Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,454
- 3,188
Salaam,
Leo nimewiwa kulisema jambo hili kwani kila mwaka naona linazidi kukua tu badala ya kufifia. Swala lenyewe ni hili la kufuturisha watu kipindi cha mwezi wa ramadhani. Kwanza kabisa tuwekane sawa hapa NI MWEZI WA RAMADHANI na SIYO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI kama wengi walivyozoea kuuita. Najua unashangaa lakini ndo ukweli huo usiojulikana kwa wengi MIEZI MITUKUFU IPO MINNE kwa waislamu na RAMADHANI si katika miezi mitukufu! Nitaleta darasa kamili juu ya jambo hili ila kwa sasa tuishie hapo.
Kumekuwa na kawaida ya watu kupupia heri na fadhila za mwezi wa ramadhani, ni jambo jema kabisa hilo kama mtu atazingatia sheria na kukusudia thawabu tu na si vinginevyo! Lakini wengine wanafanya baadhi ya mambo hayo kwa malengo ya maslahi ya hapa duniani. Hatukatai kujitengenezea mazingira mazuri duniani lakini mtu anapaswa aangalie je njia ya kujitengenezea mazingira hayo inaruhusika kwa sheria ya dini
Tujiulize maswali haya kwa pamoja
1. Kama ni heri za mwezi wa ramadhani kwanini iwe ni kufuturisha tu? Kwanini isiwe na mambo mengine ya heri? Mbona kuna mambo mengi ya kufanya na mengine yana heri nyingi kuliko hilo la kufuturisha? Ni sadaka? Yes, sasa hebu nikutajie mambo kadhaa hapa ambayo ni sadaka pia halafu uone mwenyewe kama kuna hata moja wamewahi kuthubutu hao watafuta kiki
A. Kuwanunulia vitabu vya quran watoto wa madarasa
B. Kumchukua yatima na kumhudumia
C. Kuwalisha daku wafungaji yaani kuwapatia mlo wa daku
D. Kuchangia ujenzi wa misikiti na madrasa
E. Kuchimba visima vya maji na kuwezesha huduma ndogo ndogo za misikitini
F. KUwawezesha posho/ kulipa walimu ili watoe elimu kwa umma
G. Kusaidia kulipa madeni watu wema wenye madeni sugu nk
Inawezekana mtu anashangaa niliposema kuna yenye fadhila kubwa kuliko kufuturisha!
2. Kwanini ni viwanjani (kwenye mikusanyiko) tu? Sawa hilo linaweza kuwa sahihi sana kwa aliyefuata sharia lakini kwanini ni aina (ya makundi) fulani ya watu tu tena captions zinakuwa nyingi kila mtu ajue kuwa umefuturishwa/umefuturisha?. Wenzenu wanaokusudia thawabu anafuturisha kwenye kadamnasi lakini za kimyakimya nyumba kwa nyumba nazo zinakuwepo.
Angalia makundi haya hayakumbukwi kabisa
A. Wafungwa wanaofunga. Hawa wanatekeleza ibada ya swaum kwa shida lakini kule mtaani kuna kibopa anagawa chakula barabarani muda wa magharibi mpaka adheist kina Kiranga wanakifaidi! Wengine wanakichezea
B. Wanafunzi mashuleni. Kama kuna watu wanatia huruma ni wanafunzi aisee kila mwaka unasikia andikeni barua mpewe futari lakini haijawahi kutokea watoto hawa kupewa futari. Barua zinaandikwa kila mwaka kwa mkurugenzi, mkuu wa wilaya, bakwata, vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia lakini hutaona hata mmoja akija wala kusema neno! Watoto ni watoto tu wengine wanavunjika moyo wakiona hali ngumu hawafungi!
C. Wagonjwa. Kuna waliopo majumbani kuna waliopo mahospitalini wote wanapata tabu tu hakuna anayewajali kivile na ramadhani hii
Viongozi wengi wa serikali, wa kisiasa, wafanyabishara na hata baadhi ya viongozi wa dini wameamua kutumia futari kama njia ya kuwanasa watu wanaowahitaji katika kufanikisha wao kubaki kwenye nafasi walizonazo au kupanda zaidi!
Wanasiasa wanafuturisha ili kutafuta idadi ya wapiga kura, viongozi wa serikali wanafuturisha ili kutafuta vyeo, wafanyabishara wanafuturisha kutafuta masoko, viongozi wa dini wanafuturisha kutafuta followers nk. Wote hao wanajitokeza hadharani na mapicha kibao, utaona captions tu
Rai yangu kufuturisha ni jambo jema sana tena sana lakini Enyi waislamu mliojaaliwa hebu fanyeni kwa kufuata sharia ya dini inasemaje na si kufanya vile mnavyojisikia. UKIFANYA AMALI YOYOTE KWA NIA YA KUTAKA SIFA NA ATTENTION YA WATU (KUJIONESHA, KUJIGAMBA, NK) tayari HATA JAMBO HILO LIWE LIMEWASAIDIA WATU KIASI GANI BADO LITAGEUZWA KUWA NI RIA na mfanyaji ataadhibiwa
Mwisho kuna watu ambao si waislamu nao wamekuwa wakipenda kufanya jambo hili la kufuturisha, ni vizuri lakini KWA KUWA RAMADHANI NI JAMBO LA WAISLAMU NA MMEAMUA KUWASAPOTI WAISLAMU KWENYE JAMBO LAO HILO BASI WAULIZENI HAO VIONGOZI WA KIISLAMU ILI MPEWE TARATIBU ZA KUFUATA KATIKA JAMBO HILI