Valentine Story! Guess Who Is Getting Married? Marriage games

Agela nae akiwa kwake na mumewe kitandani, akawa anawaza na kuwazua yake. Akawaza tu, sawa kaolewa, mumewe ni mchapa kazi, ana biashara zake, ana hela kiasi, wana ishi neighbourhood nzuri, mtoto anasoma shule nzuri sanaa, watu wengi wanatamani wawe kama yeye, but deep inside her heart she is hurt and hurt deep.

Why hurt, siri yake kubwaaa hajawahi mwambia mtu, ni suspect zake ambazo zilikuja kuwa proved with time ni kwamba mumewe hampendi. Hajawahi kumpendaaa. Huo ndo ukweli mchungu. Ilitokea tu she was there, while the guy needed a wife after fatal breakup. Akakubali kuolewa hoping things will change over time but they didnt.

Akajua pale alipomzaa mtoto wao wa kwanza angeuteka moyo wa mumewe, na akaomba sanaa Mungu ampe mtoto wa kiume, lakini ikashindikana akajikuta kapata mtoto wa kike. Na mume alibadilika kidogo ila akarudia hali yake na kumfanya aishi empty as usual.

Tatizo lingineni swala la mumewe kutaka watoto wawili 2, jinsia yoyote itayoletwa na Mungu ni hao hao basi. Na hilo swala kamsisitiza mara kibao. Na wa kwanza alishazaa wakike vyovyote itakavyokuwa itatakiwa azae wa kiume. Hili limesababisha atoe mimba 3, sababu zote zilikuwa watoto wa kike na kumdanganya mumewe ni miscarriage za kawaida. Hili lilimtesa sanaa usiku, mpaka kuna mda kawaza kujiua, sema akimkumbuka huyu mwanae anavumilia.

Kikubwa kilichomfanya afikirie kuwa mumewe hampendi ni sababu their sex life is terrible. Mwanaume hana mzukaa kabisaaaa. Mpaka adai yeye tendo, tena kwa kubembeleza. Akaanza kuhisi mbali sanaa. Ila katika peleleza pelez yake akagundua mumewe anaendelea na gf wa zamani ambae walivoachana ndo akaolewa yeye, na huyo dada ni mke wa mtu pia.

Kumuuliza alitmani sanaaa, sema akayaogopa majibu, what if akimwambia ndio kweli na anampenda yule dada sanaa, kama vipi waachane atafanyaje? Hayupo tayari kuwa divorced, Au mwanae alelewe na mama mwingine. Familia hakuna talaka, hamna aelitalikiwa and her mama raised her better than that.

Kutafakari akaona bora tu ajifanye mjinga, ndoa iendeleee. Maybe and by maybe it means MAYBE fate will be kind mbeleni na yule mwanaume atajua nani ni bora kwake na mambo yatabadilika. Maisha yake ni ya kuishi kwa matumaini na kuingoja kesho maana leo ishaingia shubiri.

Kwa mumewe akawa na adabu zote, mtu wa maneno machache, hata akidanganywa safari anajua tu wapo hapa hapamjini anajinyamazia tu, akirudi anampa pole, Mtu wa kwenda kama hayupo ila yupo

Akajitafakaria tu mpaka lini hali hii. Akatafakari maybe aondoke na yeye kama Anny huenda akapata mtu mwingine wa kueleweka na akawa na furaha kama Anny lakini akaona she is not that strong. Kama ameweza kuvumilia miaka yote hio what is 1 more year? Akakata shauri aendelee kucheza the fools card.
 
Anny has always been a beauty, breath taking beauty. Kila mtu alikubali kuwa yeye ni mzurii mnoo. Mpaka mama yake akawa anawakere ndugu zake kwa kujitapa pale kwa Anny kazaa,kama mtoto tu, palekwa Anny alitulia kumzaaa. Na kila mtu kamkubali Anny ni mzuri.

