Hakuna mtu anayejua madhara ya Vita atapenda kusikia Ati Marekani na North Korea wapo kwenye hali ya hatari ya kupigana.
Vita haina macho vita haichagui vita haibakizi mtu zaidi ya kuacha vilema,Vifo,Yatima na uharibifu mkubwa wa Miundombinu,Nashangwaza Sana na baadhi ya watu humu wakifurahia hali ya kutoleewana kati ya Marekani Na Korea Kaskazini ukitaka kujua Ubaya wa vita Mtafute Mzee yoyote wa Kagera akwambie madhara yake.
Leo nchi nyingine zinapatanishwa ziache vita wengine wanafurahia Vita Acheni utani ndugu zangu ni watoto wangapi leo Libya,Iraq,Syria wamepoteza waazazi na Wamama wangapi leo wamebaki wajane??
Nimefanikiwa kuangalia Muvi moja wanajaita JANJAWEED nikasema hapana Vita ni mbaya watu wanaua watoto hata wasio na hatia Mama hajui hata kushika kisu unamua Vita ni Mbaya.
Maswali machache Kwanini Korea Kaskazini wanataka kumiliki silaha hizo?na kama ni Mikataba ilisainiwa kwanini wao wavunje na watake kumiliki Silaha hizo za hatari?
Tulishuhudia Juzi pale Syria watu wanatumia silaha za kemikali kuua Raia wasio na hatia hata kidogo,Tulishuhudia Iraq Mtu anayeitwa Chemical akiua Wananchi kama Vile anaua ndege waharibifu Kweleakwelea kwa kutumia silaha za kikemikali.
Umoja wa Mataifa Unamaana kubwa sana kupiga Vita usambazaji/utengenezwaji wa Silaha hatari kama vile za kinyuklia,kikemikali,na kibiologia,Chukulia mfano hizi Silaha zikawafikia Magenge hatari duniani/magaidi unategemea nini?
Wazungu wanasema Vita ni Hatua za Mwisho kabisa endapo muafaka utashindwa kupatikana sidhani kama Mataifa yote yameshindwa kumzibiti Korea Kaskazini kwa Njia ya Mazungumzo.
Vita Haichagui Tuombe sana Juu ya Marekani na Korea Kaskazini muafaka upatikane badala ya Vita.
IJUMAA NJEMA.