lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,472
Vijana Hawa wa kizazi hiki wa CCM Ni tofauti kubwa Sana na vijana wa wakati ule,enzi za akina Mwalimu,Malechela,Kikwete,n.k.
Hawa walikua na hoja kwenye mijadala mbalimbali na hata ya Kimataifa.
Tanzania ikiwakilishwa na vijana wa wakati huo ilikonga nyoyo za washiriki wa makongamano Kimataifa .
Nasikia na nimesoma kuwa waliweza kuiwakilisha vema Tanzania kwa hoja zao motomoto,nyingi zikiitetea Tanzania na zaidi Afrika.
Sasa leo Tuna Product mpya ya vijana wa CCM ambao Ni vituko na majanga kwa Taifa,hawana hoja ila Wana vioja.
Uzuri siku hizi mijadala ipo kila siku kila sehemu,Ni rahisi kufuata mijadala na kuipima kwa sababu mijadala mingi imo kwenye mitandao ya kijamii.
Humu kwenye mitandao ya kijamii ndio utaona vituko na majanga ya Hawa vijana wa CCM ambao chama Chao ndio kinawatumia kukjitetea chama chao.
Mifano.
Kijana wa CCM atakuambia
_Kabla ya Ben Sanane hajapotea alipokua akiripoti vitisho,vijana wa CCM walisema anatafuta Kiki.
_Abdul Nondo alipopotea Vijana wa CCM walisema anatafuta Kiki,alijiteka.
_Roma mkatoliki alipotekwa vijana walisema kajiteka kutafuta Kiki.
_Ofisi za vyama vya Upinzani zikichomwa,vijana wanakuambia CDM wamechoma wenyewe kutafuta Kiki.
_Tundu alipokua akitoa taarifa kuhusu kufuataliwa na vitisho vya watesi wake,vijana wa CCM walisema anatafuta Kiki.
_Masikini Lissu alipigwa marisasi mengi Sana,vijana wa CCM walisema CDM wamempiga wenyewe ili kutafuta kiki.lol!
_vijana wa CCM wanaambiwa Wapinzani wakishinda Uchaguzi watabomoa madaraja na miundo mbinu halafu wauze screpa,halafu wanapiga makofi.
_Jana Kuna vijana wa CCM wamefanya vurugu kwenye mkutano wa Lissu huku wakidai hawamtaki Lissu jimboni Hai, wakati Hai Ni sehemu ya Tanzania na Bado miezi miwili tu watumie njia ya demokrasia ya kumkataa kwa box la kura.vijana wa CCM Hawa.
Mambo Ni mengi Sana ya ajabu wanaongea mitandaoni na majukwaani.
Sasa kitu ninachoshangaa, kama wapinzani wanajiteka,wanachoma, ofisi,wanampiga mwenzao Kwa risasi Lissu Ili watafute Kiki.Sasa kwa Nini wasiwaambie baba zao akina Magufuli,Siro na Diwani kwa kuwa wana kila Aina ya kifaa ili wawakamate akina Mbowe na Chadema wengine wanaojiteka,wanaochoma ofisi zao na waliompiga Lissu risasi ili kuwaumbua Chadema,Mbowe ,Lema,Lissu na wengine wote wenye michezo hiyo ili dunia ijue na iwahukumu Chadema?
Na hapo ndio watakua wamepata pointi ya kuvifuta vyama vya Upinzani?
Kwa mtazamo wangu,nawona vijana wa CCM huku mitandaoni na majukwaa mengine Kama vile wanasaidia kuididimiza CCM machoni na masikioni na mioyoni mwa jamii kwa kasi kubwa Sana.
Wananchi wana akili na uelewa mpana Sana,wanawadharau ,kuwapuuza na kibaya zaidi wanazidi kuichukia CCM.
Fikiria kijana wa Mtaani,mwanachama wa chama cha upinzani anaitangazia jamii na anaitaarifu Polisi kuwa anatishiwa kuuwawa,halafu vijana wa CCM wanamjibu kua anatafuta Kiki.Halafu baada ya muda kijana huyo anapote,na hapatikani Tena,wakati Kuna vijana wa CCM walisema amejiteka mwenyewe kutafuta Kiki,jamii kweli itaipend a CCM?
Mwingine anaitaarifu Polisi na jamii kuwa anafuatiliwa kuuwawa,vijaana wa CCM wanasema anatafuta Kiki,halafu baada ya muda huyo mtu anashambuliwa na anakufa mazima(Mawazo),
mwingine anajreuhiwa na kuwa mlemavu.Je jamii itaipenda CCM?
_Vijana wengine wa CCM wamesikika wakisema Hatuwezi kumpa nchi mtu mlemavu,Lol!
Je jamii inayojua ukweli wa kuwa huyo mlemavu zamani alikua mzima,hakuzaliwa mlemavu,je jamii hiyo itaipenda CCM?
Je wanaogawa Uraisi Ni vijana wa CCM au Wapiga kura?
Je wapigakura wengi wakimchagua huyo mnayemuita mlemavu mtazikataa kura zao?
Mambo Ni mengi,ngoja niishie hapa,ila CCM kubalini kataeni vijana wenu mliowapa dhamana ya kuwatetea nakuambieni kuwa Hawa ndio wanachangia kuifuta kwa kasi kubwa sana CCM mioyoni mwa watu.