Uzuri huu umemrahisishia sanaa maisha, kazi kapata kiurahisi, chochote akitakacho hajawahi kosa maishani mwake. Watu ni wakarimu kwake sababu ni mzuri sanaa, ofisini ana mashostiii kibao sababu wanapenda campani yake. Katembea hoteli nyingi mnooo, kafika sehemu nyingi, kala vingi sababu tu ya uzuri huu. Akawaza wazo linalo mjia siku zote, je asingekuwa mzuri angeishije ishije? Akamshukuru tu Mungu kwa uzuri wake.

Uzuri una gharama zake pia, umemcost vingi, ikiwemo kuolewa akiwa bado mdogo sanaa,miaka 23,na bwana wake wa chuo, waliomaliza wote. Sababu watu wengi walikuwa wnavutiwa nae, bwana wake huyoakaona amuoe jumla haraka haraka yeye Anny akiwa na miaka 23, na mwanaume akiwa na miaka 25.

At that time she was young, restless, and she thought it was cool, atasifiwa kama kawaida, kapendeza sanaaa, kaolewa mdogo, et. Ndo ikafungwa kanisani despite mama yake kumsisitiza huyo mwanaume hana kitu, ana jilostisha tu, angoje aende maofisini akapate maboss. Mama yake akijisingizia ugonjwa asiende tu kwenye hio harusi.

Pamoja na yote alimpenda sanaaa BF wake, na alikuwa mzuri, so wakiwa wote wanasifiwa ni wazuri sanaa. kila mtu alitamani kuwa yeye. The beauty of it allshe always cheated on him, so hata kwenye ndo she knew she will be a serial
cheater!

Too bad do hii ili dumu mwaka tu, na kuvunjika kiutani utani. Kikubwa kilichomshinda ni ugumu wa maisha na kumsikiliza mama yake. Mwanaume hakuwa na kazi nzuri, na familia yao haikuwa na uwezo mkubwa, ikawalazimu kuishi nje ya mji, maisha ambayo ni ya kawaida sanaaaa. Sasa Anny kwa ushangingi wake akapata kazi nzuri sanaa kwa wazungu, akajitahidi kumsihii mumewe wajitahidi kuishi kizungu maisha ya juu, ya kifahari kwa yeye Anny kugharamia.

Mumewe akaleta msimamo waisi maisha ya uwezo wao, uwezo wa mwanaume, hawezi kulelewa na mkewe. Anny kampenda na hayo ndo maisha yake inatakiwa arizike. Ukijumlisha na kelele za mama mkwe zaa, zaa, wajukuuu, zilimtibua kabisaaa akaweka vijiti 5 kisiri siri ikawa malumbano hayaishi na ndugu wa mumewe.


Huku kazini akaja mteja ana hela zake za maana, akamuelewa Anny, Anny akaacha kuvaa pete, akamwambia yupo single. Wakaaanza yao. Huku na huku mteja akamwambia Anny waishi wote Masaki kwenye apartment yake. Akaenda kwa mumwe kumuaga, ndoa imeishaaa. Mumewe akajua Anny anatania atarudi. Ndo hivo.

Mume akajua anaishi na kibuzi, kaita kikao cha familia kasamehe yote Anny arudi kwenye ndoa, Anny kasema sirudiii. Nimefika huku Masaki. Mumewe ana kazi ya kumbembeleza kila siku arudi, ndoa yao ya kanisani, haifutiki. Mume hajaoa mpaka kesho anamngoja Anny arudi nyumbani, anajua ni ulimbukeni utamuisha lakini hata wazo hanaaa.

Huyu pedeshee wa Masaki ni Mnamibia, kaishi sanaa nje, na bongo ni consultant wa multinational moja kubwa sanaaa, na anampenda Anny hakuna mfanowe. Ni aged kampita kama 12 years so ana mtreat kama kitoto. Atachotaka anampa. Na mda wote ni kumdekezaaa tu, kama haamini umri ule kumpata mtoto kama yule.

