Mbabani
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,415
- 4,035
Habari wapenda "futiboli".
Kabla ya kuajiriwa Robertinho alikuepo Zoran ambaye hakudumu na Simba kwa muda mrefu akatimka zake.
Moja ya sababu kubwa zilizomuondoa Zoran pale unyamani ni kuwakataa baadhi ya wachezaji kua hawaendani na falsafa zake na bahati mbaya baadhi ya wachezaji hao ni vipenzi vya mashabiki na viongozi, hivyo wakashindwana jamaa akasepa zake.
Akaja Mgunda "Guardiola mnene" kutoka Tanga, akaja na falsafa yake ya "boli litembee". Akalipwa pesa kidogo ila "boli likatembea kwelikweli" wakamtoa na kuleta kocha mbrazil Robertinho ambaye wakamlipa mshahara mnono zaidi akayaanza maisha ndani ya msimbazi.
Safari yake alianza kama Zoran, bwana Robertinho hakuvutiwa na uwezo wa baadhi ya wachezaji kama Clatous Chota Chama ambaye uwezo wake umeshuka sana na hawezi kurudi kwenye "form" ile ya 2018 au 2019. Akamfanyia sub kwenye moja ya mechi za ligi kuu, mashabiki wakapiga kelele sana "kama chama haingii kwenye mfumo basi kocha aingie kwenye mfumo la sivyo kocha atuachie timu yetu". Viongozi nao wakapita na upepo wa mashabiki "oya oya".
Robertinho akawa mpole, ikabidi amtumie hivyo hivyo hakua na namna. Akajitahidi kuleta pira "objektivu" akatolewa kwa mikwaju ya penat na Wydad (¼ fainali CCL).
Akaomba msimu unaofuata asajiliwe wachezaji wazuri kuja kumsaidia kutimiza malengo ya timu. Viongozi wakafanya usajili wa kufurahisha mashabiki na kupiga pesa za mwekezaji hivyo "wakaokota okota" wachezaji wakawaida wakitegemea kuja kupata matokeo makubwa.
Wamepigwa na mtani goli 5 wakapagawa, wakamtimua kocha huku wakidai wamehujumiwa na wachezaji.
Kiongozi mkubwa tena "kubwa jinga" akaja na kauli za "kimbumbumbu" eti "Kiongozi wa FIFA amesifia simba ilicheza mpira mzuri kuliko wa Wydad na Masandawana (kwa kawaida unaona viongozi nao wanachangamoto sana).
Makosa mliyoyafanya kukumbatia wachezaji waliokwisha viwango akina Bocco, Zimbwe, Chama n.k. Pia kusajili wachezaji wa kawaida akina Somba Onana kisha mnapiga "cha juu" na mnalazimisha fulani lazima acheze na nyie mashabiki acheni kocha afanye kazi yake, kama kocha hamtaki mchezaji fulani, acheni kuzomea zomea.
Viongozi na mashabiki mwacheni kocha afanye kazi yake.
kocha mdaini matokeo na makombe.