mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,873
- 18,433
Lengo kubwa la mataifa ya magharibi ni kuiangusha kiuchumi Urusi ili hatimaye idhoofike kijeshi.
Kufikia lengo hilo walimpata rais msanii na mchekeshaji Zelensky wa Ukraine, ambaye walimvimbisha kichwa na kumdanganya kuwa aigomee Urusi kuhusu kuruhusu majimbo ya mawili yaliyoko mashariki mwa Ukraine yawe na utawala wa ndani ulio huru bila kuingiliwa na Ukraine kama ilivyo Hongkong.
Kwa hiyo Zelensky akagoma kutekeleza makubaliano yaliyodhaminiwa na mataifa manne (Ujerumani, Ufaransa, Ukraine na Urusi). Mabeberu wakamdanganya kuwa watamwingiza NATO na hapo Urusi itaogopa kuishambulia.
Sambamba na ulaghai huo wakampatia shehena kubwa ya silaha na fedha ili awe na uwezo wa kujilinda. Lengo ni kwamba Ukraine itafanikiwa kuikera Urusi hadi Urusi ishindwe kuvumilia na iishambulie Ukraine.
Kwa hiyo siku Urusi iliamua kuishambulia Ukraine ilikuwa ni USHINDI MKUBWA kwa mbinu hii ya mabeberu na walishangilia sana kwa siri huku kwa hadhara wakitoa machozi ya mamba!!
Walifurahi kwa sababu hatimaye wamepata sababu ya "HALALI" ya kuiwekea VIKWAZO vikubwa mno Urusi na kujaribu kuitenga na kuisusia katika nyanja zote ikiwemo ya michezo!!
Wakiamini kwamba kwa kutumia vikwazo hivi lazima Urusi itaporomoka kiuchumi hadi ishindwe kutunza na kuendeleza jeshi lake.
Akiba yote ya Urusi iliyowekezwa nchi za nje ilichukuliwa zikiwemo mali binafsi za watu!! Ikatolewa kwenye mfumo wa kibenki wa kimataifa wa kutuma na kupokea pesa!
Wakazuiwa kutumia dola wa Euro! Kwa vikwazo hivyo pesa ya URUSI iliporomoka sana thamani! Lakini mabeberu hawakujua URUSI itajibu mapigo vipi!!
Siku ya URUSI kujibu mapigo ikawa imewadia!! Urusi ikatangaza kuwa kila atakayekuwa anahitaji bidhaa za Urusi kutoka nchi zote zilizoiwekea vikwazo, itabidi zilipe kwa pesa ya ndani ya urusi iitwayo RUBLE!!
Hilo tangazo moja lilitosha kupandisha thamani ya Ruble ndani ya wiki moja kwa asilimia 50% kutoka hapo chini ilipokuwa imefikia.
India ikatangaza kununua mafuta ya Urusi kwa kutumia Ruble japo haikuwa imeiwekea vikwazo!! Yaani nchi za ulaya magharibi inabidi ziingie sokoni kununua Ruble ili ziweze kupata mafuta.
Urusi ikasema sipokei dola wala Euro maana hizo hazina tena thamani kwangu!! Wakitaka watoe dhahabu kwa Urusi ili wanunue Ruble kisha walipie mafuta!!
Hilo likawachanganya sana na mataifa yanayounda G7 yalipokutana hivi majuzi walilijadili hilo na kuamua kwa pamoja kuwa HAWAKUBALI kulipia mafuta kwa Ruble!!
Siku hiyo hiyo G7 walipoweka msimamo huo URUSI ikatangaza kuwa KUANZIA TAREHE 31/03/2022, URUSI ITASITISHA HUDUMA YA KUUZA MAFUTA KWA NCHI ITAKAYOGOMA KULIPIA KWA RUBLE!!! Hapo ndipo ninaposema hii vita imefikia patamu!!!
Je ni yupi atanyoosha mikono!!! Ufahamu kuwa ulaya magharibi inategemea aslimia 40 ya mahitaji yake ya gesi kutoka Urusi. Je watakubali kufungiwa huduma ya gesi na Urusi!! Jibu linalotazamiwa ni kuwa HAWATAWEZA!!
Wakigoma ndani ya wiki moja hali itakuwa mbaya sana na itazua taharuki kubwa na Mataifa ya ulaya hayatatawalika kwa vurugu zitakazoibuka!
Kama wakiikubalia Urusi na kuanza kulipa kwa RUBLE pesa ya Urusi itapanda sana thamani na ile ya dola na EURO itashuka.
Mwisho wa siku vikwazo vilivyotegemewa kuiangusha Urusi kiuchumi vitageuka na kuiinua Urusi kiuchumi na kuangusha uchumi wa nchi za magharibi!!
Tarehe 31 ni keshokutwa tu ngoja tusubiri tuone!!