Na Anny anajua kupendwa na kupendeka. Basi ndo anamkolezaaa Daddy hakuna mfanooo. Kama mahaba ana mu overdose. Ile kupay attention, dady unkula nini, dady hapendi hiki, dady anependa hiki basi lazima kiwemo mezaniii. Dady ana meeting lazima suti ziagizwe mpya, daday ana homa, Dr. ataletwa kumpima kila kitu, simu za kumkumbusha Dady umekunywa dawa ni muhimu.

Japo kuna sehemu ya moyo wake ikawa inawaza huenda huyu Dady ana mke maybe familia huko kwao. Hakuwai kumuuliza, wala dady hakuwahi kusema, wakawa wanaishi tu kiutu uzima wanaelewana. Hakuna kuuliza lolote, wala kijibiwa lolote. We are here now lets love each other.

INAENDELEA.
 
THE WEDDING BELLS!

Siku hio wote wakawa wamkutana kwa Daddy kumfanyia surprise Anny. Wakawa wana hamu ya kujua ni surprise gani safari hiii, maana daddy kwa surprise hana mpinzani. Alisha msurprise gari, akamsurprise birthday, akamsurprise shares, yaani kwa hawa wawili surprise haziwaishii kiukweli.

Basi kufika wakakuta Decor, na watu wa catering, wakawa wanajiandaa na hio surprise. Anny karudi wak msurprise akafurahi kinomaaa, wakala na kunywa hatariii. Akawwambia mashostize huyu dady leo ananisurprise nini, ukute ndo ananitimua kwa party hahahaaaaa.

Mda ulipofika Dady kapiga goti, na pete ya tanzanite will you marry me Anny? Akatoaje Yes fastaaaa. atu wote wakashangilia kasoro Sisca, ambae aliwaza na kuwazua ndo ya 2 hio kwa shoga ake yeye hata moja bado. Akawa anatamani kumfuahia shoga ake ila furaha hanaaaaa.

Basi Anny ndo kukeraa ni vipi sasa, engagement mda huo huo ashaanza i want a beach wedding, oooh my God, i always wanted a beach wedding. Or we can go and marry in Dubai kama wanaigeria, au Paris, oooh my God. This time i can afford a designer gown, who shoul i wear? Vera Wang? or Valentino? I dont know.

Sisca akaondoka mdogo mdogo na mawazo akiwaza dunia ilivo na upendeleo. Hakupata usingizi kabisaaaaa usiku huo.

Angy akarudi kwake akiwa kasahau kama hakumuaga mumewe, akajua mumewe hatogundua hata kama kachelewa wala hatojaliii hata akijua. Kinyume na matarajio yake kamkuta kuraaa kam Cobraaa. Ulikuwa wapi, mwamke gani hujafundwa, ndio nini sasa? Akawa kashavurugwa na ishu ya Anny kuolewa tena na yeye kuishi kwa manyanyaso afu mwanaume anamwambia nini.

Akamjibu tu, nilikuwa kwenye engagement ya Anny, samahani sikuaga. Mume kaja juu kama moto wa kifuu, ndo anakwambia na wewe uiache hii ndoa yako upate mwanaume mwenye hela sio, sasa sikia rudi huko huko kwa Anny hapa kwangu sikutaki tenaaa! Khaaaaa! Akamjibu tu, wewe kama umeamua kurudiana jumla na ex GF, mmeona ku cheat haiwatoshi, kunifanya mimi mjinga haitoshi, sema tu ni mambo umeamua, wala usimsingizie Anny, wala usifanye kuchelewa ndo sababu. Mi naenda kulala na nitaendelea kujifanya sioni kama kawaida. Mwanaume akashtukaaa, na kupoa ghaflaaa! Baada ya mda akajikusanya kusanya eti Ajitia kukanusha. Hisia hisia zako hizo zitakuponza, mimi mke wa mtu wa nini wakati nina mke wangu wewe apo.

