walikuwa busy wanapita pita. Tukatoka hadi nje kabisa ya ukumbini, sehemu moja kwenye giza karibu na magari, pembeni ya Costa tukasimama. Akaanza kuongea kwa jazba pale.

“I just came to tell you that I hate you, I hate you”

Demu akanikunja suti yangu, huku analia.

Hapo yeye analia lakini mimi nina wasiwasi kama endepo kuna mtu atapita na kutuona. Nilihisi kwenye ile Costa kama kulikuwa na dereva na Konda wake, Basi macho yangu muda wote nilikuwa nayageuza geuza. Nawaza yani watu wapite halafu waone Bwana Harusi amekunjwa itakuaje?

Nikawa Najaribu kumsihi kwa kumwambia kesho nitamtafuta tuongee vizuri. Lakini wapi hasikii, analia tu huku amenikunja anasema “I hate you” “I hate you”

Nikamshika mikono yake na kujitoa, nikaondoka pale haraka kurudi Ukumbini, nilimwacha pale bado ana hasira na mimi nimevurugwa sababu suti yangu kwenye eneo la bega imejikunja sana kiasi cha mtu kuweza kuona na kugundua. Nilirudi chooni na kujaribu kuiweka sawa lakini kwa mbali bado iliweza kuonesha mikunjo kunjo.

Nikarudi Ukumbini watu walikuwa wanamalizia kucheza Mziki, muda wa zawadi umefika. Bibi harusi aliniuliza mbona Suti yako imejikunja hivyo, nikajifanya kama sijamsikia nikazuga pale.

Watu wanapita na kutoa zawadi, mara namuona yule X wangu wa Kitengo anakuja kutoa zawadi ameambatana na familia yake. Niliona ameacha Bahasha fulani kwa wapokea zawadi kisha akasogea kwa Maharusi kutoa mkono wa Pongezi. Nilimpa Mkono lakini sikuwa sawa kabisa. Aliniangalia na kitabasamu fulani hivi cha kejeli.

Kusema ukweli Mpaka hapo furaha yote ya siku yangu muhimu haikuwepo tena. Natamani harusi iishe tu tuondoke. Pombe kichwani naona kabisa inapungua.

Washkaji zangu niliowapa kazi ya kuhakikisha muda wote wawe wanapita pita pale mbele wakiona glass yangu ya pombe imekwisha waniletee nyengine, niliona na wao walishalewa tayari, mimi hawakunikumbuka tena.

Nawaza huyu Mwanamke kwenye ile Bahasha ameweka nini?
 
Hata kabla sijatangaza kuwa naoa, nilikuwa na hofu kuhusu Ma X zangu wawili, nilijua kutokana na Ukaribu wa familia zetu lazima habari zingewafikia na lazima wangekuwepo siku ya Harusi yangu.

Kilichokuwa kikinipa mawazo ni kwamba hawa Ma X zangu hatukuachana vizuri. Halafu akili zao mbovu nazijua. Baadhi ya wana, familia na Marafiki walikuwa wakiwajua.

Mfano, mmoja Kati yao ilinibidi niachane nae kinguvu mwezi mmoja kabla ya Kutangaza Kikao cha Kwanza cha Harusi. Alivyosikia naoa alinipigia simu na kuniahidi lazima atakuja kufanya varangati, nakumbuka alinipigia simu na kuniambia “Wewe si kidume, Jiandae kudhalilika Baba”

Nikiri wazi kuwa huyu demu alikuwa akinipenda sana, hata kuachana kwetu nilifanya kazi sana, hakuridhika.

Kwa hiyo wakati wote wa Vikao, hili swala lilikuwa likinipa vimawazo vya hapa na pale. Nilijua lazima watakuwepo, Je nitawakabili kwa macho ya aina gani pale mbele? Hawa mademu wao walikuwa hawajuani.

Huyo mwengine sikuwa na hofu nae sana sababu nilijua siku ya harusi lazima wazazi wake watakuwepo, kwa hiyo niliamini hatoweza kufanya drama mbele ya wazazi wake, lakini pia kwa heshima ya kazi yake Serikalini niliamini asingeweza kufanya utoto wowote. Nilijipa moyo.

Ebhana siku hazigandi, mara siku ya harusi ikafika. Kuondoa mawazo na ile aibu, tulivyotoka tu Kanisani na Bibie, kwenye gari tuliyopanda kuna mhuni wangu mmoja nilimwambia aniwekee Serengeti Light za Kutosha kwenye gari.

Wakati tupo Beach watu wanapiga mapicha, Mimi akili yangu haikuwepo pale kabisa, nilikuwa natoka narudi, natoka narudi hadi kwenye gari, nakunywa pombe zangu kwa siri kisha narudi kupiga picha, nakumbuka mpaka Dereva wetu alinishangaa. Nakumbuka aliniambia “Vipi Mzee uko sawa, angalia usije Kuzima”

Kwa kifupi nilikuwa nawawaza sana wale mademu. Kila muda ulivyosogea hofu ilinizidi, Tukamaliza kupiga mapicha picha pale hao, safari hadi Ukumbini.

Ule muda tunasubiri watu wote waingie Ukumbini ndo Maharusi tushuke kwenye gari, Mimi nilikuwa busy kunywa pombe zangu. Mpaka wife alikuwa ananishangaa. Nilikuwa na mdanganya kuwa bila kunywa pombe sitaweza kucheza mziki vizuri mbele za watu. Aliniamini.

Mara ule muda wa maharusi kuingia ukumbini ukawadia. Hao tukaingia huku tunacheza. Watu wote walikuwa wamesimama kutushangilia maharusi. Baada ya kuzipita Meza kama mbili tatu, Macho yangu yakatua kwa X wa kwanza, yule Mfanyakazi wa Serikali, kutokana na pombe nilizokuwa nazo kichwani sikujali sana, nikajikaza.

Kufika mbele, bado nikiwa na Bibie tunacheza nashangaa X wangu wa Pili amekaa kwenye Meza Kuu ya Wazazi wangu. Dah

Inaendelea

"mmoja Kati yao ilinibidi niachane nae kinguvu mwezi mmoja kabla ya Kutangaza Kikao cha Kwanza cha Harusi"

Kwa tabi hizi huwezi kua na ndoa nzuri ya furaha.
 
Back
Top Bottom