KERO Vibarua maopereta wa mashine DP World tunapitia changamoto nyingi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari muda huu, natumaini nyote ni wazima wa afya, mimi ni mmoja kati ya maopareta vibarua katika bandari ya DSM ambapo kwa sasa ipo chini ya Dp World.

Kiuhalisia tunapitia mazingira magumu ya kazi na kipato ni kidogo ambacho ni chini ya Dollar 4 ukilinganisha na kazi tunazofanya.

Mfano mzuri maopereta wa Terminal tractor tunaingia kwenye mionzi Zaidi ya saa 9 bila kupumzika kwa siku lakini hatuna Bima, chakula, mikataba wala vifaa vya kuzuia mionzi, tukihoji tunaambiwa tusitegemee kupewa chochote hapo juu kwani wao wamekuja kutafuta pesa.

Tunaomba msaada japo tupewe mikataba angalau tufaidi keki ya Taifa, na tuna imani haya mambo Mh Rais hayatambui lakini kiuhalisia tunateseka mnooo humu ndani.
 
Back
Top Bottom