Akwambia wewe jua mi najua, na sijajua leo wala jana, safari zako zamikoani bahari beach nazijua zooote. Nimemuachia Mungu, iko siku Mungu huyu huyu ninae muabudu atakuabishaaaa Mchana kweupeeee jua linawakaaaaa. Na mimi nitakuwpo hapa hapa kushuhudia ukiumbukaaaa. Mi nalala sitaki maneno.

Mwanaume akaingia kabatini akaweka nguo zake kadhaa akaondoka usiku huo wa saa 7. Angy akajua tu ndoa ndo imeishia hapooooooooo! Akajilazaaa tu akihesabu paa, hata lepe la usingizi halikumpitia.

ITAENDELEA
 
More and more mystrey!

Siku hio ana hili wala lile, kaenda kwenye meeting Sisca, akaona akae restaurant ya hapo hotelini amngoje Angy, manake jana yake alimwambia the marriage is so bad, she knew the marriage was on the rocks before, but it could be the real end this time.

Akawa anamuonea huruma Angy, how she is bottling up every thing, and trying to hold on over the years. Akawa anawaza na kuwazua. Aksikia habari yako, can i give you company! Kucheki hivi mkaka wa maana, kapiga suti, and there was some ellegance and class about hima akajikuta tu kawa mkarimuuu.

Kutambulishana akamwambia yeye ni lawyer, kumcheki kidoleni bonge la peteeee ya ndoa, akajua tu ngoma ya kitoto haikeshi. Basi wakaongea ongea na nini, wala haa hakumficha, akamwambia tu, yuko married with 2 kids, mkewe anafanya kazi bank. Hivo yaani.

Basi baadae Angy akawa kaja, yule kaka akaaga akamuachia business card yake. Akaipokea akawa tu kaiweka mezani. Basi Anny anamwambia waoooh, he is cute, so cute jamaniiii. Akamjibu tu he is married as shit. Angy akatikisa kichwa tu.

Ndo kumpasha kuwa jibaba limehama nyumbani siku ya pili, yupo mwenyewe na mtoto. Bado hajapata akili afanye nini. Yani network bado haijarudi kabisaaa. Akawa anamwambia tu ningeondoka ila ada zenyewe ghali sanaa, afu mwanangu atateseka sanaa, maana hawa wanaume kama wa kwangu ukisema uondoke akufate utachora chini, labda anaombea leo kesho niondokeee, kuondoka ndo nimemrahisishia kazi.siondoki pale, kodi atalipa na ada atatoa. Hata kama hanitaki najivictimise yeye ndo mkosefu, mi namwangalia tu.

Sisca akamwambia sasa shoga si utaborekaaa, ujana unakupita waiting in vain for some one you are not sure. Bora utafute kazi uwe unatoka asubuhi umeoga angalau na kupendezaaa, walau utakutana na wanaume wengine na watu wengineee, kuliko kukaaa nyumbani unawazaaa tu, utapata alcers. Angy akaona hilo litakuwa swala la msingi sio kidogo.

Wakakata shauri wamwambie Anny aongee na dady kazi ipatikane, maana ana network kubwa. Anny akasema haina neno atampanga Daddy kama kwaida, haitoshindikana jambo. Wakiwa wanaondoka Sisca akaiacha ile business card pale mezani. Angy akamkumbusha umeacha business card ichukue tu, huwezi jua, akamwambia achana nayo. Drama drama za side chick siziwezi. Mburaaaaah! Wakaondoka wakiwa wameiacha pale mezani.

