Huna tofauti na mtu anayetaka tanzania tuhalalishe uuzwaji wa bangi sababu eti nchi nyingine wanaruhusuUbaguzi tu kwa walimu, mbona madaktari, manesi, wanajeshi, polisi, migambo, mapilot, wafanyakazi wa benki, bot, zimamoto, uhamiaji, Tanesco, wanavaa kwanini sisi wanatukatalia kuvaa? Tunataka sare.
Unaonaje hizo pesa za sare serikali ikanunua madawati shuleni??madai ya msingi ya walimu ni sare??SARE ni nzuri,itasaidia kuondoa hisia za unyanyampaa wa kimavazi kuambiwa unavaa nguo hiyohiyo,kauka nikuvae wiki nzima,wakati wenzako wanabadilisha kila siku.
vaa mwenyewe aiseeUbaguzi tu kwa walimu, mbona madaktari, manesi, wanajeshi, polisi, migambo, mapilot, wafanyakazi wa benki, bot, zimamoto, uhamiaji, Tanesco, wanavaa kwanini sisi wanatukatalia kuvaa? Tunataka sare.
Ubaguzi tu kwa walimu, mbona madaktari, manesi, wanajeshi, polisi, migambo, mapilot, wafanyakazi wa benki, bot, zimamoto, uhamiaji, Tanesco, wanavaa kwanini sisi wanatukatalia kuvaa? Tunataka sare.
Mbona Libermann pre and primary walimu na wafanyakazi wote wanava sare? Hakuna shida hapo sema kwa huku serikalin wamalize kwanza matatizo ya msingi ndo waanze mbwembwe.Si kweli kwamba ni ya kudhalilisha....Nchi za wenzetu mfano Mozambique walimu wanavaa overcoat km za madaktari na kwa kweli zinaongeza heshima.
Ha ha ah yani una maana kuwa ile taarifa ya sare ni feki na hii ya kukanusha ni feki. Duh!! Bongo mm nawaza tu NSSF daah!! TanzaniaaaMaajabu ya Tanzania unaeza kukuta hata hii taarifa ya kukanusha nayo ni feki....
Hili kanusho ni la uongo.. Tupe source yake.. Nembo yenyewe imefifia inaonekana watu walii google tuYAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.
Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016