Angy kufika nyumbani, dada wa kazi anamwambia Baba karudi yupo ndani! Mmmmmmh! Nini? Baba karudi yupo ndani. Eeeeeehhhhhh! Hajaniulizia? Kakuulizia nikamwambia umetokaaa. Tobaaa! Ngoja niende huko ndani. Akafika za mda baba flani. Salama tu mama flani, nimerudi. Akamjibu nakuona umerudi, karibu sisi tupo. Mumewe akamtwanga swali, huniulizi nilikuwa wapi? Akamjibu aaah bwana nikuuulize ulikuwa wapi, hapa kwako bwanaaa unakuja mda wowote unaojisikia na kutoka mda unaojisikiaaa, mtu chake, hata ukikuta mlango umefungwa we vunja tuuu, si wako bwana unaulipia kodi, hakuna atakae kuuuliza. Kweli mke wangu unanijibu hivooo?

Sasa nikujibu vipi, sio kwako hapa? Wewe mtu mzima. Ukienda mahali umeamua sio mtoto kama huyu Melissa wetu useme anakosea nimkanye, au hajui alitendalo, wewe ukifanya lolote ni maamuzi binafsi tu. Nishakwambia knock your self out. Mi wala hunistui, siku ingine kaa mwezi, kaa mwaka utajua mwenyewe ukirudi utanikuta hapa nafanya kazi yetu ya kushirikiana kumlea huyu mtoto, sababu kesha kosa baba, inabidi niwe baba yake na mama yake, nitafanyaje sasa.

Mwanaume akakaa kimyaaa kwa mda. We endelea tu na huo mdomo wako, iko siku utakipata unachotafutaa, nitakupa unachonitafuta. Akataka kunyamaza ila akaona vimemkaba sanaaa bora tu atapikeee. Nachokitafuta kishakushinda siku nyingiiii sanaaa kunipaaa, sema vile nina roho ya kuridhika navumilia.

Mi namna hii nyumba itanishindaa, unakuja nyumbani uwe na furahaaa, amani, upendo inakuwa majunguuu majunguuu na kashfaaa! Mi mambo ya uswahili sipendiiiii. Vitu unahisi hisi tu ndo kujiaminishaaa moja kwa mojaaaaa. Hivi huwazi maybe just maybe there is 0.0001 chance you are wrong amd it is all your imigination? Hivi ukijua umenikosea sanaa utafanyaje? Mwanaume kabwatukaaaaaa. Angy kaamua tu kumpa jibu la mjinga ambalo ni kumkalia kimyaaa.

Anny akawa kamtext kazi imepatikana ofisini kwa Dady. Akaona asimtibue zaidi yule mwanaume atampa hio taarifa ya kuanza kazi siku ingine.
 
The power of new beginings!

Anny aakawa yupo busy planning the big day, akawa kashaongea na dady aende U.s kuangalia designer colections za msimu huo. Daddy akawa kakubali kabisaaa. Na akawa ana debate afanye beach wedding au destination wedding.

Wakawa wamekutana for brunch kujadili what colors, sare, decor na mambo kama hayooo. Basi wakajadili pale sababu hela ipo, kila kitu kikawa kinaenda fresh. Baadae ndo kumuelezea ile kazi ipo ofisini kwa dady. So atalipwa vizuri, na hakutokuwa na ishu yoyote wala nini.

Angy ndo akamwambia Anny, Sisca met this guy he was cuteee! Way too cute sema kampotezea coz he is married. Anny akawa anampa tu, we jilegeze utazeeka nyumbani, ndoa kwa mkewe kwani wewe tatizo lako nini? Kama ingekuwa yeye Anny, anavoona angeungana na Johny deep kwenye usemi wa "If there is a man who is inlove with 2 women, and has to chose, he really loves the second because if he loved the first he will never have noticed the second. So anachezea bahati, mtu anaweka ndoa yake kwenye line ili wawe wote bado anaona hiko ni kitu kidogo olaaaaaaaa!

Wakaongea pale na kuhusu mume jeuri wa Angy, akawa anawaambia siku hizi namjibujeee, nampa za uso, hata simuogopi, akinianza tu nammalizia. Hahahaaaaaaa! Wakacheka. Anny akamwambia wewe jibu sanaaa tu, siku ukute bag yako iko nje. Hahahaaaaaa! Akamwambia weeeee, navunja mlango. Asintanieee.

Baadae wakaagana kila mtu akarudi ofisini, Angy akarudi nyumbani kumpeleka mtoto piano classes. Sisca kufika ofisini akaambiwa kuna mgeni wako alikujaa. Akajua wa kikazi. Akauliza nani, akambiwa flani! The maried guy! Akastukaaa! Akauliza alisema anataka nini? Akaambiwa hajasemaa but kasema atarudi tenaaa. Akamwambia akija mwambie sipo.

Mda wa kutoka anashangaa anaitwa Siscaaa, kugeuka the married guy, akajibalaguzaa. Akaulizwa why are you avoiding me? Tuko na tatizo? Akajikosha hapanaaa, didnt know it was you. Basi MBA (Married but available) hakukawiza akamwambia lets go for drinks somewhere. Sisca akamwambia tu, well natamani but i cant , sipendi drama, tunaweza kukutwa tumekaa, nikapigwaa, kutolewa kwenye tabloids, i really pass.

MBA anakomaa sio kihivooo, i just wanna talk and be friends, sipo huko ulipo! We can go somwhere my wife hatogundua. Hiiiiiii! Trust me. Alingangania sanaa akaamua tu aende akasikie hilo la huko. Kufika kule, he was really nice, and she missed company kiukweli. Ukizingatia the guy was hot, watu wanangali mambo yakawa bambam. Tofauti alivohisi ataboreka akajikuta kaenjoy kichiziii. Story hii, story hii,mara wacheze music saa 7 hii hapa. Wakaagana. Ila MBA safari hii alijibipu na simu ya Sisca.

Akarudi home hoiii, akiwa kachangamka lakini full of life. Akakuta missed call 6 za Anny. Akasema atampigia kesho. Mara Anny akapiga, you are such a slut my friend, nimekuja ofisini nilitaka unisindikize mahali, nikakuona na MBA, ooh my God, he is cute, nikajibanzaa tu sikutaka kuharibu picha. Nikawaona mnaongozanaa, please tell me you got laid! You cant pass that di.ck. It is evil! and dispeakable! Hahaaaa! Akamwambia hamnaaa we just talked! Anny anagomba talk what bwanaaa, mume wa mtu ukimpata jivinjari, hana time na wewe jivinjariiii, anakudanganya jivinjariii. Sisca anamwambia it is not good, ana mkewe. Anny anakuja juu mke kitu gani wewe, wewe mambwana wangapi umeporwa mpaka leo hii? Ishu kuporana mabwanaaa. Mke mwenyewe alimpora kwa mtu, wewe unamdokolea yeye, hivo hivo siku zinaendaaa. Hahaaaaa! Wakacheka tuuuu. Anny anamwambia if you werent too proud you could be having a di.ck right now, hot sexy, steamy night, ila sababu ni zobaa lala bwanaaaa. Mi nishaukalia wa daddy round 1 kiuno chote hoiiii nangoja round 2. We lala na kikoko hicho ndo ushaharibu. Hahahaaaa!

Angy huku mume karudi na mshawasha akawa anamwangalia tu, mume kakumbuka zawadi ya mtoto siku hio, anauliza nini kimeisha kwenye friji, rangi imechakaa hii, kesho nitamleta fundi sijui nini. Sababu anajua atamtibua na kwenda kazini asubuhi, akaona usiku huo ampozee kwanza. Basi akawa ane anacheka na kujiongelesha, kama yamekwisha kabisaaaa. Hadi wanataniana.

Akwa anawaza tu, kweli siku hazifanani, siku zingine Mungu anakuona kama hivi, siku zingine shetani anakukalia kooni basi tabu tupuuu. Hapa mambo yakienda vizuri huenda nikapewa mechi leo, sijuiiii, ngoja nijioneee. Akamtengea chakula fresh, basi anasifia hiki chakula umepika mke wangu kitamu sanaaa, unajua kupikaaaa.

Hakufanya ajizi wala nini, kaenda kuoga fastaa, kajifukizaa marashi, akataka kuvaa bikini set akaona akishushuliwa ataumbuka sanaaa. Akaona tu bora avae dira, maana aibu zingine za kiutu uzimaaa. Akawa kajilaza anasoma gazeti la mwaka arobaini na sabaaa. Anazuga tuuu.

Baba la baba kaja, straight bafuni, wala hakuchukua taulo katoka huko moja kwa moja kitandani, kaanza kuushika mzigo mwenyewe bila mizunguko. Sababu nae Angy nae alikuwa kammiss, akaonesha ushirikiano wa hali ya juu. Mechi kali ikachezwa. Kama sio wao waliotifuna juzi. Saa kumi kamshwa tena mzee anataka cha asubuhiii, kama kawaida bila hiyanaaa kaonesha ushirikiano. Baadae baba la baba kaenda kuoga, Angy nae bafuni humo humo, baba la baba akajua mahaba niteketezeaaa, kampa kingine cha bafuni, akajua wakitoka kuoga hoi atalala, ili baadae amuandae mtoto shule, manake yeye anadamka ga sanaa kuwahi kazini.

Wanatoka kuoga anaona mtu anatoa seti mpya ya chupi za maana na sisiria anavaa. Akashtuka kwanzaaa, akaamua akae kimya. Anaona mtu anajipaka mafuta hana stress, akakaa kimya, akaona anajipaka foundation, make up, ikabidi amuulize hizo date zenu za umbea umbea mmenza kukutana alfajiriii? Mbona unavaa, unajiandaa, mimi nitakuja kukukataza haya mambo ya mashoga, alfajiri yote hii unaenda wapi.

Akamwambia mi naenda kazini, nimepata kazi. Mwanaume kadakia nini? Unasemaje? Nimeanza kazi ndo naenda ku report. Hahahaaaa! Akacheka, huo umbea wenu sasa too much mpaka alfajiri au mnaenda kuniloga kwa mganga leo, anajitia kutania tania. Angy akavaa kisuti kifupiii juu ya chupi tuuu, bila tight wala nini. Mumewe anamuangalia tu. Hivi kweli unaenda kazini? Ndio kweli baby nimepata kazi. Na hukuona umuhimu wa kuniambia au kujadili hio kama mumeo humu ndani? Angy akakaa kimya. Sasa mimi mumeo nasema hakuna kufanya kazi. Huli humu ndani? Huvai? Husuki nywele za gharama? Sikupi hela za kuchezea kwenye botiques. Mimi kama mumeo nasema vua nguo ulale hapo, na kulea mtoto.
Angy akajipulizia perfume, akanyanyua mkoba, akamwambia baby tusigombaneee, kuna leo na kesho, leo upo nashukuru sijawahi kupungukiwa, ya kesho anayajua Mungu, kazi ni jamba la neema, tuna mtoto huyu huwezi jua, sikukwambia kwa mambo kama haya, badala ufurahi mkeo naenda kazini, hata ukikwama nitakuwepo kukuboost, lakini ndo hivoo kashfa juu ya kashfa. Mi naenda bwanaaa. Kwa hio ndo unaenda kuanza kazi na bikini tupu ndani ya kimini afu mume nikae nafurahiii, unanikalia kichwaniii si ndiooo, wewe nenda ka resign tu, huu mjadala haujaisha.

Akamuacha dada maelekezo cha kufanya, huyooo ready for the first day in the office.

ITAENDELEA SAA 1 USIKU.
 
Sawa Lara tutafanyaje sasa na stori imenoga tunaitaka..Ngoja tukapike kabisa.
 
Back
Top Bottom